Tafuta

UNICEF's Copenhagen warehouse prepares aid for Gaza

UNICEF,Italia yazindua kampeni ya watoto kati ya vita na dharura zilizosahauliwa

UNICEF Italia mwaka 2023 inaadhimisha Siku ya Watoto na Vijana Duniani inayofanyika kila mwaka tarehe 20 Novemba kwa ajili ya haki ya amani na kuzindua kampeni yenye kauli mbiu Watoto kati ya vita na dharura zilizosahaulika kwa kuzingatia nchi ya:Palestina/Israel,Haiti,Siria, Sudan,Ukraine na Yemen.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kila tarehe 20 ya kila mwaka ni siku ya watoto na vijana iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1954. UNICEF Italia mwaka huu 2023 inataka kuadhimisha Siku ya Watoto na Vijana Duniani  kwa ajili ya haki ya amani na kuzindua kampeni yenye kauli mbiu "Watoto kati ya vita na dharura zilizosahaulika", kwa kuzingatia nchi ya Palestina/Israel, Haiti,Siria, Sudan, Ukraine na Yemen. Kwa hiyo Duniani kote, mashambulizi dhidi ya watoto yanaendelea bila kukoma: zaidi ya watoto milioni 400 wanaishi katika maeneo yenye migogoro. Kulingana na Umoja wa Mataifa, kati yam waka 2005 na 2022, inakadiriwa watoto 120,000 wameuawa au kulemazwa na vita ulimwenguni kote, wastani wa karibu watoto 20 kila siku. Migogoro inawajibika kwa asilimia 80 ya mahitaji yote ya kibinadamu na inatatiza upatikanaji wa mahitaji ya kimsingi, kama vile chakula na maji, na kuwalazimisha watu kuingia kwenye umaskini uliokithiri. Baadhi ya takwimu kutoka nchi sita zinazoripotowa  kwa Ufupi ni kwamba kuanzia tarehe 7 Oktoba hadi 15 Novemba, kwa mujibu wa  habari zilifikiwa UNICEF watoto 4,609 waliuawa na zaidi ya 9,000 kujeruhiwa katika Ukanda wa Gaza.

Philipe Lazzarini kamishna mkuu wa Umoja wa mataifa wa UNRWA
Philipe Lazzarini kamishna mkuu wa Umoja wa mataifa wa UNRWA

Katika Israel, watoto 33 waliuawa. Wanawake na watoto wanachangia theluthi mbili ya vifo vilivyoripotiwa. Katika  nchi ya Ukraine, kutokana na zaidi ya miaka 2 ya vita, maisha ya watoto ni hatari. Kufikia Oktoba  tarehe 8, zaidi ya watoto 1,750 wamepoteza maisha au kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 560 waliouawa na karibu 1,200 kujeruhiwa, hasa kutokana na mabomu; Nchini Siria, baada ya zaidi ya miaka 12 ya migogoro, watu milioni 15.3 (karibu 70% ya watu), watoto milioni 7, watu milioni 2.6 wenye ulemavu, wakimbizi wa ndani milioni 5.3 wanahitaji msaada; Nchini Yemen, zaidi ya miaka 8 ya migogoro imeharibu maisha ya mamilioni ya watoto. Watu milioni 21.6, wakiwemo watoto milioni 11.1, wanahitaji aina moja au zaidi ya usaidizi wa kibinadamu; Nchini Sudan, vita vinahatarisha afya na ustawi wa watoto milioni 24 wa Sudan. Watoto milioni 3 wamefurushwa kwa lazima, ikiwa ni janga kubwa zaidi la kuhama kwa watoto duniani.

Watoto wanatesaka Sudan Kusini
Watoto wanatesaka Sudan Kusini

Nchini Haiti, takriban nusu ya idadi ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na karibu watoto milioni 3, waathirika wa historia ngumu ya umaskini, ukosefu wa utulivu wa kisiasa na hatari za asili. Watoto wanabeba mzigo mkubwa wa ulimwengu katika shida, na mamilioni ya watu wanajitahidi kuishi. Migogoro na migogoro katika sehemu moja ya dunia inaweza kuathiri maisha ya watoto maelfu ya maili. Watoto hawaanzishi migogoro na hawana uwezo wa kuizuia. Wanahitaji sisi sote kuweka usalama wao kwanza na kufikiria siku zijazo ambapo wao ni afya, salama na elimu. Hakuna mtoto anayestahili chini. Siku ya Kimataifa ya Watoto na Vijana" inawakilisha fursa adhimu ya kukuza na kueneza ufahamu kuhusu haki za watoto wote. Kwa kuzingatia tarehe 20 ijayo ya Novemba, UNICEF Italia imezipatia shule za viwango vyote baadhi ya zana ambazo zinaweza kuwasaidia walimu kuunda, ndani ya madarasa, nyakati za utafiti wa kina unaozingatia haki za vijana wote wa kike na kiume. Siku ya Kimataifa ya Watoto na Vijana ilianzishwa mwaka 1954 kwa Azimio 836 (IX) na huadhimishwa kila tarehe 20 Novemba kila mwaka.

Wakimbizi wa Siria wakiwa na watoto
Wakimbizi wa Siria wakiwa na watoto

Lengo ni kukuza mshikamano wa kimataifa, ufahamu miongoni mwa watoto duniani kote na kuboresha ustawi wao. Tarehe 20 Novemba 1959 ni tarehe muhimu kwani ndiyo siku ambayo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Tamko la Haki za Mtoto. Tarehe nyingine muhimu ni 1989 wakati Baraza Kuu lilipitisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watoto na Vijana. Akina mama na baba, walimu, wauguzi na madaktari, viongozi wa serikali na wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wanajumuiya za kitawa na wazee, wafanyabiashara wakubwa na wataalamu wa vyombo vya habari, pamoja na vijana na watoto wenyewe, wanaweza kuchukua jukumu muhimu katika kuakisi umuhimu wa maadhimisho haya katika jamii, jumuiya na mataifa yao. Siku ya Watoto na Vijana Duniani inampatia kila mmoja wetu mwanzo mzuri wa kuunga mkono, kukuza na kusherehekea haki za watoto kupitia midahalo na uingiliaji kati ili kujenga ulimwengu bora kwa watoto.

Wakimbizi wa Rohinya na watoto wako
Wakimbizi wa Rohinya na watoto wako

Kuna zaidi ya watoto milioni saba walionyimwa uhuru wao duniani kote. Wengi wa hawa wanaishi katika vituo vya kuwazuilia wahamiaji, gerezani au katika "taasisi za mapokezi", kama vile vituo vya watoto yatima. Na mara nyingi wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi za unyanyasaji, vurugu, ubaguzi wa kijamii na kunyimwa haki zao za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Kunyimwa uhuru wa watoto ni suala la msingi kwa sababu huathiri maendeleo ya kibinafsi ya watu wazima wajao. Papa Francisko mara kadhaa  anapenda kusema ni kuwaibia ndoto zao. Bado hadi miaka michache iliyopita haijawahi kushughulikiwa kwa njia ya kikaboni na ya kupita. Mabadiliko yalikuja mnamo 2014, wakati Umoja wa Mataifa uliamua kuagiza utafiti wa kimataifa.

16 November 2023, 17:02