Tafuta

 Kuzuia saratani ya shingo la uzazi inawezekana.Hawa ni kikundi cha wanawake wa Cabo Verde wakiwa sehemu ya tukio la mazoezi  ya kupambana na saratani. Kuzuia saratani ya shingo la uzazi inawezekana.Hawa ni kikundi cha wanawake wa Cabo Verde wakiwa sehemu ya tukio la mazoezi ya kupambana na saratani.  (Cecilie_Arcurs)

UN,WHO:Inawezekana kuzuia saratani ya shingo ya kizazi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limetangaza kuwa mwezi wa Januari ni mwezi wa kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya shingo ya kizazi.Makala hii inaakisi kuhusu ugonjwa huo unasababishwa na nini,tiba yake pamoja na jinsi ya kujikinga.Kwa hiyo inawezekana kuzuia au kupona iwapo inagunduliwa mapema.

Habari kutoka Umoja wa Mataifa

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) limebainisha kuwa katika ulimwenguni kote, saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa wanawake, ambao walikuwa ni wagonjwa wapya 604,000 mnamo 2020. Takriban asilimia 90 ya vifo 342,000 vilivyosababishwa na saratani ya shingo ya kizazi vilitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Viwango vya juu zaidi vya saratani hiyo na vifo ni kutoka bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika ya Kati na Kusini-Mashariki mwa Asia. Wanawake wanaoishi na Virusi vya UKIMWI - VVU wana uwezekano mara 6 zaidi wa kupata saratani ya shingo ya kizazi ikilinganishwa na idadi ya watu kwa ujumla, na inakadiriwa asilimia 5 ya visa vyote vya saratani ya mlango wa kizazi huchangiwa na VVU.  Na mchango wa VVU katika saratani ya shingo ya kizazi huathiri vibaya wanawake wenye umri mdogo, na matokeo yake, asilimia 20 ya watoto wanaopoteza mama zao kutokana na saratani ya shingo ya kizazi. Katika Ukurasa wa Shirika la Umoja wa Mataifa (WHO) la Afya ulimwenguni limetangaza kuwa mwezi wa Januari ni mwezi wa kuhamasisha jamii kuhusu gonjwa la saratani ya shingo ya kizazi. Na katika ukurasa wa Umoja wa Mataifa, umeakisi kuhusu ugonjwa huo, unasababishwa na nini, tiba yake pamoja na jinsi ya kujikinga.

Gonjwa hili baya linasababishwa na nini?

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kwa njia hiyo limetangaza kuwa mwezi wa Januari  2024 ni mwezi wa kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya shingo ya kizazi. Kwa hiyo Virusi vya aina ya Human Papiloma (HPV) ni maambukizi ya kawaida ya zinaa ambayo yanaweza kuathiri ngozi, sehemu za siri na koo. Takriban watu wote wanaofanya ngono wataambukizwa wakati fulani wa maisha yao, kwa kawaida bila dalili. Mara nyingi mfumo wa kinga huondoa (HPV) kutoka katika mwili. Maambukizi ya mara kwa mara ya HPV yanaweza kusababisha seli zisizo za kawaida kukua, ambazo huendelea na kuwa saratani. Maambukizi ya mara kwa mara ya HPV kwenye shingo ya kizazi ikiwa haitatibiwa, husababisha asilimia 95 ya saratani ya mlango wa kizazi. Kwa kawaida, inachukua miaka 15-20 kwa seli zisizo za kawaida kuwa saratani, lakini kwa wanawake walio na kinga dhaifu, kama vile wenye VVU isiyotibiwa, mchakato huu unaweza kukuwa haraka na kuchukua miaka 5-10.  Sababu za hatari zinazoweza kusababisha saratani ni pamoja na kiwango cha aina ya HPV iitwayo oncogenicity, hali ya kinga mwilini, uwepo wa magonjwa mengine ya zinaa, idadi ya kuzaa watoto, ujauzito wa kwanza katika umri mdogo, matumizi ya uzazi wa mpango wakutumia homoni, na kuvuta sigara.

Ufahamu wa habari na huduma ya kuzuia

Kukuza ufahamu wa umma, utowaji wa habari na huduma ni muhimu katika kuzuia na kudhibiti katika kipindi cha maisha yote. Kupata chanjo katika umri wa miaka 9-14 ni njia nzuri sana ya kuzuia maambukizi ya HPV, saratani ya mlango wa kizazi na saratani zingine zinazohusiana na HPV. Uchunguzi kuanzia umri wa miaka 30 (miaka 25 kwa wanawake wanaoishi na VVU) unaweza kugundua ugonjwa wa kizazi, ambao unapotibiwa, pia huzuia saratani ya shingo ya kizazi. Katika umri wowote wenye dalili au mashaka, kugunduliwa mapema na kufuatiwa na matibabu ya haraka kunaweza kutibu saratani ya shingo ya kizazi.

Kuhusu chanjo ya Virusi vya aina ya Human Papiloma (HPV)

Hadi kufikia mwaka 2023, kuna chanjo 6 za HPV zinazopatikana ulimwenguni. Chanjo zote hizo zinalenga kulinda dhidi ya aina hatarishi za HPV 16 na 18, ambazo husababisha saratani nyingi za mlango wa kizazi na zimeoneshwa kuwa salama na zenye ufanisi katika kuzuia maambukizi ya HPV na saratani ya shingo ya kizazi. Kama kipaumbele, chanjo za HPV zinapaswa kutolewa kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 9-14, wa kubalehe na kabla ya kuanza kujamiiana.  Chanjo zinaweza kutolewa kama dozi 1 au 2. Watu walio na kinga iliyopunguzwa wanapaswa kupokea dozi 2 au 3.  Baadhi ya nchi pia zimechagua kuwachanja wavulana ili kupunguza zaidi maambukizi ya HPV katika jamii na kuzuia saratani kwa wanaume zinazosababishwa na HPV.  Kuna njia nyingine ya kuzuia maambukizi ya HPV ambayo na: Kutovuta sigara au kuacha kuvuta sigara, kutumia kondomu, kutahiriwa kwa wanaume kwa hiari.

Wanawake lazima wachunguzwe kizazi kila baada ya miaka 5-10

Wanawake wanapaswa kuchunguzwa saratani ya shingo ya kizazi kila baada ya miaka 5-10 kuanzia umri wa miaka 30. Wanawake wanaoishi na VVU wanapaswa kuchunguzwa kila baada ya miaka 3 kuanzia umri wa miaka 25. Mkakati wa kimataifa unahimiza angalau kufanya uchunguzi mara mbili kipimo cha juu cha HPV katika umri wa miaka 35 na tena katika miaka 45. Ugonjwa wa saratani mara chache hutoa dalili, ndiyo maana uchunguzi wa mara kwa mara wa saratani ya shingo ya kizazi ni muhimu, hata kama umepata chanjo ya dhidi ya HPV. Ukusanyaji binafsi wa sampuli kwa ajili ya kupima HPV, ambayo inaweza kuwa chaguo linalopendelewa na wanawake, imeonesha kuwa wa kuaminika ilkilinganishwa na sampuli zilizokusanywa na watoa huduma za afya. Baada ya kipimo cha HPV chanya (au njia nyingine ya uchunguzi) mtoa huduma ya afya anaweza kutafuta mabadiliko kwenye seviksi (kama vile saratani) ambayo yanaweza kuibuka na kuwa saratani ya shingo ya kizazi ikiwa haitatibiwa.  Matibabu ya awali ya hali ambazo zinaweza kuwa saratani ni utaratibu rahisi na kuzuia saratani ya kizazi. Matibabu yanaweza kutolewa wakati huo huo ulipotembelea hospital kwa uchunguzi au baada ya kipimo cha pili (njia ya kuona, kupima na kutibu), ambayo inapendekezwa haswa kwa wanawake wanaoishi na VVU. Matibabu ya kabla ya kuwa na saratani ni ya haraka na kwa ujumla hayana maumivu na ni nadra kusababisha matatizo.

Saratani ya shingo inaweza kupona kwa utambuzi na matibabu

Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuponywa iwapo itagunduliwa na kutibiwa katika hatua ya awali ya ugonjwa. Kutambua dalili na kutafuta ushauri wa matibabu ili kushughulikia wasiwasi wowote ni hatua muhimu. Wanawake wanapaswa kuonana na mtaalamu wa afya ikiwa watagundua:Kutokwa na damu isiyo ya kawaida kati ya siku za hedhi, baada ya kukoma hedhi, au baada ya kujamiiana, Utokaji mwingi au harufu mbaya kwenye sehemu za siri. Dalili kama vile maumivu ya mara kwa mara ya mgongo, miguu au nyonga. Kupoteza uzito, uchovu na kupoteza hamu ya kula. Usumbufu au kutojihusi uko sawa sehemu za siri. Uvimbe kwenye miguu. Tathmini za kimatibabu na vipimo vya kuthibitisha utambuzi ni muhimu na kwa ujumla zitafuatwa na rufaa kwa huduma za matibabu zaidi, ambazo zinaweza kujumuisha upasuaji, tiba ya mionzi na tibakemikali ili kutoa huduma tegemezi na udhibiti wa maumivu. Wakati nchi za kipato cha chini na cha kati zikiongeza uchunguzi wa shingo ya kizazi, wagonjwa wengi wa saratani ya shingo ya kizazi watagunduliwa, hasa katika idadi ya watu ambao hawakuchunguzwa hapo awali. Kwa hivyo, mikakati ya rufaa na udhibiti wa saratani inahitaji kutekelezwa na kupanuliwa pamoja na huduma za kuzuia.

Jitihada za Nchi karibu zote katika kukomesha saratani ya shingo  ya kizazi

Kwa mujibu wa Shirila la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) nchi zote zimejitolea kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kama tatizo la afya ya umma. Mkakati wa Kimataifa wa WHO unafafanua uondoaji kama kupunguza idadi ya wagonjwa wapya kila mwaka hadi 4 au pungufu zaidi kwa kila wanawake 100,000 na kuweka malengo matatu yatakayofikiwa ifikapo mwaka mwaka 2030 kuweka nchi zote kwenye njia ya kutokomezwa katika miongo ijayo: Asilimia 90 ya wasichana kupatiwa chanjo ya HPV wakifikia umri wa miaka 15, Asilimia 70 ya wanawake wachungyzwa kwa kipimo cha ubora wa juu wakiwa na umri wa miaka 35 na 45, Asilimia 90 ya wanawake wenye ugonjwa wa mlango wa kizazi wapate matibabu. Inakadiria kuwa wagonjwa wapya milioni 74 wa saratani ya mlango wa kizazi wanaweza kuepuka, na vifo milioni 62 vinaweza kuepukwa kwa kufikia lengo hili la kutokomeza.

Saratani ya Shingo ya Uzazi inatibitika ikiwa itagunduliwa mapema
08 January 2024, 15:27