Tafuta

Hakimu wa ICJ asikiliza maombi ya dharura la hatua za dharura za Afrika Kusini,kwamba mahakama iamuru Israel isitishe harakati zake za kijeshi huko Gaza. Hakimu wa ICJ asikiliza maombi ya dharura la hatua za dharura za Afrika Kusini,kwamba mahakama iamuru Israel isitishe harakati zake za kijeshi huko Gaza. 

Afrika Kusini yafikisha madai kwa ICJ dhidi ya Israel kuhusu vitendo vya mauaji ya kimbari

Kesi ya kwanza ya kusikilizwa dhidi ya Israel inayoshutumiwa na Afrika Kusini kwa mauaji ya kimbari,ilifunguliwa Alhamisi 11 Januari 2024,katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini Hague.Wakati huo huo,mapigano yanaendelea katika Ukanda wa Gaza na kusabisha wahanga wengi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 11 Januari 2024 Afrika Kusini imezungumza mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya haki (ICJ,)baada ya kuwasilisha kesi katika jitihada za kukomesha mauaji ya raia huko Gaza,i huku kiishutumu Israel kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina madai ambayo Israel imekanusha vikali ikisema kuwa hayana msingi wowote. Hatua hii inafanyika wakati Gaza mashambulizi huko makubwa ya Israel, yanaendelea kwa njia ya anga, ardhini na baharini kutwa  na kucha yakiwaathiri watu milioni 2.3, zaidi ya 23,000 kupoteza Maisha, maelfu kujeruhiwa na zaidi ya milioni kutawanywa, wakati  Israel ikilipiza kisasi cha mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba 2023  ambayo yalisababisha vifo vya takriban raia 1,200 wa Israel na wa kigeni kusini mwa Israel na wengine 250 kuchukuliwa mateka. Wakiwasilisha kesi yao, timu ya wanasheria wa Afrika Kusini wameiiambia ICJ mjini Hague kwamba Israel imeonesha “mfano wa mwenendo wa mauaji ya kimbari tangu ilipoanzisha vita kamili Gaza, eneo la kilomita za mraba 365 ambalo imekuwa ikilikalia kimabavu tangu 1967. Mahakama imeelezwa kuwa “Mauaji haya si kingine ila ni uharibifu wa maisha ya Wapalestina. Yanafanywa kwa makusudi, hakuna anayeachwa, hata watoto wachanga waliozaliwa”.

Machafuko yasiyo na mfano

Hatua za Israel zimewafanya watu milioni 2.3 wa Gaza kukabiliwa na mashambulizi ya anga, nchi kavu na baharini ambayo hayajawahi kushuhudiwa, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia na uharibifu wa makazi na miundombinu muhimu ya umma, alisisitiza Adila Hassim. Israel pia ilikuwa imezuia msaada wa kutosha wa kibinadamu kuwafikia wale wanaohitaji na kusababisha hatari ya kifo kwa njaa na magonjwa kwa sababu ya kutowezekana kutoa msaada wakati mabomu yanaanguka, mwanasheria wa Afrika Kusini amedai. “Wapalestina huko Gaza wanakabiliwa na mashambulizi ya mabomu popote wanapokwenda,” Bi. Hassim ameliambia mahakama, akiongeza kuwa watu wengi wameuawa kiasi kwamba mara nyingi walizikwa bila kutambuliwa katika makaburi ya pamoja. Na wakati Wapalestina wengine 60,000 wamejeruhiwa na kulemazwa, alibainisha.

Hakuna palipo salama kwa Wapalestina

Aliendelea kusema kwamba Wapalestina wanauawa wakiwa majumbani mwao, katika maeneo wanayotafuta makazi, hospitalini, shuleni, misikitini makanisani na walipojaribu kutafuta chakula na maji kwa ajili ya familia zao. Pia wanauawa ikiwa wameshindwa kuhama katika maeneo ambayo wamekimbilia na hata kama walijaribu kukimbilia kwenye njia salama zilizotangazwa na Israel.” Kama sehemu ya madai yake dhidi ya Israel, Afrika Kusini ilidai kwamba mabomu 6,000 yalipiga Gaza katika wiki ya kwanza ya Israel kujibu mashambulizi ya Hamas. Hii ni pamoja na matumizi ya mabomu ya pauni 2,000 angalau mara 200 “katika maeneo ya kusini ya Ukanda huo ambayo yaliteuliwa kuwa salama, na kaskazini, ambapo kambi za wakimbizi zinapatikana” amesema Bi Hassim. Silaha hizi zilikuwa “baadhi ya mabomu makubwa na ya uharibifu zaidi yanayopatikana,” alisisitiza, akiongeza kwamba mauaji yakimbari hayatangazwi mapema, lakini mahakama hii ina faida ya wiki 13 zilizopita za ushahidi ambao unaonyesha bila shaka muundo wa tabia na uhusiano wa nia inayohalalisha madai yanayokubalika ya vitendo vya mauaji ya kimbari.”

Wajibu wa Mkataba

Ni kwa sababu ya hatua hizi ambapo Israel ilikiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, majaji wa (ICJ) baadaye walisikia, wakirejea mkataba wa kimataifa uliotiwa wino na wanachama wa Umoja wa Mataifa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuzuia uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mkataba huo “ulijitolea kuokoa ubinadamu”, alisisitiza John Dugard, ambaye pia anawakilisha Afrika Kusini, na nchi zote ambazo zimetia saini Mkataba huo amesema “zina wajibu sio tu kuachana na vitendo vya mauaji ya kimbari bali pia kuyazuia.” Kesi hiyo itakiwa kuendelea siku ya tarehe 12 Januari 2024 kwa maelezo ya upande wa Israel.

12 January 2024, 13:52