Tafuta

Watoto njiti katika hospitali ya Al Shifa huko Gaza ambao wanahitaji msaada mkubwa. Watoto njiti katika hospitali ya Al Shifa huko Gaza ambao wanahitaji msaada mkubwa.  

Israel,kuzingirwa kwa hospitali ya Al Shifa kunazuia kuachiliwa mateka

Wakati Gaza ikiwa katika machafuko na wahanga zaidi ya elfu 11 wa Palestina,nyuma na mbele kati ya UN na Israel inaongezeka:Katibu Mkuu wa UN, Bwana Guterres, amerejea kushutumu kushindwa kuwalinda raia;na wakati huo huo Waziri Mkuu Netanyanu akajibu kuwa anapaswa kushutumu Hamas.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Hali halisi ya ghasia za vitan kati ya Israel na Palestina inazidi kuwa ngumu kila kukicha. Matangazo na kukanusha yanaenea karibu na uwezekano wa kuachiliwa kwa baadhi ya wale waliotekwa nyara na Hamas. Kitu chenye mzozo sasa, kwa kundi la Kiislamu ni kuzingirwa kwa kituo cha afya ambapo watoto na wagonjwa walikufa kutokana na ukosefu wa rasilimali muhimu. Wakati huoo huo Umoja wa Mataifa umerejea kuishambulia Israel kwa kushindwa kuwalinda raia huko Gaza. Kwanza kuna tetesi za Hamas za makubaliano ya kuachiliwa wanawake na watoto 80 wa Israel kwa kubadilishana na wanawake na vijana wa Kipalestina wanaozuiliwa nchini Israel. Ndipo makubaliano hayo yalisitishwa na Hamas baada ya mzingiro mkali uliofanywa katika hospitali ya Al Shifa kupigishwa magoti na ukosefu wa mafuta muhimu kwa ajili ya miundombinu ya afya, upungufu ambao tayari umesababisha vifo vya watoto wachanga 5 na wagonjwa 7 waliokuwa mahututi.

Hofu kuhusu kuongezeka vifo katika kituo cha afya

Youssef Abu Rish, naibu waziri wa Afya katika Ukanda huo alitangaza kuwa "Tunahofia kwamba idadi ya watu inatazamiwa kuongezeka- kutokana na mapigano yanayoendelea na uhaba wa mafuta. Muktadha ambao unashuhudia kuongezeka kwa shutuma kati ya Hamas na Israel juu ya kundi hilo kukataa lita 300 za mafuta. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, wakati akiendelea kukataa kusitishwa kwa mapigano, hauondoi makubaliano juu ya mateka, lakini unapelekea makumi ya Adanim, mawakala wa kijasusi, kuwa uwanjani kwa mara ya kwanza,ambao ujumbe wao kama ilivyoelezwa na mamlaka ya Israeli, ni kuongoza kwa uratibu wa haraka wa nguvu kwa kuchanganya akili sahihi ya kulenga.

UN:Israel haiwalindi raia

Na wakati Gaza iko katika machafuko na wahanga zaidi ya elfu 11 wa Palestina, nyuma na mbele kati ya UN na Israel inaongezeka: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Antonio Guterres, alirejea kushutumu kushindwa kuwalinda raia; na wakati huo huo Waziri Mkuu Netanyanu akajibu: "Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anatushambulia badala ya wale wajeuri wa Hamas." Na Wakati huo huo, njia ya masaa 7 ya kibinadamu imefunguliwa kwa Wapalestina kuelekea kusini mwa Gaza.

Gaza,waathiriwa makao makuu ya UNDP:mauaji ya raia lazima yakomeshwe

Na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limesema mabomu ya jana usiku yalisababisha vifo na majeruhi kadhaa. Wakati mkuu wa majeshi ya Israel akielekea Ukanda huo, Waziri Mkuu Netanyahu amedhamiria kuwashinda Hamas kwa gharama yoyote kwa nia ya kuweka udhibiti kamili wa usalama. Kwa hiyo Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa lilitangaza "idadi kubwa ya vifo na majeruhi" katika "mashambulio ya mabomu" katika makao makuu yake katika Jiji la Gaza, yaliohamishwa na wafanyakazi wake na sasa yamekaliwa na mamia ya Wapalestina waliokimbia makazi yao. "Maafa yanayoendelea ya raia waliofariki na kujeruhiwa walionaswa katika mzozo huu lazima yakomeshwe," UNDP ilisema katika taarifa yake kuwa . "Raia, miundomsingi ya kiraia na kutokiuka kwa miundo ya Umoja wa Mataifa lazima iheshimiwe na kulindwa wakati wote. Sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kanuni za kutofautisha, uwiano na tahadhari, lazima ziheshimiwe na kuungwa mkono" .

Israeli inahakikisha ukanda wa kibinadamu

Pia  tarehe 12 Novemba 2023  jeshi la Israel lilihakikisha mikondo ya  misaada ya kibinadamu kwa saa 7 (hadi saa kumi jioni saa za huko, saa 3 usiku nchini Italia) kwa wakazi wa Palestina wanaotaka kuhama kutoka kaskazini hadi kusini mwa Ukanda huo. Msemaji wa jeshi Avichai Adraee alisema haya kwenye X kwa lugha ya  Kiarabu. Mtaa unaohusika ni Salah ad Din. Adraee aliongeza kuwa kutakuwa na ukanda salama kutoka hospitali ya Shifa hadi mji wa Gaza kwa wale wanaotaka kufika Salah ad Din na kusitishwa kwa "mbinu" katika operesheni za kijeshi kutahakikishwa (hadi saa 2 usiku kwa saa za huko) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalya kaskazini mwa Ukanda na katika kitongoji cha karibu na  Izbat Malien.

Netanyahu anakataa usitishaji mapigano

Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu alikataa wito unaoongezeka wa kimataifa wa kusitisha mapigano siku ya Jumamosi, 11 Novemba akisema vita vya Israel kuwaangamiza wapiganaji wa Hamas wanaotawala Gaza vitaendelea kwa "nguvu kamili." Usitishaji wa mapigano utawezekana tu ikiwa mateka wote 239 wanaoshikiliwa na wanamgambo huko Gaza wataachiliwa, alisema katika hotuba yake ya  televisheni. Kuhusiana na hilo, katika mahojiano na NBC, alisema kwamba makubaliano ya kuachiliwa kwa baadhi ya mateka mikononi mwa Hamas "yanaweza kuwepo". Kiongozi huyo wa Israel pia alisisitiza kuwa baada ya vita hivyo, vilivyoingia katika wiki yake ya sita, Gaza itaondolewa kijeshi na Israel itadumisha udhibiti wa usalama. Pia alikataa wazo kwamba Mamlaka ya Palestina, ambayo kwa sasa inasimamia maeneo yanayojitawala katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, inaweza wakati fulani kudhibiti Gaza.

Mkurugenzi wa Al-Shifa: tayari kuhama kama Israel itaruhusu

Mkurugenzi wa hospitali ya Al-Shifa ya Gaza, Mohammad Abu Salmiya, alisema wafanyakazi wa matibabu na wagonjwa wako tayari kuhamishwa mara moja ikiwa Israel itaruhusu. Alitangaza haya kwenye Radio Ashams huko Nazareti, iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Israeli. Aliongeza kuwa uingiliaji kati wa mashirika ya kimataifa ni muhimu ili kuhakikisha uhamishaji salama kwenye kituo cha matibabu katika sehemu ya kusini ya Ukanda huo. Ilirejelea zaidi ya wagonjwa 700, wakiwemo watu wanaotumia mashine za kusafisha damu na watu waliojeruhiwa, na vifo vitatu na vifo vinne zaidi katika siku mbili zilizopita kutokana na ukosefu wa oksijeni na usafishaji wa damu.

13 November 2023, 10:47