Mkurugenzi Mkuu wa FAO ahutubia mzunguko wa Wakulima wa Afrika
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), QU Dongyu, mnamo tarehe 11 Oktoba 2023 alitoa wito wa kuchukua hatua za haraka ili kuisaidia bara la Afrika kurejea katika mwelekeo wa kufikia malengo ya kimataifa kuhusu usalama wa chakula na lishe, akielekeza kujihusisha na sayansi, teknolojia na uvumbuzi, uwekezaji na hifadhi la bara ya vijana wabunifu, kama suluhisho zinazowezekana. Bwana Qu alialikwa kuhutubia sehemu ya kwanza mjini Vatican kuhusu tukio la "Vatican Roundtable of African Farmers" lililoandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Maisha na Sayansi Jamii kwa kuwaweka Wakulima wa Afrika katikati ya mjadala na kutoa nafasi na sauti kwa uthabiti wao na mitazamo yao ya kipekee. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Fao alisema hili ni tukio lililoundwa ili kuwapa wakulima kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara fursa ya kuleta mitazamo yao ya kipekee na uzoefu madhubuti katika mstari wa mbele wa mijadala ya kimataifa juu ya maendeleo ya kilimo katika eneo lao. Watunga sera wa Afrika, viongozi wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya maendeleo, taasisi za fedha za kimataifa, sekta binafsi, wasomi, na mashirika ya kiraia pia walialikwa. Wakulima kutoka Kenya, Malawi, Nigeria, Sierra Leone, na Zimbabwe waliwasilisha miktadha yao madhubuti ya uvumbuzi na teknolojia ya kilimo na mapendekezo muhimu ya sera.
Idadi ya wasio na lishe bora imeongezeka
Mkutano huo ulifanyika siku chache kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano la Chakula Duniani kuanzia 16 hadi 20 Otoba 2023. Tukio kuu la kila mwaka la FAO limeundwa ili kukuza mazungumzo na mijadala kati ya wadau husika, kuanzia vijana na wakulima, wazalishaji wadogo, Watu wa Asilia, watunga sera, wawekezaji wa kilimo na wanasayansi, wote wakiwa na lengo moja la kuhamisha ufinyu wa uzalishaji wa usalama wa chakula ili kufikia upana wa uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora na maisha bora, bila kuacha mtu nyuma. Afrika imekuwa msisitizo mkubwa wa juhudi za FAO tangu kuanzishwa kwake, karibu miaka 60 iliyopita. Kwa bahati mbaya, idadi ya watu wasio na lishe bora imeongezeka hadi zaidi ya milioni 281 tangu kuzuka kwa janga la Uviko 19, wakati mizozo na shida ya hali ya tabia nchi inaendelea kulikumba bara hilo. Mwaka huu 2023 tu, Kimbunga Freddy kilipiga Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, na kuna ukame unaoendelea nchini Uganda na Somalia.
Na wakati Sudan, Mali, Niger na zingine zikiendelea kukabiliwa na mzozo, takwimu mpya iliyotolewa majuma mawili tu yaliyopita ilithibitisha kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kuwa moja ya shida kubwa zaidi za chakula duniani, ikiwa na robo moja ya watu - zaidi ya watu milioni 25 wanakabiliwa na shida au viwango vya dharura vya uhaba wa chakula. Hii yote ina maana kwamba Afrika haiko kwenye njia ya kufikia malengo ya kimataifa kuhusu usalama wa chakula na lishe yaliyowekwa katika Ajenda ya 2030, wala malengo ya Azimio la Malabo iliyokubaliwa na Wanachama wa Umoja wa Afrika. Kwa hiyo "Barani Afrika, tunahitaji mifumo ya kilimo bora zaidi na ya haraka, yenye ufanisi zaidi, inayojumuisha zaidi, thabiti na endelevu zaidi ili kuongeza tija ya kilimo kuwa mara 2 zaidi ya ilivyo sasa," alisema Bwana Qu
Ufumbuzi unaowezekana
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa FAO alijikita juu ya masuluhisho yanayoweza kutokea, na "jinsi gani tunaweza kufanya haraka kuyatekeleza. "Sayansi, uvumbuzi na teknolojia, kwa mfano, hutoa fursa muhimu kwa ukuaji wa uchumi na uundaji wa ajira mpya katika mifumo ya kilimo cha chakula kwa kuchangia katika kuzalisha zaidi na kidogo; kwa kupunguza upotevu wa chakula na upotevu, kwa kusaidia uzalishaji wa chakula kukabiliana na athari za mgogoro wa tabianchi, na kwa kuboresha upatikanaji wa fedha na taarifa za soko. Lakini ikiwa maendeleo yao yanapatikana tu kwa kila mtu. Pili, kuleta mabadiliko ya kweli na kwa kiwango kunahitaji uwekezaji, sio tu kwa ajili ya biashara za kilimo, lakini pia kwa utafiti wa kilimo, mafunzo kwa wakulima, utumiaji wa mashine, pamoja na kuanzishwa kwa teknolojia mpya na aina mpya za mazao, na mifumo endelevu ya uzalishaji. Katika muktadha huu, FAO inashirikiana na sekta ya kibinafsi kupitia mipango mikuu kama vile Hand-in-Hand Initiative, ambayo imeundwa ili kuharakisha mabadiliko ya kilimo na maendeleo endelevu ya vijijini na kwa sasa inajumuisha nchi 36 za Afrika.
Vijana wawezeshwe ambao ni wepesi na wabunifu
Hatimaye, kukiwa na asilimia kubwa ya vijana duniani, zaidi yapaswa kufanywa ili kuwawezesha vijana wa bara hilo, ambao ni wepesi, ubunifu na uwezo wao wa kuvumbua unaweza kuwa jambo la kubadilisha katika juhudi za kuondokana na umaskini na njaa katika kanda,” Alisema Bwana Qu. Hii ndiyo sababu ushiriki wa vijana ni mojawapo ya nguzo tatu za Kongamano la Chakula Duniani, ambalo Mkurugenzi Mkuu alilianzisha mnamo mwaka wa 2021. Sehemu ya kwanza ilifanyika katika Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii, mjini Vatican, na kufadhiliwa na Bayer AG, kwa udhamini wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha.
Kuhusiana na Jukwaa la Chakula Duniani 16-20 Oktoba 2023
Tukio kuu la Jukwaa la Chakula Duniani (WFF) linajumuisha Jukwaa la Vijana Ulimwenguni la WFF, Jukwaa la Sayansi na Ubunifu la FAO na Jukwaa la Uwekezaji wa Kuunga Mikono na FAO. Majuamuisho haya matatu yaliyounganishwa yanaleta pamoja suluhisho za kijasiri na zinazoweza kutekelezeka ili kuchochea mabadiliko ya mifumo yetu ya kilimo kulingana na changamoto na majanga ya sasa, zikimulika hasa umuhimu wa ushirikiano kati ya kizazi cha sasa na kijacho na ujanja wao wa pamoja katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi na uwekezaji katika maeneo muhimu ya kilimo na chakula. Kwa njia hiyo kwa mwaka 2023, tukio kuu la Jukwa hii la Chakula duniani WFF litafanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Oktoba 2023 katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Roma, Italia. Kwa juma zima, litahamasisha mijadala na makongamano miongoni mwa wadau husika, kuanzia barubari na vijana, wakulima, wazalishaji wadogo, watu wa Asili, watunga sera, wawekezaji wa kilimo na wanasayansi, kutoka pembe nne za dunia, wote wakiwa na lengo moja la kuhamisha kutoka ufinyu kama wa sindano ya uhakika wa chakula ili kufikia mustakabali bora wa chakula kwa wote, bila kumwacha mtu yeyote nyuma.