Tafuta

Mgogoro kati ya Iran, Siria na Israeli. Mgogoro kati ya Iran, Siria na Israeli.  (AFP or licensors)

Malengo ya Iran yapigwa huko Siria na Iraq.Mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran

Mvutano kati ya Iran na upande mmoja na Israel na Marekani ni mkubwa,baada ya kuuawa kwa jenerali wa Pasdaran huko Damascus na kushambuliwa kwa mabomu kwa wanamgambo wanaoiunga mkono Iran nchini Iran.Katika ripoti ya Wakala wa Umoja wa Mataifa wa nishati ya nyuklia,(IAEA)Tehran imerejea kuzalisha uranium iliyorutubishwa sana.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Jenerali Sayyed Razi Mousavi, mkongwe wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, anayehusika na wanamgambo wa Tehran nchini Siria, aliuawa siku ya Noeli tarehe 25 Desemba 2023 katika uvamizi wa kombora katika eneo la vijijini la Damasco. Maneno makali yalitoka kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Iran, kuwa Israel hakika italipa uhalifu huo,  alitishia Rais wa Iran Ebrahim Raisi. Hali hiyo inachangiwa zaidi na mashambulizi ya Marekani, yaliyotokea usiku kati ya tarehe 25 na 26 Disemba, dhidi ya maeneo matatu ya vikosi vya Washia wanaounga mkono Iran nchini Iraq. Uvamizi huo ulisababisha kifo 1 na majeruhi 24. Rais wa Marekani, Joe Biden, binafsi alifuatilia shughuli hizo. Kulingana na ripoti iliyotolewa na Pentagon, mkuu wa Ikulu alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin, na maafisa wengine wa usalama wa kitaifa.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanaona uhusiano kati ya hatua za Israel na zile za Marekani katika siku za hivi karibuni katika ardhi za Siria na Iraq, kuwa ngumu kwa kuzingatia kwamba mwaka 2020 Wamarekani walimuua Jenerali wa Iran, Qassem Suleimani, kamanda wa vikosi vya Quds, ambaye Mousavi alikuwa mshirika wake wa karibu, nchini Irak kupigwa nchini Siria. Wakati huo huo, hata hivyo, serikali ya Baghdad imeshutumu mashambulizi ya mabomu na kuzungumzia "ukiukwaji wa uhuru" na kutaja shambulio hilo kama "kitendo cha uadua wa wazi."

Kwa kuongezea kiwango cha wasiwasi pia ni ripoti mpya kutoka kwa wakala wa Umoja wa Mataifa wa Nishati ya Nyuklia(IAEA)ambao wanaripoti jinsi ambavyo Iran imerejea katika majuma ya hivi karibuni kwa kiwango cha juu cha uzalishaji wa uranium iliyorutubishwa hadi  asilimia 60%, kuendelea na ongezeko lake la nyuklia, hata kama Tehran inakataa kuthibitisha bomu la atomiki. Ripoti ya IAEA ilisema kuwa wakaguzi wake wamekuwa wakikagua kiwango cha uzalishaji kilichoongezeka tangu mwishoni mwa Novemba katika vituo vya Natanz na Fordow. Kufuatia na ukaguzi wao inawakilisha kurudi kwa viwango vya awali vya uzalishaji. Ongezeko la shughuli ya kurutubisha madini ya uranium ilianza baada ya kuzuka kwa mzozo kati ya Israel na Hamas.

Habari za ulimwwengu na ghasia zake
28 December 2023, 11:34