Tafuta

Tanzania imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike 245 kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya kwa mkoa wa Mara. Tanzania imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike 245 kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya kwa mkoa wa Mara. 

Ukeketaji ni Ukatili Dhidi ya Utu, Heshima na Haki Msingi za Wanawake Duniani

Madhara yanayosababishwa na ukeketaji yanaweza kuwa ya papo kwa papo kama maumivu makali wakati wa ukeketaji, mshtuko, homa kali, kumwaga damu nyingi na mara nyingine hata kupelekea kifo, kuambukizwa magonjwa kama Virusi vya ugonjwa wa UKIMWI na wakati mwingine wakijikuta wanatumbukia katika ugonjwa wa Sonona. Tanzania imeanza mpango mkakati wa kutokomeza ukeketaji tangu mwaka 2021 hadi mwaka 2025: Utu, heshima na haki msingi!

Na WMJJWM, - Dar Es Salaam, Tanzania

Wataalamu wa afya wanasema, madhara yanayosababishwa na ukeketaji yanaweza kuwa ya papo kwa papo kama maumivu makali wakati wa ukeketaji, mshtuko, homa kali, kumwaga damu nyingi na mara nyingine hata kupelekea kifo, kuambukizwa magonjwa kama Virusi vya ugonjwa wa UKIMWI na wakati mwingine wakijikuta wanatumbukia katika ugonjwa wa Sonona. Yapo pia madhara ya muda mrefu kama vile; kuathirika kisaikolojia, ulemavu au kovu la kudumu katika uke, fistula, kupata shida wakati wa kujifungua na muda mwingine kupelekea kupata ugumba. Mtandao wa Mashirika yanayopinga ukeketaji sehemu mbalimbali za dunia umeendelea kusimama imara katika kuhahikisha kuwa ukeketaji unakoma ifikapo 2030. Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu kufikia mwaka 2030 ni mchakato wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inajizatiti katika kutokomeza umaskini, baa la njaa na magonjwa duniani. Watu wanapaswa kupatiwa elimu bora, kwa kuhakikisha usawa wa kijinsia pamoja na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote.

Ukeketaji ni ukatili dhidi ya utu, heshima na haki msingi za wanawake
Ukeketaji ni ukatili dhidi ya utu, heshima na haki msingi za wanawake

Tanzania imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike 245 kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya kwa mkoa wa Mara katika msimu wa ukeketaji mwaka 2022. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa mdahalo kuhusu jitihada zinazofanywa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji unaovuka mipaka ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya Ukeketaji unaoendelea katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam Oktoba 10, 2023.

Ukeketaji ni suala linalogusa: mila, desturi, imani, uchumi na siasa
Ukeketaji ni suala linalogusa: mila, desturi, imani, uchumi na siasa

Katika mjadala huo ambapo washiriki wamepeana uzoefu wa jinsi ya kudhibiti watoto wasiende kukeketwa nje ya mipaka wakati wa misimu ya ukeketaji, Waziri Dkt. Gwajima amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Umma na binafsi liliwakamata watu zaidi ya 20 waliohusika na vitendo hivyo na baada ya zoezi hilo, Tanzania imeendelea kutoa elimu kwenye jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari. "Lakini haitoshi kusubiri msimu wa ukeketeji watoto wanakimbia wanavushwa mipaka ni lazima tujikite ndani kwenye jamii zetu ambapo Tanzania tumeshatengeneza Mkakati wa Kutokomeza Ukeketaji pamoja na Mpango kazi wake wa utekelezaji wa mwaka 2021 -2025" amesema Waziri Dkt. Gwajima.

Dkt. Doroth Gwajima wakati wa mdahalo juu ya ukeketaji Barani Afrika.
Dkt. Doroth Gwajima wakati wa mdahalo juu ya ukeketaji Barani Afrika.

Ameeleza kwamba mkakati huo utahusisha elimu na huduma kwa manusura wa ukeketaji pamoja na kufikia hadi ngazi ya vijiji kwa sababu ni suala la ukeketaji limekuwa sio tu mila na desturi bali kwenye imani, uchumi na siasa. "Jamii haiangalii tena madhara yanayotokana na ukeketaji kwa watoto wetu, suala hili limekuwa kama imani na kutumiwa na baadhi ya wanasiasa pia hivyo elimu kwa viongozi pia muhimu" ameongeza Waziri Gwajima. Wengine walioshiriki mdahalo huo ni Waziri wa Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii, kutoka Uganda, Mituuzo Peace Regis, Afisa Mtendaji Mkuu wa Masuala ya ukeketaji kutoka Kenya Bernadetha Loloju na Mkurugenzi wa masuala la Wanawake kutoka Ethiopia Seleshi Tadesse.

DKT Gwajima D.
11 October 2023, 11:47