Ethiopia:Vijana wasaidiwe kupata elimu na fursa za ajira ili wabaki nchini mwao!
Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Katika mkutano kati ya Waziri wa Mkuu wa Jamhuri ya Hungari na Kardinali Berhaneyesus Souraphiel, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Addis Ababa nchini Ethiopia amesema kuwa taifa la Ethiopia linakabiliwa na shida za uhamiaji na usafirishaji wa binadamu na kwa kutumia njia mbadala ya kupata suluhisho inawezekana kupitia elimu ya vijana. Amethibitisha hayo, mwishoni mwa wiki iliyopita alipokutana na waziri huyo, akiwa katika ziara nchini Huko. Kardinali anasema kuwa Kanisa Katoliki Ethiopia linajitahidi kukabiliana na shida ya uhamiaji kwa kutafuta fursa mbalimbali za nafasi ya ajira kwa vijana iliwaweze kunufaika na kujenga taifa lao.
Unyanyaswaji kwa wahamiaji ni picha mbaya sana
Akiendelea kusisitiza umuhimu wa kuelimisha vijana, Kardinali Berhaneyesus amefafanua kuwa wakati vijana wanapohama wanakabiliwa na hatari ya kifo na kwa wale ambao wanajaliwa kufika mwisho wa safari wanakabiliwa na hatari ya unyanyaswaji na kwa upande huo, anamesema inasikitisha sana na siyo picha nzuri ya kutazama. Kwa hivyo amependekeza vijana kubaki katika nchi yao ili waweze kuiboresha na kwa wale ambao wangependelea kupata riziki mahali penginepo basi, waweze kutayarishwa kuhusu vikwazo na hatari wanazoweza kukabiliana nazo.
Akizungumzuia juu ya madhara wanayoyapata wahamiaji, Kardinali amethibitisha kwamba hii ni shida kubwa nyingine ambayo inawakabili wahamiaji wakati wanapofika mwisho wa safari yao na ambayo huwafanya kukata tamaa baada ya kutambua kuwa hali ya maisha ni kinyume na matarajio yao. Kutokana na hiyo, anasisitiza kuwa elimu ni kigezo muhimu cha kuweza kupata mwafaka wa vijana hao katika maisha na ili waweze kubaki mahalia, japokuwa matatizo ya uchumi na ukosefu wa ajira bado unaikumba nchi ya Ethiopia.
Elimu kwa vijana ni ufunguo dhidi ya kuhama nchi mahalia
Kadhalika Askofu Mkuu wa Ethiopia akijikita kuelezea juu ya kupata elimu kwa vijana, kutokana na kwamba, vijana waliohitimu elimu ya kutosha , ni kiegezo muhimu katika taifa na kwa manufaa yao. Hata hivyo amweze kuwapongeza kuwepo kwa vijana wengi nchini Ethiopia ambao wamepata wafadhali wa masomo kutoka nchi ya Hungaria na baada ya kufuzi masomo yao wamezea kurudi mwakwao na ili kusaidia uboreshaji wa nchi!
Kwa upande wake Waziri Azbej ya nchini ya Hungaria amesema ni furaha kubwa kwake kutambua kuwa vijana ambao wamepokea ufadhili wa masomo katika nchi ya Hungaria wamerejea katika nchi yao na wanasaidia katika kuendeleza na kuboresha nchi. Kadhalika amesema kuwa nchi yake imejitolea kuwasaidia wakristo ambao wanaoteswa duniani na kwa njia ya pekee anasifu ushirikiano baina ya Kanisa Katoliki la Ethiopia na nchi ya Hungaria katika tendo la kuwafikia watu maskini. Mwisho Waziri Azbej amemwalika Kardinali Berhaneyesus na viongozi wote wa kidini kutembelea nchi ya Hungaria!