Tafuta

Moshi ukipaa baada ya mabomu ya wanajeshi wa Israel kuanguka kati ya mpaka wa Lebanon na Israel. Moshi ukipaa baada ya mabomu ya wanajeshi wa Israel kuanguka kati ya mpaka wa Lebanon na Israel. 

Mashariki ya Kati,kamanda wa Hezbollah auawa Lebanon

Juma moja baada ya kuuawa kwa kundi la Hamas namba mbili,Saleh Arouri huko Beirut,Wissam Hassan Tawil,mkuu wa vikosi vya wasomi wa Hezbollah,aliuawa katika kijiji kilicho kilomita 6 kutoka mpaka kati ya Israel na Lebanon.Huko Gaza,wakati huo huo,vita vinaingia katika awamu mpya.Waziri wa Marekani Blinken alitua tarehe 7 usiku mjini Tel Aviv kwa ajili ya ujumbe wake dhidi ya kuongezeka kwa mzozo katika eneo hilo.

Vatican News

Lengo jipya lililofikiwa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas na washirika wake wa Kishia,tarehe 7 Januari 2024, kamanda wa Hezbollah Wissam Hassan Tawil aliuawa akiwa ndani ya gari katika kijiji cha Majdal Selm, karibu kilomita 6 kutoka mpaka na Israel. Uvamizi huo ulianza baada ya shambulio la Hezbollah dhidi ya kituo cha ulinzi wa anga cha Israel kwenye Mlima Meron.

Lebanon yasema ndiyo katika azimio la UN

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib alitangaza kuwa nchi hiyo iko tayari kutekeleza azimio namba 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linatoa udhibiti kamili wa jeshi hadi mpakani na kupokonywa silaha kwa Hezbollah ambayo haitaweza kupelekwa kusini mwa nchi hiyo kwenye  Mto Litani. Kwa upande wake, Tel Aviv ni thabiti katika lengo la kurudisha angalau watu elfu 80 nyumbani kwa usalama huko  Galilaya".

Blinken aliwasili Israel

Hatari ya kuongezeka kwa mzozo katika eneo hilo ndio msingi wa safari mpya ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken  ambayo ni ya nne tangu kuanza kwa mapigano  hayo tarehe 7 Oktoba 2023  na ambaye baada ya Saudi Arabia alitua  Israel  usiku wa tarehe 7 Januari 2024. Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema: “ Vita havina maslahi ya mtu yeyote,” huku akisisitiza haja ya kujenga mustakabali salama pia kupitia kuundwa kwa taifa la Palestina huko Gaza. Blinken pia kuna lile la kupunguza kasi ya mapigano huko Gaza, ili kuruhusu Wapalestina kurudi polepole kaskazini mwa Ukanda huo, dhana kwamba Israel ingeruhusu tu kwa kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka zaidi kutoka sehemu ya Hamas.

Hali katika Ukanda wa Gaza

Wakati huo huo, vita vya upande wa kusini vimeingia katika awamu mpya yenye sifa ya operesheni maalum na mashambulizi machache, ya angani na ya ardhini, kwa ajili ya ulinzi zaidi wa raia. Wakati huo huo, malori 202 ya misaada ya kibinadamu yamewasili katika Ukanda huo, hasa yakisafirisha chakula, maji safi na dawa. Hali, hata hivyo, bado ni ngumu sana  kwani kulingana na makadirio, idadi ya vifo imefikia  watu 23,0000.

08 January 2024, 16:37