Tafuta

Vatican News
Wosia wa Kitume wa Papa Francisko baada ya Sinodi unajikita katika masuala mengi ambayo yanatazama ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja Wosia wa Kitume wa Papa Francisko baada ya Sinodi unajikita katika masuala mengi ambayo yanatazama ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja 

Australia:Querida Amazonia inawatia moyo na changamoto kwa Kanisa la Australia!

'Querida Amazonia' inatia moyo na changamoto kwa Kanisa la Australia kwa mujibu wa Askofu Mark Coleridge Rais wa Baraza la Maaskofu Australia,akielezea juu ya Wosia wa Kitume Baada ya Sinodi uliotolewa tarehe 12 Februari 2020.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mark Coleridge Rais wa Baraza la Maaskofu Australia, akielezea juu ya Wosia wa Kitume wa Papa Francisko baada ya Sinodi “Querida Amazonia”, iliotangazwa tarehe 12 Februari 2020 anasema kuwa hati hiyo haitazami Kanda moja tu ya mbali duniani, lakini ina mambo mengi ya kusema hata kwa Kanisa la Australia.  Askofu amesema: “Amazonia iko mbali sana nasi lakini matatizo yake yanafanana nasi”. Kwa namna ya pekee, “masuala muhimu yaliokabiliwa katika Sinodi na Hati ya Kipapa, kuhusu utamaduni wa watu asilia na uwelewa fungamani wa kiekolojia, vinastahili umakini na kipaumbele katika muktadha wa Australia”, amesisitiza Askofu.

Kama ilivyo Amazonia, hata Australia wanafanya uzoefu wa kwa namna ya janga kubwa la motot, uharibifu wa mazingira ya asili na si tu katika mazingira lakini pia hata kwa wanyama na bayoanuai, juu ya jumuiya na kwa watu wengi. ‘Querida Amazonia’, anathibitisha Askofu wa Brisbane  kama alivyosisitiza Papa Francisko kwenye wosia wake wa  Laudato Si, kuhusu uwajibikaji wa Kanisa wa kutunza nyumba yetu ya pamoja , ambao unahitaji ujasiri katika mafundisho ya kipapa katika mantiki maalum”.

Kwa mujibu wa Askofu Coleridge anaonesha   umakini wa Papa kuhusu utamaduni wa watu asilia katika Amazonia ambao pia unatazama kwa namna ya pekee  hata Australia  kwa kufikiria hali mbaya ya ukosefu wa maendeleo  ili kuweza kukidhi pengo kubwa lililopo la uchumi kijamii , kati ya watu wa asili na wasio asili nchini Austalia. Kutokana na kesi kama hiyo ndiyo changamoto kubwa  na kuwatia moya Kanisa la nchi yao pia. Rais wa Baraza la Maaskofu Austalia pia amebainisha juu ya mwaliko wa Papa Francisko kwa maaskofu wote duniani kuweza kusaidia Kanisa la Amazonia ili kuondoa pengo kubwa lililopo la ukosefu wa makuhani.

Kama Australia anasema wazo  hili linaweza kuanza kupitishwa siku, wiki , miezi au miaka bila hata  waamini kupata Ekaristi takatifu na ni ngumu kutambua. Watu wa Amazonia wana uchungu mkubwa. Vile vile Askofu Mkuu ameelezea juu ya umuhimu wa huduma ya walei ambao wako mstari wa mbele katika masuala ya Kanisa, na nafasi ya watawa na mashemasi wa kudumu katika Kanisa la Amazonia.  Ikiwa kila mmoja anajikita kuwa sehemu na kufanya sehemu yake, ushuhuda kwa namna hiyo wa Kanisa unakuwa na nguvu zaidi.

13 February 2020, 17:17