Tafuta

Vatican News
Baada ya mwezi kupiai wa kimbunga Kenneth nchini Msumbiji bado ni dharura Baada ya mwezi kupiai wa kimbunga Kenneth nchini Msumbiji bado ni dharura  (ANSA)

MSUMBIJI:Bado ni dharura ya kibinadamu baada ya mwezi kuhusu kimbunga Kenneth!

Matumaini,amani na upatanisho ndiyo kaulimbiu iliyochaguliwa kuongoza ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Msumbiji mwezi Septemba mwaka huu.Licha ya hayo hali ya nchi ni ngumu katikati ya nyumba ambazo hazina paa na utapiamlo.Kwa maana hiyo bado kuna dharura ya kibinadamu baada ya mwezi wa kimbunga Kenneth.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Matumaini, amani na mpatano ndiyo kauli mbiu iliyochaguliwa kuongoza ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Fracisko nchini Msumbiji. Kauli mbiu hiyo inakumbushwa na ujumbe wa Maaskofu wa Musumbiji kuhusu ziara hiyo inayotarajiwa mwezi Septemba 2019 katika nchi tatu. Katika ujumbe wa maaskofu wanasema, matumaini, amani na mpatano yanaleta mwangwi mkubwa katika mioyo ya wote kwa sababu yanatia moyo wa kuweza kushinda kwa ujasiri kadha iliyosababaishwa na kimbunga cha kitropiki na ili kuweza kukabiliana kwa imani na matumaini hasa pia hali ya matatizo ambayo kwa sasa watu wanakabiliana nayo katika Wilaya ya Cabo Delgado, kutokana marudio ya mara kwa mara ya mashabulizi ya kisilaha yanayosababishwa na makundi ambayo hayatambulikani rasmi na serikali.

Maandalizi kiroho kwa ajili ya Papa kwa kuongoza na matumaini, amani na mapatano

Na ili kuweza kufanikisha ziara hii ya Baba Mtakatifu Francisko na ikiwa kipindi cha neema, maaskofu wansema, “ tuna haja ya watu wote kujiandaa vema kiroho”. Kwa maana hiyo  maaskofu hao wameamua kuwa mwezi Julai na Agosti katika majimbo ya Msumbiji kuwa na  vipindi maalum vya sala. “ Ili kuweza kufanikisha hili, maparokia yetu na jumuiya watafanya vipindi vya sala na tafakari juu ya kauli mbiu ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko ili kumwomba Bwana kwa njia ya ziara ya Baba Mtakatifu atujalie neema ya amani na mapatano. Na Mama Maria mkingiwa dhambi ya asili na msimamizi nchini Msumbiji aweze kuwaombea na kuwasindikiza katika maandalizi ya ziara hiyo.

Tarehe za ziara ya Baba Mtakatifu Francisco barani Afrika

Ikumbukwe kuwa Baba Mtakatiffu Francisko anatarajia kufanya ziara yake ya kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius, kuanzia tarehe 4-10 Sepemba 2019. Anafanya ziara hiyo mara baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa wakuu wa nchi na maaskofu wa nchi hizo zote, ambapo ataweza kutembelea miji ya  Maputo Msumbiji, Antananarivo nchini Madagascar na Port Louis huko Mauritius. Hata hivyo ratiba nzima ya ziara yake itatolewa muda mwafaka.

Matumaini, amani na mapatano ndiyo kauli mbiu ya ziara ya kitume nchini Msumbiji

Matumaini, amani na mapatano ndiyo kauli mbiu inayoongoza  ziara ya kitume ya Papa nchini Msumbiji. Katika ramani ya nchi inaonesha, Baba Mtakatifu na njiwa ikiwa ni ishara ya amani. Mikono miwili inamaanisha makaribisho ya nchi ya Msumbiji kwa Baba Mtakatifu na hata ujumbe wa matumaini, amani na mapatano unaobebwa na watu wa msumbiji. Wakati huo huo rangi katika nembo zipo tano za bendera ya Msumbiji. Kijani inamanisha matumaini, nyekundu ina maana ya mapatano na rangi nyeupe ina maana ya amani, wakati rangi ya njano ikimaanisha rangi ya Vatican.

Zimechangwa dola bilioni 1.2 katika mkutano wa ufadhili Msumbiji

Hata hivyo kuhusiana na hali halisi nchini Msumbiji jumla ya dola bilioni 1.2 zimechangishwa mjini Beira katika mkutano wa kimataifa wa siku mbili wa ufadhili kwa ajili ya ujenzi mpya wa kijamii, uzalishaji na mioundombinu nchini Msumbiji baada ya taifa hilo kuathirika vibaya na vimbunga mapema mwaka huu. Msumbiji inahitaji dola bilioni 3.2 kwa ajili ya kuyasaidia majimbo yaliyosambaratishwa vibaya na kimbunga Idai na Kenneth ya Sofala, Manica, Tete, Zambezia, Inhambane, Nampula na Cabo Delgado. Katika mkutano huo wa kimataifa ulioandaliwa na serikali ya Msumbiji na kuwezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, Muungano wa Ulaya na Benki ya Dunia miongoni mwa waliochangia kiasi kikubwa cha fedha ni Muungano wa Ulaya ambao umetoa dola milioni 200, kati ya hizo dola milioni 100 zinatoka mfuko wa tume ya Muungano wa Ulaya na milioni 100 zingine kutoka Benki ya uwekezaji ya Ulaya.

Katika mkutano huo uliowaleta pamoja takribani washiriki 700 kutoka mashirika ya kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres uliosomwa kwa niaba yake umesema pamoja na mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF kutoa dola milioni 24 hapo awali na hata Umoja wa Mataifa kuzindua ombi la msaada wa kibinadamu la dola milioni 282 ambalo limefadhiliwa kidogo sana bado mamilioni ya watu Msumbiji wanahitaji msaada, tunakabiliwa na changamoto kubwa, mahitaji ya msingi ya watu hayafikiwi, hatari ya kulipuka  magonjwa iko dhahiri na athari kubwa za kutokuwepo na uhakika wa chakulakutokana na kupotea kwa mazao wakati wa vimbunga.”

Umoja wa mataifa kuongeza juhudi zake kwa ajili ya athari za msumbiji

Bwana Guterres amewashukuru wote waliotoa mchango na kurudia wito wake wa ukarimu zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa , kwamba: “Huu ni wakati wa kudhihirisha mshikamano wetu na nchi ambayo imeathirika na moja ya majanga makubwa na mabaya kabisa yanayohusu hali ya hewa katika historia ya Afrika, majanga ambayo pia yanatuonya kuhusu kuchukua haraka hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.” Katibu Mkuu pia ameahidi kwamba Umoja wa Mataifa utaongeza juhudi za kushughulikia athari za muda mfupi na za muda mrefu za majanga, na kwamba msaada wa dharua wa kibinadamu sasa utageuka polepole na kuwa wa ujenzi mpya na kusaidia juhudi za serikali za kuiendeleza mbele nchi hiyo katika masuala ya maendeleo.”Ujumbe wangu uko bayana Umoja wa Mataifa na kamwe hataipa kisogo Msumbiji.”

Kisiwani Madagascar ni "mpanzi amani na matumaini"

Mpandaji wa amani na matumaini ndiyo kauli mbiu itakayo ongoza ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kisiwa cha Madagascar. Katika nembo ya nchi inawakilisha mnazi wa msafiri, mafuta na mbuyu. Hata hapa inaonesha Baba Mtakatifu na baadhi ya watakatifu, mashahidi wa nchi, wamisionari na mashuhuda wa imani hadi kifo dini.

Katika nembo ya Mauritius ya ziara ya Papa anaongozwa na kauli ya mhujaji wa amani

Na kwa kuhitimisha na kauli mbiu za ziara nchini Mauritius, “Papa Francisko ni mhujaji wa amani”, ndiyo maneno yaliyo chaguliwa kutengeneza kaulimbiu ya ziara yake huko Mauritius. Katika Bendera ya Mauritius,inaonesha Papa akiwasalimia watu!

https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2019-03/mwezi-septemba-papa-anafanya-ziara-nchini-msumbiji-madagascar.html

03 June 2019, 14:39