Tafuta

COP28  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa COP28 huko Dubai. COP28 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa Mkutano wa COP28 huko Dubai.  (ANSA)

COP28:Guterres,kwa miaka 2 ijayo,serikali ziandae mipango mipya ya utekelezaji wa tabianchi kitaifa

Katika makubaliano ya kihistoria kwenye hitimisho la kilele cha mkutano wa COP28,Dubai unaashiria mwanzo wa mwisho wa nishati ya mafuta.Katibu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa:"Enzi zake lazima ziishe kwa haki na uadilifu.Katika kipindi cha miaka miwili ijayo,serikali zitahitaji kuandaa mipango mipya ya utekelezaji wa tabianchi kitaifa katika uchumi mzima.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Katika tamko la Bwana Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wakati hotuba yake ya kuhitimisha COP28 huko Dubai tarehe 12  Desemba 2023 alisema kuwa: “Kwa wale ambao walipinga marejeo ya wazi ya kuondoa nishati ya mafuta katika maandishi ya COP28, ninataka kusema kwamba kuondoa nishati ya mafuta ni jambo lisiloepukika, tupende usipende. Tuwe na matumaini kuwa haitachelewa sana. Bila shaka, ratiba, njia na malengo yatakuwa tofauti kwa nchi katika viwango tofauti vya maendeleo. Lakini juhudi zote lazima zilingane na kufikia sifuri halisi duniani ifikapo 2050 na kudumisha lengo la nyuzi 1.5. Na nchi zinazoendelea lazima ziungwe mkono kila hatua. Enzi ya mafuta lazima iishe na lazima ziishe kwa haki na usawa.” Mkataba wa Mfumo, alisisitiza, ulifanyika katika wakati madhubuti katika mapambano dhidi ya mzozo wa tabianchi, wakati ambao unahitaji matarajio makubwa katika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na katika haki ya tabianchi. Masuala ya mpito wa nishati na mustakabali wa nishati ya mafuta yalikuwa katikati ya tahadhari.

Kwa mujibu wa Karibu Mkuu alisisitza kuwa Global Stocktake (yaani chombo kinachosimamia hatua na usaidizi wa tabianchi)kimethibitisha wazi umuhimu wa kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi 1.5, jambo ambalo linahitaji kupungua kwa kasi kwa utoaji wa gesi chafuzi duniani muongo huu. Zaidi ya hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa aliongeza, “kwa mara ya kwanza, matokeo yanatambua haja ya kuacha nishati ya mafuta, baada ya miaka mingi ambayo majadiliano juu ya suala hili yamezuiwa. Sayansi inatuambia kuwa kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi 1.5 haitawezekana bila kuondoa nishati zote za mafuta katika vipimo vya nyakati vinavyopatana na kikomo hiki. Hili limetambuliwa na muungano unaokua na tofauti wa nchi.”

“Wakati huo huo, COP28 iliidhinisha ahadi ya kuongeza mara tatu uwezo wa nishati mbadala na ufanisi maradufu wa nishati ifikapo 2030,” aliendelea Bwana Guterres, akikumbuka kuwa mafanikio pia yamepatikana kuhusiana na kukabiliana na hali na fedha. “Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, serikali zitahitaji kuandaa mipango mpya ya utekelezaji wa tabianchi kitaifa katika uchumi mzima. Mipango hii lazima iwiane na lengo la nyuzijoto 1.5 na kufunika gesi chafuzi zote”, alisisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba “lazima pia ziungwe mkono na sera na kanuni zinazoaminika za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na kujumuisha bei ya kaboni na kukomesha ufadhili wa mafuta.

Na utayarishaji na utekelezaji wa mipango hii lazima ufadhiliwe kikamilifu na kuungwa mkono. Lakini - alionya -"mengi zaidi yanahitajika kuweka tumaini la kiwango cha nyuzi 1.5 hai na kuhakikisha haki ya tabianchi kwa wale walio mstari wa mbele wa shida. Nchi nyingi zilizo hatarini zinazama katika deni na hatari ya kuzama katika bahari inayoongezeka. Ni wakati wa kuongeza fedha ikiwa ni pamoja na kurekebisha, hasara na uharibifu na mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa. Dunia haiwezi kumudu ucheleweshaji, maamuzi au hatua nusu. Nina imani kuwa licha ya tofauti nyingi, dunia inaweza kukusanyika na kukabiliana na changamoto ya mzozo wa tabianchi.

Mipango hii lazima iwiane na lengo la nyuzijoto 1.5 na kufunika gesi chafuzi zote", alisisitiza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huku akisisitiza kwamba: "lazima pia ziungwe mkono na sera na kanuni zinazoaminika za tabianchi, ikiwa ni pamoja na kujumuisha bei ya makaa na kukomesha ufadhili wa mafuta. Na utayarishaji na utekelezaji wa mipango hii lazima ufadhiliwe kikamilifu na kuungwa mkono." Lakini alionya kuwa "mengi zaidi yanahitajika kuweka tumaini la kiwango hai cha nyuzi 1.5 na kuhakikisha haki ya tabianchi kwa wale walio mstari wa mbele katika  shida. Nchi nyingi zilizo hatarini zinazama katika deni na hatari ya kuzama katika bahari inayoongezeka. Ni wakati wa kuongeza fedha, ikiwa ni pamoja na kurekebisha, hasara na uharibifu na mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa. "Dunia haiwezi kumudu ucheleweshaji, maamuzi au hatua nusu. Nina imani kuwa licha ya tofauti nyingi, dunia inaweza kukusanyika na kukabiliana na changamoto ya mzozo wa tabianchi. Kuungana pande nyingi kunasalia kuwa tumaini bora la ubinadamu. Ni muhimu kukusanyika pamoja karibu na suluhisho halisi, la vitendo na la maana la tabianchi ambalo ni sawa na shida ya tabianchi,” alihitimisha.

Tamko la Guterres wakati wa kufunga COP28
14 December 2023, 11:53