Ghana:Uzinduzi wa Ujenzi wa Kanisa Kuu la Kidini ni ishara ya Umoja wa Taifa!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mji mkuu wa Ghana hivi karibuni utaona ujenzi wa Kanisa jipya Kuu la kwanza Kitaifa kwa ajili ya kidini ambalo ni ishara ya umoja wa Nchi hiyo na ambao ni mpango wa ushirikiano kati ya Serikali na viongozi wa Kidini katika Nchi hiyo, miongoni mwa viongozi wa Kidini ni Askofu Mkuu mstaafu Charles Palmer – Buckler wa Jimbo Kuu Katoliki Accra. Shughuli za ujenzi huo limezinduliwa rasmi tarehe 6 Machi katika maadhimisho ya mwaka wa 63 wa Uhuru wa Ghana. Siku moja kabla ya siku kuu ya Huru kwa mujibu wa Shirika la Habari Katoliki, walifanya hafla fupi ya kuweka jiwe la kwanza la msingi kutoka Nchi Takatifu Yerusalem. alilokabidhi Balozi wa Israeli Bwana Shab Coope kwa Rais wa nchi ya Ghana, Bwana Nana Addo Dankwa Akufo- Addo ambaye ni mdau mkubwa wa kuanzisha tukio la ujenzi huo na ambaye mwanzo alikuwa amesema kwamba “ni shukrani kwa Bwana kwa ajili ya baraka na neema ambayo taifa hili limepokea”. Katika hafla hiyo kulikuwa na viongozi wawakilishi msingi wa mamlaka ya raia na kidini.
Kanisa Kuu hili la Muungano wa Kidini Kitaifa litakuwa na mchanganyiko wa ujenzi wa kisasa ambao utawakilisha ishara za kikristo na nyingine za urithi wa utamaduni mahalia na ambalo litaweza kuwa na uwezo wa nafasi ya watu elfu tano kwa mujibu wa mkandarasi wa ujenzi, Bwana David Adjaye Obe. Jengo hili pia litakuwa na vikanisa vidogo vidogo vya ndani; kisima cha ubatizo na jumba la maonyesho ya Biblia; shule ya muziki na sehemu ya nafasi za picha za kisanii. Yote hayo yametafakariwa kwa kina kama ishara za umoja, maelewanao na roho ya watu wa Ghana. Kanisa Kuu hilo litakuwa ni eneo la kitaifa nchini Ghana ambapo waamini wake wote wa madhehebu yote ya kikristo katika nchi wataweza kuungana kwa pamoja katika kuabudu, kusifu, kutafakari na kuadhimisha liturujia na ibada za mazishi . Aidha Kanisa kuu hili litakuwa linatumika kufanya maadhimisho rasmi ya misa za mazishi kitaifa na sherehe mbalimbali za kutoa shukrani.