Tafuta

Rais Mattarella alietembelea shughuli za kimisionari huko Abidjan nchini Ivory Coast ikiwemo hata nyumba ya urafiki ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Rais Mattarella alietembelea shughuli za kimisionari huko Abidjan nchini Ivory Coast ikiwemo hata nyumba ya urafiki ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  (ANSA)

Ivory Coast:Rais Mattarella katika Nyumba ya Mt.Egidio huko Abidjan

“Nilianza nikisema hii ni ndoto na kiukweli ni tumaini.Na matumaini ni kipengele hicho ambacho hubadilisha ndoto kuwa ukweli halisi."Ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Iitalia Bwana Mattarella wakati alipotembelea'Nyumba ya Urafiki'ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio huko Abdjani,Ivory Cost.Hao ni watoto maskini na vijana walioondolewa mitaani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kabla ya kuondoka kutoka nchini Ivory Cost kuelekea nchini Ghana akiwa katika ziara yake, barani Afrika,  Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella  tarehe 4 Aprili 2024, alasiri alitembelea Nyumba ya Urafiki ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio katika jiji kuu Abidjan.  Kwa mujibu wa Shirika la habari za kidini la Baraza la Maaskofu Italia (SIR) linabainisha   kuwa kwa kupokelewa na wahusika wa Jumuiya hiyo, kiongozi wa Nchi ya Italia kwa kusindikizwa na mwanaye Laura, alipitia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jumuiya hiyo, iliyopo nchini humo kwa zaidi ya miaka thelathini.

Rais Mattarella mara alipowasili Ivory Coast na kulakiwa uwanja wa Ndege
Rais Mattarella mara alipowasili Ivory Coast na kulakiwa uwanja wa Ndege

Kwanza kabisa alitembelea watoto wa Shule ya Amani, wanaotoka katika vitongoji duni vya Abidjan, ambao walimwonesha Rais baadhi ya michoro na maandishi dhidi ya vita na ujumbe mwingi uliotumwa kwa wenzao wanaoteseka kutokana na migogoro inayoendelea nchini Ukraine na Mashariki mwa Congo DRC. Pamoja na Shule za Amani (zinazohudhuriwa na watoto 3,000 nchini Ivory Coast), pia ni watoto wengi ambao hawajasajiliwa wakati wa kuzaliwa na kwa hivyo hawajulikani katika ofisi ya usajili.

Rais Mattarella kukutana na kundi la watoto walitoka mitaani

Rais Mattarella baadaye alikutana na kundi la watoto wa zamani waliokuwa wanaishi mitaani na sasa waliokaribishwa katika Nyumba ya Ndoto, ambapo kuna  Vijana kwa ajili ya Amani, ambayo ni harakati ya vijana ya Jumuiya. Katika kufafanua hali ya watoto hao “Walielezea jinsi vijana mara nyingi hupoteza matumaini katika siku zijazo na kuiona tu katika uhamiaji. Miaka minne iliyopita, walibainisha kuwa Laurent, mvulana wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 14, alipatikana akiwa maiti ndani ya behewa la mizigo ya ndege iliyotua jijini Paris Ufaransa.

Mattarella alitembelea shule moja huko Vridi -Ivory Coast
Mattarella alitembelea shule moja huko Vridi -Ivory Coast

Baada ya mkasa huo, Vijana wa Amani walifanya makongamano mashuleni kuelezea hatari za safari za matumaini kuelekea Ulaya, ambapo vijana wengi wanakufa au kupotea katika jangwa na bahari ya Mediterania, na kuwaelezea juu ya uwezekano wa kujenga maisha ya baadaye katika nchi ya mtu binafasi hasa kwa kuweza kugundua tena thamani ya mshikamano.

Rais Mattarella akiwasalimia watoto
Rais Mattarella akiwasalimia watoto

Tunajivunia kuwa sehemu ya Nchi yetu na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio

Baada ya kusalimiana na baadhi ya watoto hao waliosaidiwa kujua kusoma na kuandika kutokana na kukosa shule ya karibu kwa sababu  ya umbali mrefu,   na mchango wa familia za Kiitaliano, Rais alikutana na kundi la wazee ambao wanakabiliwa na matatizo mengi barani Afrika, kutokana na kukosa pensheni hadi kutengwa na jamii kunakosababishwa pia na chuki. Kwa njia hiyo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inajenga muungano kati ya vizazi kwa kuleta suala la uzee kwa jamii ya Ivory Coast. Mwishoni salamu zilikuwa ni kutoka kwa Alphonse Krecoum, kwa niaba ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambaye alimshukuru na kusema: “Asante Mheshimiwa Rais kwa kukutana, katika ‘Nyumba hii ya Urafiki’ baadhi ya watu ambao ni sehemu ya familia yetu. Hapa vijana wengi, wakijaribiwa na tukio la uhamiaji, ambalo mara nyingi huwa mchezo wa kuigiza, hugundua tena mshikamano kama thamani ya kujenga mustakabali wa amani barani Afrika. Tunajivunia kuwa raia wa Ivory Coast na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, kwa mshikamano na wale wote wanaohitaji, tujenge mustakabali katika miji yetu ambayo kuna nafasi kwa kila mtu.”

Shughuli ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio duniani ni kukuza ndoto

Akijibu hotuba ya mhusika wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio huko Ivory Cost, Rais Mattarella alisema: “Hii na shughuli nyingi na mipango ambayo jumuiya ya Mtakatifu Egidio inatekeleza duniani kote ina kitu kimoja kwa sababu ya msingi inayowaunganisha wote na ni ndoto ya ubinadamu bora kwa mshikamano unaowahakikishia wote mustakabali wa pamoja ni wa amani na unaofaa kwa hali ya kibinadamu. Na hii ni ndoto, kiukweli ni tumaini. Na matumaini ni kipengele hicho, hali ambayo inabadilisha ndoto kuwa ukweli, ukweli halisi.”

Matarella atembelea Ivory Coast na hata vituo vya huduma kama kile cha Nyumba ya Rafiki
06 April 2024, 15:30