Tafuta

Israel imeshambulia Khan Younis Kusini mwa ukanda wa Gaza. Israel imeshambulia Khan Younis Kusini mwa ukanda wa Gaza.  (ANSA)

Mashariki ya Kati,uvamizi mkubwa wa Israel huko Khan Younis

Mashambulizi yanaendelea kusini mwa Ukanda wa Gaza,licha ya kuanza kwa awamu mpya,isiyo na makali ya vita ambayo imetangazwa katika siku za hivi karibuni.Kesi dhidi ya Israel imeanza Januari11,2024,mjini Hague kufuatia shutuma zilizotolewa na Afrika Kusini.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hamas yanaendelea kulenga Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza ambapo handaki la chini ya ardhi linalotumiwa na Harakati ya msimamo mkali kuwashikilia mateka pia liliripotiwa kupatikana hapo. Kaskazini, hata hivyo, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinasema kuwa wameshambulia kituo cha amri cha Hezbollah na eneo la kurusha roketi kusini mwa Lebanon.

Mkutano kati ya Blinken na Abu Mazen

Kwa upande wa kidiplomasia, Waziri wa Mambo ya Nchi za  Nje wa Marekani  Bwana Antony Blinken alikutana na Rais Abu Mazen wa Palestina tarehe 10 Januari 2023 huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katika kituo cha vyombo vya habari kutoka Bahrain, na kituo kingine katika ziara yake ya Mashariki ya Kati, Blinken alitangaza kwamba kiongozi huyo atajitolea kufanya mageuzi katika Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina( PNA), lakini akibainisha kuwa Gaza haiwezi kutenganishwa na taifa la Palestina. Abu Mazen pia alishiriki katika mkutano huko Aqaba, kwenye Bahari Nyekundu, na Mfalme Abdullah II wa Yordan na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri. Wote wawili hao katika taarifa ya pamoja, walitarajia hatua madhubuti ya jumuiya ya kimataifa kufikia usitishaji madhubuti wa vita kati ya Israel na Hamas.

Netanyahu: ‘Hatutaikalia Gaza’

Kuhusu hatma ya Gaza, taarifa pia ilitoka kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliyekabidhi video iliyotolewa tarehe 10 Januari  jioni kuwa: “Israel haina nia ya kuikalia kwa kudumu Gaza au kuwaondoa raia wake. Israel inapigana na magaidi wa Hamas,  na sio idadi ya Wapalestina.” Kwa upande wake, Hamas kwa mara nyingine tena walisisitiza misimamo yake, huku wakitoa wito wa kusitishwa kikamilifu uhasama huko Gaza kwamba: “Ikiwa Israel haitakubali masharti haya, mateka hawatarejea nyumbani wakiwa hai”,walisema kupitia msemaji wao.

Kesi ya Hague dhidi ya Israel

Kesi dhidi ya Israel inayotuhumiwa kwa mauaji ya halaiki katika ombi lililotolewa na Afrika Kusini tarehe 29 Disemba 2023 imetarajia kuanza tarehe 11 Januari 2024 mjini Hague, katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Hasa, huko Afrika Kusini “iliomba Mahakama ioneshe hatua za muda za kulinda dhidi ya madhara zaidi, makubwa na yasiyoweza kurekebishwa kwa haki za watu wa Palestina chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari.” Israel na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wanakanusha vikali madai hayo kuwa ya uongo; nchi hiyo, kama ilivyotangazwa katika siku za hivi karibuni na Rais wa Israel Isaac Herzog, itawasilisha kesi ya kujilinda kuonesha kwamba inafanya iwezavyo katika hali ngumu sana  ili kuepusha majeruhi ya raia huko Gaza.

MSF: maelfu watoroka kusini mwa Lebanon

Wakati huo huo, mvutano na Hezbollah ya Lebanon unaendelea kupamba moto. Taarifa zainabaiisha kuwa tarehe 9 Israel iliwaua wanamgambo wanne wa Lebanon kwa shambulio la anga kusini mwa Lebanon wakati huo huo Hezbollah iliposhambulia kamandi ya jeshi la Israel kaskazini mwa jimbo la Kiyahudi. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka(MSF) liliripoti kuwa maelfu ya raia wanakimbia kutoka kusini mwa Lebanon kutafuta hifadhi zaidi kaskazini au katika miji mikubwa ya Ardhi ya Mierezi, yaani Lebanon.

11 January 2024, 15:36