Vita vinaendelea kwenye vitongoji katika Jiji la Gaza
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Kwa sasa kuna mapigano usiku na mchana katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi ya anga na mizinga ya Israel inafuatana mara kwa mara na kurushwa kwa makombora na mabomu. Na zaidi kwa kuingia wanajeshi katika Jiji la Gaza kunaweza kusababisha vita vya msituni vya muda mrefu na vya umwagaji damu. Serikali inayoongozwa na Beniamjn Netanyahu imetangaza kuwa: "tuko kwenye kilele cha kampeni, tutaendelea hadi ushindi". Wakati huo huo, hali ni ngumu kutokana na uwezekano wa kufunguliwa kwa upande wa kaskazini kwenye mpaka na Lebanon kutokana na maneno yaliyosemwa Ijumaa tarehe 3 Novemba 2023 katika ujumbe wa televisheni kutoka kwa Nasrallah, kiongozi wa Hezbollah, chama cha Kishii kinachounga mkono Iran.
Lengo la kupambana na Hamas
Kiukweli, vitendo vya Israel vinazidi kuenea kila kona. Wanamgambo wa Hamas wanatumia mtandao tata wa maandaki katika maeneo ya chini ya Ukanda huo ambao unaruhusu harakati za askari na silaha bila kuteseka na mashambulizi yoyote kutoka angani. Maandaki ya Kundi hilo la Harakati pia yapo chini ya hospitali na shule. Na hospitali ya Quds huko Gaza ilikuwa eneo la mapigano makali. Wakati hospitali ya al-Shifa katika Mji wa Gaza, ambayo ni kubwa zaidi katika Ukanda huo, kulingana na jeshi la Israel, ni nyumba ya ghala muhimu la mafuta na ni mwenyeji wa kamanda mkuu wa Hamas. Na mlango wa hospitali hiyo pia ulipigwa na uvamizi wa Israel ambao ulisababisha vifo vya watu sita. Hii imeripotiwa na shirika la utangazaji la al-Jazeera, likibainisha kuwa msafara wa magari ya wagonjwa yalilengwa ambayo yalitakiwa kuwasafirisha majeruhi na wagonjwa kuelekea kivuko cha Rafah. Vyanzo vya matibabu vilivyotajwa na mtangazaji vinazungumza juu ya mauaji. Mapigano na waathiriwa pia katika Ukingo wa Magharibi.
Ziara ya Waziri Blinken wa Mambo ya Nchi za Nje,Marekani
Wakati huo huo, Ikumaa 3 Novemba 2023 amaefanya ziara mpya nchini Israel ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Bwana Anthony Blinken. Kwa njia hiyo Marekani inasisitiza kuwa katika muktadha wa vita hivyo kumekuwepo na misimamo ya kibinadamu ili kuruhusu kuingia katika Ukanda wa Gaza kwa mahitaji ya kimsingi, kuondoka kwa raia wengi iwezekanavyo na kuachiliwa mateka mikononi mwa Hamas, suala jingine muhimu ambalo bado halijaonekani kutatuliwa. Hata hivyo, idadi ya vifo inaongezeka kwa kasi. Kwa sasa inasadikika kuwa zaidi ya watu 1,400 waliuawa katika uvamizi wa Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, na zaidi ya watu 9,000 katika mashambulizi ya Israel hadi sasa.