Tafuta

Mfalme wa Norway ampokea Rais wa Tanzania huko Oslo tarehe 13 Februari 2024. Mfalme wa Norway ampokea Rais wa Tanzania huko Oslo tarehe 13 Februari 2024.  (ANSA)

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Tanzania nchini Norway

Jumanne tarehe 13 Februari 2024,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Maflme wa Norway akiwa katika ziaya ya kiserikali katika nchi ya Kakazini mwa Ulaya baada ya Vatican.Na vile vile amekutana na Spika wa Bunge la Ufalme wa Norway huko Oslo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ziara ya Mama Samia Suluhu Hassani haiishii Vatican tu imeendelea katika Nchi ya Kaskazini mwa Ulaya penye baridi kali sana na theruji. Mama Samia kupitia ukurasa wa Ufalme ameonekana akipokelewa na wanajeshi nawa eneo na pia Mfalme wa Norway pamoja na familia yake ya kifalme.

Rais wa Tanzania akiwa na Mfalme wakati wa afla ya mapokezi nchini Norway
Rais wa Tanzania akiwa na Mfalme wakati wa afla ya mapokezi nchini Norway

Hata hivyo mapema Jumanne tarehe 13 Februari 2024, Balozi wa Norway nchini Tanzania,  Bwana Tone Tinnes, aliandika katika chapisho lake kwenye akaunti ya X, ambayo pia taarifa iliwekwa tena na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwamba: “Maandalizi makubwa katika Ikulu ya Kifalme leo (Jumanne 13,Februari), tayari kumkaribisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenda Norway.”

Mama Samia akiwa na Mfalme wa Norway
Mama Samia akiwa na Mfalme wa Norway

Kwa mujibu wa tovuti ya Ubalozi wa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za washirika wa Norway kwa maendeleo ya muda mrefu na inaunga mkono azma ya Tanzania ya kuwa nchi ya kipato cha kati isiyotegemea misaada.

Mama Samia akiwa na Spika wa Bunge  la Norway Svein Harberg
Mama Samia akiwa na Spika wa Bunge la Norway Svein Harberg

Mkuu wa Nchi ya Tanzania  kwa njia hiyo anatembelea nchi ya Norway kwa  mara baada ya kuhitimisha ziara yake mjini Vatican siku ya Jumatatu tarehe 12 Februari 2024, iliyoanza tarehe 10 Februari na ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Baba Mtakatifu Francisko, kwa kujikita na mtazamo wa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Vatican, na vile vile baada ya Mkutano huo na Papa Francisko, Rais alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.

Mama Samia akiwa anatembea na mwenyeji wake Mfalme wa Norway Haakon katika Nyumba ya kifalme ya Oslo
Mama Samia akiwa anatembea na mwenyeji wake Mfalme wa Norway Haakon katika Nyumba ya kifalme ya Oslo
13 February 2024, 17:55