Tafuta

2023.11.13 Upumzike kwa amani Indi Gregory.Umekataliwa maisha hata kwa kusindikizwa kama ilivyokuwa imeombwa na wengi. 2023.11.13 Upumzike kwa amani Indi Gregory.Umekataliwa maisha hata kwa kusindikizwa kama ilivyokuwa imeombwa na wengi. 

Indi Gregory mtoto wa Kiingereza amefarik,Baba anaonesha hasira

Mtoto mdogo Indi Gregory wa Kiingereza amefariki dunia ambaye alikuwa na ugonjwa nadra sana wa mitocondry,kwa namna moja ni kama kuhukumiwa kufa na Mahakama kuu ya London,kukatisha matibabu yaliyokuwa yakimsaidia kuishi.Papa Francisko alikuwa amemwombea na familia yake siku chache zilizopita.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mtoto mdogo  wa Kiingereza Indi Gregory amefariki dunia, Jumatatu tarehe 13 Novemba 2023 majira ya saa 1,45 asubuhi masaa ya Kiingereza huko London, ambaye alikuwa ameondolewa kwenye msaada wa maisha uliomtunza hadi sasa, kutokana na ugonjwa wake nadra sana. Hayo yalithibitishwa na wakili Simone Pillon na Iacopo Coghe wa Utetezi wa maisha ambao ni sehemu ya timu ya wanasheria ya familia ya Gregory.

Baba ya Indi: "Tuna hasira na tumejaa aibu"

"Maisha ya Indi yamekwisha saa 1:45, asubuhi  mimi na Claire tuna hasira, tumeumia moyo, tuna aibu." Hayo yalikuwa ni maneno ya Dean, baba yake Indi Gregory, katika ujumbe kwa mawakili wake. "NHS na mahakama hazikuchukua tu nafasi yake ya kuishi, pia zilimwondolea heshima ya kufa katika nyumba ya familia alimokuwa," ameandika. "Claire alikaa pamoja naye hadi pumzi yake ya mwisho," anaandika baba ya Indi, Dean Gregory, katika ujumbe uliotumwa kwa wanasheria wake, akizungumzia dakika za mwisho za binti yake karibu na mama yake. “Walifanikiwa kuuchukua mwili wa Indi na hadhi yake, lakini hawataweza kuitoa roho yake, walijaribu kumuondoa Indi bila mtu yeyote kujua, lakini tulihakikisha anakumbukwa milele, nilijua kuwa yeye ni maalum tangu siku hiyo alipozaliwa."

Meloni: "Uwe na safari njema Indi, tulifanya kila tuwezalo"

Kwa upande wa Waziri Mkuu Giorgia Meloni wa Jamhuri ya Italia kufuatia na tukio hili la kusikitisha, ameandika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kuwa, "Tulifanya kila tuliloweza, kila liwezekanalo. Kwa bahati mbaya haikutosha. Uwe na safari salama, Indi mdogo."

Mtoto alipata uraia wa Italia akakataliwa

Ikumbuwe Jamhuri ya Italia ilikuwa imempatia uraia mtoto huyo mdogo ili akatibiwa katika moja ya Hospitali maalum ya watoto Bambino Gesu, Hospitali ya Kipapa, ambayo ilikuwa imsindikiza katika ile njia iitwayo Shufaa, ya kumfanya asindikizwe katika hali yake, lakini, Mahakama kuu ya London chini Uingereza haikukubali, kwa kile ambacho madkatari walisema hawezi kupona.


Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 11 Novemba 2023 pia alikuwa ametoa ombi lake kwa ajili ya mdogo huyo Indi na kuwaombea wazazi wake. Hata hivyo siyo kwa mara ya kwanza  ya kesi kama hii kuwaombea, kwani Baba Mtakatifu Francisko mara kdhaa amekuwa akitoa mwaliko juu ya kuheshimu maisha tangu kutungwa kwake hadi kifo cha hadhi ya binadamu!

13 November 2023, 09:56