Cerca

Vatican News
Tarehe 5 Septemba siku ya kukumbuka kifo cha Mama Taresa Calcutta mahali ambapo familia ilizunguka kaburi lake kusali Tarehe 5 Septemba siku ya kukumbuka kifo cha Mama Taresa Calcutta mahali ambapo familia ilizunguka kaburi lake kusali  (ANSA)

Familia ya Mama Teresa wa Calcuta waadhimisha sikukuu!

Tarehe 5 Septemba Askofu Mkuu Thomas D’Souza aliongoza ibada ya Misa asubuhi mapema mahalia ambapo kulikua na mapadre zaidi ya 30 wa Mwili wa Kristo ambao walishirikiana, hao am ni shirika la kiume lililoanzishwa na Mama Teresa, akiwa na watawa na waamini ambao baadaye walitoa heshima katika kaburi la mama yao mpendwa

Frt. Titus Kimario - Vatican

Katika sikukuu ya Mtakatifu Mama Teresa wa Calcuta, “familia ya Mama Teresa” ilikutana kwa ajili ya misa ya kumkumbuka Mama Teresa na sala mbele ya kaburi lake katika nyumba mama ya Wamisionari wa Upendo. Askofu Mkuu Thomas D’Souza , aliongoza ibada ya Misa kunako saa 6.00 asubuhi masaa ya mahalia  ambapo kulikua na mapadre zaidi ya 30 wa Mwili wa Kristo ambao  walishirikiana naye ambalo ni shirika la kiume lililoanzishwa na Mama Teresa.

Baada ya misa, mapadre na waumini walikusanyika kuzunguka kaburi la Mama Teresa, Mama mkuu wa masista, Sista Mary Prema alikumbushia umuhimu wa kukaa kama familia. “Masikini, wasiopendwa na wasiotakiwa hawana familia. Mungu ametuchagua sisi kuwa familia yao. Watawa wote wa Mama Teresa, mabrother, mapadre na masista tumeitwa katika familia hii moja ili kuwa familia kwa ajili ya masikini”. Aliendelea kufafanua kwamba, sisi sote tumeitwa kushirikishana upendo wa Mungu katika roho ya furaha ya Mama Teresa. Sista Prema pia aliwasha mishumaa mitano katika kaburi la Mama Teresa, kama ishara ya matawi matano ya wamisionari wa Upendo wanaofanya kazi pamoja kama familia moja ya masista, mapadre, mabruda, walei wa kujitolea na wagonjwa.

Tangu siku ya kifo chake, 5 Septemba 1997 na baada ya mazishi ya kitaifa kama heshima kwake, kaburi la Mama Teresa ni kituo cha hija ulimwenguni kwa wakristu na hata watu wa imani nyingine. Papa Fransisko alimtangaza Mama Teresa kuwa mtakatifu mwishoni mwa mwaka wa huruma ya Mungu tarehe 4 Septemba 2016. Kwa watu waliokuwa wamemfahamu wanamshuhudia Mama Teresa kwamba alikua mtakatifu katika maisha yake.

07 September 2018, 08:54