Tafuta

Vatican News
Nembo zinazo ongoza ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji,Madagascar na Mauritius kuanzia tarehe 4-10 Septemba 2019 Nembo zinazo ongoza ziara ya Papa Francisko nchini Msumbiji,Madagascar na Mauritius kuanzia tarehe 4-10 Septemba 2019 

Mwezi Septemba Papa anafanya ziara nchini Msumbiji,Madagascar na Mauritius

Dkt. Alessandro Gisotti,Msemaji Mkuu wa mpito wa vyombo vya habari Vatican,ametoa taarifa kuwa,Papa Francisko atafanya ziara yake ya kitume nchini Msumbiji,Madagascar na Mauritius,kuanzia tarehe 4-10 Sepemba 2019

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa mpito wa vyombo vya habari Vatican,Dkt Alessandro Gisotti, tarehe tarehe 27 Machi 2019 ametoa taarifa ya kwamba Baba Mtakatifu Francisko atafanya ziara yake ya kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius kuanzia tarehe 4-10 Sepemba 2019. Dkt. Gisotti anathibitisha kwamba:"kwa kupokea mwaliko kutoka kwa wakuu wa nchi na maaskofu wa nchi hizo zote, Baba Mtakatifu Francisko atatimiza Ziara yake ya Kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius kwa kutembelea miji ya  Maputo Msumbiji, Antananarivo nchini Madagascar na Port Louis huko Mauritius". Hata hivyo ratiba nzima ya ziara yake itatolewa muda mwafaka.

Matumaini, amani na mapatano ndiyo kauli mbiu ya ziara ya kitume nchini Msumbiji

Matumaini, amani na mapatano ndiyo kauli mbiu inayoongoza  ziara ya kitume ya Papa nchini Msumbiji. Katika ramani ya nchi inaonesha, Baba Mtakatifu na njiwa ikiwa ni ishara ya amani. Mikono miwili inamaanisha makaribisho ya nchi ya Msumbiji kwa Baba Mtakatifu na hata ujumbe wa matumaini, amani na mapatano unaobebwa na watu wa msumbiji. Wakati huo huo rangi katika nembo zipo tano za bendera ya Msumbiji. Kijani inamanisha matumaini, nyekundu ina maana ya mapatano na rangi nyeupe ina maana ya amani, wakati rangi ya njano ikimaanisha rangi ya Vatican.

Kisiwani Madagascar ni mpanda amani na matumaini 

Mpandaji wa amani na matumaini ndiyo kauli mbiu itakayo ongoza ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kisiwa cha Madagascar. Katika nembo ya nchi inawakilisha mnazi wa msafiri, mafuta na mbuyu. Hata hapa inaonesha Baba Mtakatifu na baadhi ya watakatifu, mashahidi wa nchi, wamisionari na mashuhuda wa imani hadi kifo dini.

Katika nembo ya Mauritius ya ziara ya Papa anaongozwa na kauli ya mhujaji wa amani

Na kwa kuhitimisha na kauli mbiu za ziara nchini Mauritius, “Papa Francisko ni mhujaji wa amani”, ndiyo maneno yaliyo chaguliwa kutengeneza kaulimbiu ya ziara yake huko Mauritius. Katika Bendera ya Mauritius,inaonesha Papa akiwasalimia watu!

27 March 2019, 14:06