Tafuta

Kila tarehe 22 Machini siku ya Maji duniani:Unicef inasema kuwa 'Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwa watu wote kungesaidia kupunguza magonjwa na vifo hasa miongoni mwa watoto.' Kila tarehe 22 Machini siku ya Maji duniani:Unicef inasema kuwa 'Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwa watu wote kungesaidia kupunguza magonjwa na vifo hasa miongoni mwa watoto.' 

UNICEF,Siku ya Maji Duniani:Watoto 1000 chini ya miaka 5 wanakufa kila siku!

Kila siku zaidi ya watoto 1000 chini ya miaka 5 wanakufa kwa sababu ya magonjwa yanayohusiana na maji na huduma za usafi zisizostahili.Upatikanaji wa maji ya kunywa kwa wote ni hitaji la msingi na haki ya binadamu.Linasema UNICE katika Siku ya Maji Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 22 ya kila mwaka

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani tarehe 22 Machi 2024 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto(UNICEF) linakumbusha kwamba kila siku, zaidi ya watoto 1,000 walio chini ya umri wa miaka 5 wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusishwa na ukosefu wa maji na usafi wa mazingira, na kuua zaidi ya watu milioni 1.4 kila mwaka. Ulimwenguni, karibu watoto bilioni 1 (milioni 953) wanakabiliwa na viwango vya juu au vya juu vya mkazo wa ukosefu wa maji. Kwa mfano Nchini Italia inakadiriwa kuwa mnamo 2022 kulikuwa na takriban watoto elfu 298 walioathiriwa na viwango vya juu au vya juu sana vya mkazo wa maji. Ulimwenguni, watoto milioni 240 wanakabiliwa sana na mafuriko katika pwani na watoto milioni 330 wanakabiliwa sana na mafuriko ya mito. Mtu mmoja kati ya 4 duniani hana maji ya kunywa yaliyodhibitiwa kwa usalama. Zaidi ya hayo, watu 2 kati ya 5 bado hawana usafi wa mazingira unaosimamiwa kwa usalama (bafu) na 1 kati ya 4 hawana vifaa vya msingi vya maji (vifaa vya kunawa mikono).

Utofauti mkubwa kati ya maskini na wanoishi vijijini

Takwimu zinaonesha tofauti kubwa, huku maskini zaidi na wale wanaoishi vijijini wana uwezekano mdogo wa kutumia huduma za kimsingi. Katika nchi nyingi, mzigo wa kukusanya maji unaendelea kuwaangukia wanawake na wasichana. Ulimwenguni, katika nyumba 2 kati ya 3, wanawake ndio wanaohusika na kubeba maji. Asilimia 16% ya idadi ya watu duniani, au watu bilioni 1.8, hukusanya maji kutoka kwa vyanzo vilivyo nje ya nyumba. Kati ya hao, 63% ya wanawake wana jukumu la kusafirisha maji, ikilinganishwa na 26% ya wanaume. Ulimwenguni, wasichana wana uwezekano mkubwa wa kuchota maji kuliko wavulana katika maeneo yote isipokuwa Afrika Kaskazini na Asia Magharibi.

Asilimia 45 ya wakazi Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaochota maji ni wanawake

Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, asilimia 45 ya wakazi wanachota maji na wanawake wana uwezekano wa kusafirisha maji mara nne zaidi ya wanaume. Upatikanaji wa maji ya kunywa kwa wote ni hitaji la msingi na haki ya binadamu. Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwa watu wote kungesaidia kupunguza magonjwa na vifo hasa miongoni mwa watoto. Mkazo wa maji: uwiano kati ya mahitaji ya jumla ya maji na usambazaji unaopatikana wa maji ya uso na chini ya ardhi. Mahitaji ya maji yanajumuisha matumizi ya nyumbani, viwandani, umwagiliaji na ufugaji. Thamani za juu zinaonyesha ushindani mkubwa kati ya watumiaji. Huduma za maji ya kunywa zinazosimamiwa kwa usalama - yaani, maji ya kunywa kutoka kwenye chanzo kilichoboreshwa, yanayoweza kufikiwa kwenye tovuti, yanayopatikana inapohitajika, na yasiyo na uchafuzi wa kinyesi na kemikali za kimsingi - inawakilisha safu mpya kabambe kwenye ngazi inayotumika kufuatilia maendeleo ya maji ya kunywa.

Chama cha Legambiente (Italia)na mchango wa UNHCR

Katika Siku ya Maji Duniani 2024, Legambiente pamoja na mchango wa UNHCR wanawasilisha lengomtazamo halisi wa “Maji, migogoro na uhamaji wa kulazimishwa: usimamizi sahihi wa rasilimali za maji kama chombo cha utulivu na amani.” Kati ya mwaka 2000 na 2023, kulikuwa na migogoro 1,385 ambayo iliona rasilimali za maji kama kichocheo au kama silaha dhidi ya idadi ya watu. Wahamiaji wa kulazimishwa wanaongezeka, huku Pembe ya Afrika na Somalia hasa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi: mnamo mwaka 2023, kulingana na Shirika la Umoja wa mataifa la Wahamiaji (UNHCR,) walikuwa ni  karibu watu milioni 3 wahamiaji wa kulazimishwa ndani ya nchi kutokana na mchanganyiko wa ukame na mafuriko na hali ya migogoro na ukosefu wa usalama. Zaidi ya hayo ni ugumu katika maeneo ambayo wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao wanakaribishwa kutoa huduma za maji na usafi wa mazingira. Mazoea mazuri ya Shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji ( UNHCR) wanabainisha kuwa  kutoka upanuzi wa mfereji wa maji huko Agadez nchini (Niger) hadi uwekaji Solar juu ya  visima 295 mnamo mwaka 2023. Ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji ni wa dharura. Nchini Italia kwa mfano wanabainisha kuwa lazima pia ifanye sehemu yake, Serikali lazima iharakishe utekelezaji wa PNACC na juu ya rasilimali zinazohusiana za kiuchumi zinazohitajika kuanzia hatua tatu muhimu.”

Maji ni kama daraja la amani badala ya migogoro

Maji ni kama daraja la amani badala ya kuwa chanzo cha migogoro. Hili ndilo ombi lililozinduliwa na Chama kimojawapo cha Kitaifa kiitwacho Legambiente(Kinachohus Mazingira) naShirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa(UNHCR) likilenga “Maji, migogoro na uhamaji wa kulazimishwa: usimamizi sahihi wa rasilimali za maji kama chombo cha utulivu na amani” iliyochukuliwa kutoka katika ripoti yenye Kauli mbiu: “ Ubinadamu katika mwendo:madhara ya mzozo wa hali tabianchi kwa uhamaji wa kulazimishwa iliyotolewa katika fursa ya maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani  kwa mwaka 2024, ambayo  kwa usahihi katika mada ya rasilimali za maji kama chombo cha amani. Mgogoro wa maji duniani, tokeo la moja kwa moja la msukosuko wa hali ya tabianchi unaojidhihirisha kwa kukithiri kwa matukio ya hali ya Tabianchi, kama vile ukame, mafuriko na dhoruba na usimamizi usio endelevu wa rasilimali za maji, ni tishio kwa sayari lakini pia kwa amani.

Ifikapo 2050 watu milioni 216 watalazimika kuhama

Kwa hakika, usimamizi na udhibiti wa rasilimali za maji unazidi kusababisha kuzorota kwa mivutano na migogoro katika maeneo hatarishi zaidi ya dunia yenye athari kali kwa mustakabali wa idadi ya watu, kulazimika kukimbia, wakati mwingine kuelekea makazi au kambi zilizoathiriwa na hali mbaya ya hewa na. ambapo inazidi kuwa vigumu kutoa huduma za maji na usafi wa mazingira. Kulingana na ripoti ya pili ya Benki ya Dunia ya Groundswell, inatabiriwa kuwa ifikapo mwaka 2050, karibu watu milioni 216 wanaweza kulazimika kuhama kutokana na athari za hali ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na shinikizo la maji. Miongoni mwa maeneo ya dunia yaliyoathirika zaidi ni Pembe ya Afrika: nchini Somalia pekee mwaka 2023, kulingana na makadirio ya UNHCR, ukame mkubwa zaidi katika miaka 40 iliyopita na mafuriko, pamoja na hali ya migogoro na ukosefu wa usalama, imesababisha karibu mamilioni 3 ya watu wahamiaji wapya wa kulazimishwa ndani ya nchi.

Kati ya 2000 na 2023 kulikuwa na migogoro 1,385 inayohusishwa na usimamizi wa rasilimali maji

Kwa kurejea kwenye migogoro, kati ya 2000 na 2023 kulikuwa na migogoro 1,385 iliyohusishwa na usimamizi wa rasilimali za maji (chanzo ni Taasisi ya Pacific). Kati ya hizi, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Siria ambavyo viliibuka sio tu kutokana na mivutano ya kidini, kijamii na kisiasa, lakini pia na ukosefu wa upatikanaji wa maji uliochochewa na kipindi kirefu cha kiangazi (tangu 2007 hadi 2010) na migogoro katika eneo la Sahel barani Afrika kati ya wakulima na wafugaji kuhusu masuala ya matumizi ya ardhi na upatikanaji wa rasilimali za maji, ikichochewa na vipindi virefu vya ukame, mvua kubwa na mafuriko. Kwa kuzingatia hilo, ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji unahitajika haraka. Kwa hakika, kulingana na Umoja wa Mataifa, ingawa watu bilioni 3 duniani wanategemea maji ambayo yanavuka mipaka ya kitaifa, ni nchi 24 tu kati ya 153 zinazotangaza kuwa na makubaliano ya ushirikiano wa maji ya pamoja.

Siku ya Maji duniani (UNICEF)
22 March 2024, 10:44