Tafuta

Wizara ya Mambo ya Ndani,Waafghanistani milioni 1.3 wamesajiliwa kama watafuta hifadhi nchini Pakistani huku 800 elfu wametambuliwa kama wakimbizi. Wizara ya Mambo ya Ndani,Waafghanistani milioni 1.3 wamesajiliwa kama watafuta hifadhi nchini Pakistani huku 800 elfu wametambuliwa kama wakimbizi.  (AFP or licensors)

Pakistan,Waafghanistan milioni 1.7 wana hatari ya kurejeshwa makwao

Kwa mujibu wa takwimu rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani,Waafghani milioni 1.3 wamesajiliwa kama watafuta hifadhi nchini Pakistani huku 800 elfu wametambuliwa kama wakimbizi.Mbali na hao,kuna watu milioni 1.7 wanaoishi nchini kinyume cha sheria,kwa sababu hawana hati za kawaida na hawatambuliwi kama waomba hifadhi au wakimbizi.

Vatican News.

Pakistan si mahali salama tena kwa wakimbizi wanaotoka Afghanistan bila vibali muhimu: hawa ni watu milioni 1.7 ambao sasa wako chini ya kukamatwa na kufukuzwa kwa lazima. Tarehe 3 Oktoba 2023, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistani Sarfraz Bugti alikuwa ametoa taarifa ambayo muda wake uliisha  tarehe 1 Novemba 2023, ambapo alitoa muda wa mwezi mmoja kuondoka kwa hiari nchini kwa sehemu ya jumuiya kubwa ya Afghanistan ambao walikuwa wamekimbilia katika nchi jirani ya Pakistan. Msemaji wa Amnesty International Italia Bwana Riccardo alisema hayo kwa vyombo vya Habari vya Vatican News - Vatican, kuwa, "Iwapo uamuzi huu ulioisha muda wake utafuatiwa na kufukuzwa kwa wingi katika nchi ambayo ni maskini na iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi la hivi karibuni, maisha ya watu hawa yatakuwa hatarini."

Jumuiya ya Waafghan nchini Pakistan

Kulingana na takwimu rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, kiukweli, Waafghani milioni 1.3 wamesajiliwa kama watafuta hifadhi nchini Pakistan,  huku 800 elfu wametambuliwa kama wakimbizi. Mbali na hao, kuna watu milioni 1.7 wanaoishi nchini kinyume cha sheria, kwa sababu hawana hati za kawaida na hawatambuliwi kama waomba hifadhi au wakimbizi. "Ukweli kwamba hawana nyaraka sahihi sio kosa lao," anaelezea Noury. Kwa hakika, hadhi ya ukimbizi inathibitishwa na hati iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa lakini taratibu hizi ni za polepole sana, alielezea. "Tunajua kuhusu vitisho, vitisho na majaribio ya unyang'anyi ya maafisa wa Pakistani dhidi ya watu hawa. Kwa hivyo, kwa muhtasari, ni kutowajibika kwao kulipa uzembe na ucheleweshaji wa wengine", anatangaza msemaji wa Amnesty Italia.

Uhamisho wa Wafghanistan umekuwa ukiendelea kwa miongo

Uhamisho wa Afghanistan kuelekea Pakistan umekuwa ukiendelea kwa miongo kadhaa. Mitiririko ya kwanza ni ya miaka ya 1970, ikichochewa na utaftaji wa fursa bora za kiuchumi, kisha kutoroka kutoka katika  uvamizi wa Kisoviet katika miaka ya 1980 na kutoka katika serikali ya kwanza ya Wataliban katika miaka ya 1990. Walakini, tangu Waaliban warudi madarakani mnamo Agosti 2021, inakadiriwa kuwa zaidi ya Waafghan 600,000 wamewasili. Lakini wengi wao waliishia katika kambi za wakimbizi ambako walikabiliwa na hali mbaya ya maisha iliyoonesha wazi wa ukosefu au  upatikanaji mdogo wa elimu, huduma za afya na kazi.

03 November 2023, 18:24