Tafuta

Mwanzoni mwa mkutano wa Italia na Afrika, Waziri Mkuu Meloni alipokea viongozi katika Seneti. Mwanzoni mwa mkutano wa Italia na Afrika, Waziri Mkuu Meloni alipokea viongozi katika Seneti.  (ANSA)

Mkutano wa Italia na Afrika mjini Roma:makumi ya viongozi wa kisiasa wanahudhuria

Mamlaka za juu zaidi za Ulaya pia zinashiriki katika tukio la "Italia-Afrika,daraja la ukuaji wa pamoja” ambalo lilianza jioni tarehe 28 Januari 2024 na Italia ni mwenyekiti wa G7 katika nusu ya kwanza ya mwaka ambayo imejitolea kufanya maendeleo ya Afrika kuwa mada kuu katika mamlaka yake.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Kuna takriban nchi arobaini za Kiafrika zilizopo mjini Roma, Italia kwa ajili ya Mkutano wa Italia na Afrika, uliofunguliwa Dominika jioni, tarehe 28 Januari 2024, katika ukumbi wa Taifa na unaendelea katika Seneti na majopo mbalimbali. Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, pia aliwasili katika Ikulu ya Italia kwa ajili ya mkutano huo.

Waziri Mkuu wa Italia akihutubia
Waziri Mkuu wa Italia akihutubia

Kabla yake, rais wa Bunge la  Umoja wa Ulaya EU, Bi Roberta Metsola, na rais wa Baraza la Ulaya, Bwana Charles Michel, walikuwa tayari wameingia. Lengo lao ni kutoa fedha kwa nchi za Afrika ili kukuza maendeleo ya kiuchumi. Nchi nyingi zinawakilishwa katika ngazi ya wakuu wa nchi na serikali, na wengine na wakuu wa diplomasia au mawaziri wa ngazi ya juu, walioitwa jijini Roma kwa Mkutano huu ambao tayari ni mpango unaobeba kauli mbiu: "Italia-Afrika, daraja la ukuaji wa pamoja." Wazo ni kuwasilisha Italia kama daraja kati ya Ulaya na Afrika, ili kuipatia bara la  zamani mabonde mapya ya usambazaji wa nishati na uwekezaji mkubwa kwa Afrika.

Wakuu wa Nchi na Seerikali kutoka Afrika sehemu kubwa na Ulaya pia
Wakuu wa Nchi na Seerikali kutoka Afrika sehemu kubwa na Ulaya pia

Serikali ya Italia inakusudia kuwasilisha Mpango wa Mattei kwa kila mtu kwa undani, mpango ulioongozwa na Enrico Mattei, mwanzilishi wa Eni,(shirika la mafuta)ambaye, tayari katika miaka ya 1950, alifanya kazi katika uhusiano wa ushirikiano na nchi za Afrika, akiwasaidia kuendeleza rasilimali zao za asili. Kwa Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni, Mpango wa Mattei  anabainisha kuwa: "unaweza kutegemea euro bilioni 5.5 kati ya mikopo, shughuli za zawadi na dhamana: takriban bilioni 3 kutoka katika mfuko wa tabianchi ya Italia na bilioni 2.5 na nusu kutoka mfuko wa ushirikiano wa maendeleo." Waziri Mkuu Meloni aliongeza kuwa Italia inafanya "chaguo sahihi la sera ya kigeni, ambayo italeta kuhifadhi nafasi  ya heshima kwa Afrika katika ajenda ya yetu ya Urais wa G7."

Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Afrika wakikutana mjini Roma
Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Afrika wakikutana mjini Roma

Italia, ambayo inaongoza G7 katika nusu ya kwanza ya mwaka, kwa hakika imejitolea kufanya maendeleo ya Afrika kuwa mada kuu ya mamlaka yake. Ni mara ya kwanza katika Mkutano wa Italia na Afrika, ambao hadi sasa umekuwa ukifanyika mara kwa mara katika ngazi ya mawaziri, umepandishwa hadhi ya kuwa kilele cha Wakuu wa Nchi na Serikali; na ni tukio la kwanza la kimataifa kufanyika nchini Italia tangu kuanza kwa Urais wa G7, ambapo ni muhimu na kusisitiza umuhimu ambao Italia inatoa kwa ajili ya  ushirikiano na mataifa ya bara la Afrika.

29 January 2024, 17:52