Tafuta

Tanzania imekuwa ni mwenyeji wa Mkutano wa pili wa kutokomeza Ukeketaji ambao umewashirikisha washiriki 900 kutoka Barani Afrika kuanzia Oktoba, 09 hadi 11, 2023 . Tanzania imekuwa ni mwenyeji wa Mkutano wa pili wa kutokomeza Ukeketaji ambao umewashirikisha washiriki 900 kutoka Barani Afrika kuanzia Oktoba, 09 hadi 11, 2023 . 

Mkakati wa Kupambana na Vitendo Vya Ukeketaji Barani Afrika

MMkutano pili wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala yakutomeza ukeketaji uliofanyika jijini Dar Es Salaam Oktoba 9-11, 2023. Mh. Riziki Pembe amesema mikakati madhubuti iliyowekwa katika maazimio ya mkutano huo yataleta mabadiliko kwa kizazi kijacho katika kupambana na Ukeketaji. "Jambo hili si tu linakiuka haki ya msingi ya wanawake na wasichana bali pia ni ukatili mkubwa ambao sote tunakubaliana kwamba haukubaliki" No Ukeketaji!

Na WMJJWM, - Dar es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe amesema hakuna sababu ya kuendelea kukiuka haki za binadamu na ukatili kwa wanawake na wasichana kutokana na mila zenye madhara. Mhe. Pembe ameyasema hayo wakati akihitimisha mkutano pili wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala yakutomeza ukeketaji uliofanyika jijini Dar Es Salaam Oktoba 9-11, 2023. Amesema mikakati madhubuti iliyowekwa katika maazimio ya mkutano huo yataleta mabadiliko kwa kizazi kijacho katika kupambana na Ukeketaji. "Jambo hili si tu linakiuka haki ya msingi ya wanawake na wasichana bali pia ni ukatili mkubwa ambao sote tunakubaliana kwamba haukubaliki" amesema Waziri Riziki Ameongeza kwamba, teknolojia itumike kuwakutanisha wadau wote na kubadilishana mawazo ya kutekeleza maazimio waliyojiwekea ili kutokomeza kabisa ukeketaji Barani Afrika na Duniani kwa ujumla. Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Toufiq akizungumza katika mkutano huo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinalindwa kwa kukubali Programu za kutokomeza ukeketaji zinasimamiwa. "Hapa Tanzania juhudi mbalimbali zimefanyika tangu mwaka 1990 hatimaye, Sheria ya kupinga ukeketaji ilitungwa mwaka 1998 na katika kuendeleza mapambano Serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukeketaji pamoja sheria ya mtoto.” Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo wamesema makubaliano yaliyopatikana kwa pamoja watayafikiasha katika Mamlaka za nchi zao ili hatua ziweze kuchukulua katika kupambana na kutokomeza vitendo vya ukeketaji Afrika.

Ukeketaji ni mila na desturi zilizopitwa na wakati
Ukeketaji ni mila na desturi zilizopitwa na wakati

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Tanzania imekuwa ni mwenyeji wa Mkutano wa pili wa kutokomeza Ukeketaji ambao umewashirikisha washiriki 900 kutoka Barani Afrika kuanzia Oktoba, 09 hadi 11, 2023 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere. “Kwa mwaka huu wa 2023, Tanzania tumepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kutokomeza Ukeketaji ambapo kama imekuwa na washiriki 200 kutoka mikoa yetu yote ya Tanzania na Nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika na Mabara mengine jumla ya washiriki ni 700” amesema Dkt. Gwajima. Waziri Dkt. Gwajima amefafanua kuwa Mkutano huo umeonogeshwa na Kaulimbiu isemayo “Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji” (Changes in a Generation) lengo kuu ni kutoa fursa kwa wadau wanaopambana na ukeketaji kuunganisha nguvu za pamoja, kubadilishana uzoefu, kujengeana uelewa na maarifa katika kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji katika nchi za Afrika.

Ukeketaji ni uvunjaji wa haki msingi za binadamu na ukatili mkubwa
Ukeketaji ni uvunjaji wa haki msingi za binadamu na ukatili mkubwa

Kwa mujibu wa Dkt. Gwajima amesema, wakati wa mkutano huo kumefanyika pia Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ambayo ufanyika Oktoba ya kila mwaka. Maadhimisho hayo ni ya 12 tangu kuanza kuadhimishwa ni utekelezaji wa Tamko la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Na. 66/170 la tarehe 19 Desemba, 2012. Lengo la siku hii ni kutathmini jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha upatikanaji wa Haki, Ulinzi, Ustawi na Maendeleo ya Mtoto wa Kike. Akifafanua kuhusiana na hali ya kitakwimu kwenye masuala ya Ukeketaji nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema kwa sasa ni takwimu zinaonesha kuwa  mkoa wa Manyara una asilimia 58, Dodoma asilimia  47, Arusha  asilimia 41, Mara asilimia 32, Singida asilimia 31 na Tanga Asilimia 14 hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanashirikiana katika kutoa elimu kwa jamii ili vitendo hivyo vitokomee nchini Tanzania Tanzania ilipata fursa ya kushiriki Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini Burkina Faso mwaka 2018 ambao ulishirikisha jumla ya nchi 22 wanachama wa Umoja wa Afrika. Mkutano huo uliazimia kwamba kila kanda katika Afrika ianzishe ushirikiano wa kupambana na mila na desturi ya ukeketaji sambamba na kudhibiti mipaka kuzuia mwingiliano wa mila hiyo kutoka nchi moja kwenda nyingine (Crossboader FGM) na mkutano kama ule unafanyika kila baada ya kipindi fulani katika nchi inayoteuliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

14 October 2023, 12:00