Tafuta

Wanaharakati wa tabiachi wameandamana dhidi ya mafuta katika Jiji la Maonesho wakati wa  COP28,Dubai Wanaharakati wa tabiachi wameandamana dhidi ya mafuta katika Jiji la Maonesho wakati wa COP28,Dubai 

UNICEF-COP28:zaidi ya vijana 770elfu wameshiriki katika mashauriano

Ni zaidi vijana 770,000 770 ambapo ni zaidi ya 80% walishiriki katika mashauriano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kwa kipindi kati ya Julai hadi Septemba 2023 katika muktadha wa kilele cha Mkutano wa COP28 huko Dubai.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kati ya Julai na Septemba 2023, washiriki 771,046 walifikiwa na jukwaa la kimataifa la Repoti ya U na majukwaa 57 ya kikanda na kitaifa katika mashauriano ya kimataifa kuhusu maoni ya vijana wakati wa  kujiandaa na Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi, kwa kushirikiana na YOUNGO, kikundi rasmi cha vijana cha Umoja wa Mataifa, Mkataba wa Mfumo wa Mabadiliko ya Tabianchi, na Vijana Mabingwa wa Hali ya Hewa (YCC) wa COP28.

Vijana wamekuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya mafuta
Vijana wamekuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya mafuta

Miongoni mwa washiriki waliofichua jinsia zao, takriban 64% walitambuliwa kama wanaume na 35% kama wanawake. Asilimia 80% ni chini ya miaka 30. 34% ya waliohojiwa wakijitangaza kuwa wanatoka katika jamii za mashambani na takriban 27% kutoka jamii za kiasili, huku 13% wakiwa wakimbizi au wahamiaji. Takriban Waandishi 900 wa Ripoti - U walishiriki kutoka Italia.

Vijana wanaharakati wa mazingira huko Dubai
Vijana wanaharakati wa mazingira huko Dubai

Msingi wa matokeo uchunguzi: Asilimia 24% ya waliohojiwa walisema hawajawahi kupata taarifa kuhusu hali ya tabianchi shuleni, 33% waliamini kuwa hawakujifunza vya kutosha, huku 32% walisema wamejifunza mengi kuhusu mabadiliko ya tabianchi shuleni. 65% ya waliohojiwa walikubaliana na taarifa kuwa “Ikiwa sitajifunza kuhusu mabadiliko ya tabianchi na kukabiliana nayo, maisha yangu ya baadaye yatakuwa hatarini.” Asilimia 48 ya waliohojiwa wanaamini kuwa wanaelewa jinsi wanavyoweza kuchangia katika kubadilisha sera za tabianchi nchini mwao, huku 32% hawaelewi jinsi ya kufanya hivyo. 66% ya waliohojiwa wanaamini kwamba matendo yao yanaweza kutoa matokeo  vyema  ya sera za tabianchi katika nchi zao. 58% ya waliohojiwa wanaamini kuwa wanapokea mafunzo na ujuzi unaohitajika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na athari zake. Matokeo ya utafiti yalichangia Azimio la Kimataifa la Vijana, chombo cha viongozi wa dunia kutoa sauti zao katika Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28).

Matendo madhbuti ndiyo yanayotakiwa
Matendo madhbuti ndiyo yanayotakiwa

Ripoti - U ni jukwaa la ujumbe kwa ajili ya ushiriki wa barubaru na vijana na jumuiya. Ikiwa na zaidi ya wanachama milioni 32 katika nchi 99 duniani kote, ni chombo muhimu cha kubadilishana habari, kuongeza ufahamu na kukusanya takwimu zinazoweza kutambulika kuhusu maeneo maalum ambayo huathiri watoto, ikiwa ni pamoja na wale walio hatarini zaidi. Majibu yaliyopokelewa huchanganuliwa kwa wakati halisi, kuchorwa na kuoneshwa kwenye ubao wa umma.

12 December 2023, 14:56