Tafuta

2023.10.19 Miller Puckette akiwa na  Tuzo ya Simba wa Shama 2023.10.19 Miller Puckette akiwa na Tuzo ya Simba wa Shama  

Miller Puckette aibuka na tuzo ya Simba wa shaba katika tamasha la III la Muziki,Venezia

Mtaalamu wa hisabati wa Marekani,mwandishi wa programu na mwanamuziki ni mhusika kweli kati ya wale wanaofanya kazi katika uwanja wa muziki wa kielektroniki,aliyepewa tuzo.Kwa upande wa Lucia Ronchetti,mkurugenzi wa kisanii wa Tamasha:Ni mgombea bora wa toleo la aina mpya za starehe za muziki wa kidijitali.

Na Marco Di Battista - Venezia.

Miller Puckette, mwanahisabati, mpangaji programu na mtunzi  wa muziki wa  mitindo mingi ya kidijitalii, mara baada ya kutunukiwa Simba wa Shaba katika toleo la 2023 la Tamasha la Muziki Mdogo huko Venezia, Italia na Lucia Ronchetti, mkurugenzi wa kisanii wa Toleo la III la Muziki alisema kuwa: "Niliweka mikono yangu kwenye kompyuta inayoweza kutoa sauti na hilo lilikuwa jambo la pekee mnamo mwaka  1979, nilipoanza. Uwezekano wa kutengeneza vitu nilivyokuwa nikifikiria kwa miaka mingi, nikisikia ghafla, ulikuwa kama mlango unaofunguliwa.  Ilichochea maisha yangu yote. Sikuweza kufanya kitu kingine chochote.”

Historia iliyofunikwa kwa urahisi

Urahisi wa maneno hayo (na mengine yaliyotamkwa na Puckette wakati wa afla ya tuzo) na unyenyekevu uliosindikizwa nao unaweza kutufanya tusahau kwamba Waamerika ni aina ya historia  katika eneo la muziki wa kielektroniki duniani kote. Ni yeye aliyebuni na kutengeneza programu mbili: ‘Max/Msp’ na ‘Pure Data’, ambazo zilibadilisha ulimwengu wa kidijitali. Kutoka katika kompyuta kubwa na vituo vya data au takwimu tumehamia Kompyuta za kawaida  au tuseme Mac -zinazoweza kufikiwa na kila mtu. Kutoka katika kazi ya mtu binafsi tumehamia kwenye ushirikishwaji wa nyenzo, hadi kufikia mwingiliano wa mtandaoni kati ya watu wanaoishi katika ncha tofauti  duniani.

Puckette: ni sura muhimu katika nyanja kadhaa

Afla ya kupewa tuzo ilikuwa na sifa ya kupongezwa kwa kupigiwa makofi, hivyo ilikuwa muhimu sura yake katika nyanja mbalimbali, ambapo umuhimu huo uliooneshwa na ushuhuda wa tuzo nyingi alizopokea. Kama mwanahisabati, tuzo ya kwanza katika Shindano la Hisabati la William Lowell Putnam; katika uwanja wa muziki, kwa kutaja tuzo chache tu, Ubunifu wa Programu wa Mwaka wa 1990, Tuzo la Mafanikio ya Maisha ya Seamus mnamo 2008 pamoja na digrii nyingi za heshima na udaktari lazima zijulikane. Kwa sasa yeye ni profesa anayeibuka katika idara ya muziki ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu  Diego huko California nchini Marekani. Kama mwalimu alifunza vizazi vingi vya watunzi, wasanii, waandaaji programu na watafiti. Wale ambao wamefanya kazi naye wanatambua wazi nia yake wazi na shauku ya kufanya kazi pamoja. Sehemu ya umaarufu wake ni kutokana na ukweli kwamba aliunda toleo huria la programu yake ya Max MSP, ambayo ilikuwa imeidhinishwa na Ircam huko Paris. Programu mpya, inayoitwa Pure Data, na hii inaendelea kupatikana bila malipo kwa kila mtu.

"Muziki Mdogo" kwenye Tamasha la Muziki wa Kisasa

Tunaelekea katika  hafla rasmi ya kukabidhi tuzo ya Simba ya Dhahabu kwa Mafanikio ya Maisha (na tamasha ambalo tayari limeuzwa) ambalo mwaka huu litakwenda kwa Brian Eno, tukumbuke kwamba jina la toleo hili la 67 la Tamasha la Kimataifa la Muziki wa Kisasa ni la  Muziki Midogo. Kulingana na mkurugenzi wa kisanii, lengo ni kuamsha muziki unaozalishwa kupitia kipaza sauti "capture" na wakati huo huo kuchunguza asili ya (microscopic) hadubini ya sauti. "Nimechagua jina hili kwa usahihi kwa sababu ya utata wa neno hili 'Micro', kwa sababu kwa upande mmoja tunataka kuchukua umma katika safari ndani ya sauti na kwa hiyo kuchunguza (microscopy) kwa hadubini ya sauti na kwa upande mwingine tunataka kutumia  ala ya ajabu ambayo ni Kipaza sauti (maikrofoni) kana kwamba ni darubini inayotuwezesha kuona na kusikiliza kitu katika sauti ambayo hatujawahi kuisikiliza kabisa", alisema Lucia Ronchetti na akiongeza kuwa "micro” udogo  hu unataka kuonesha ukubwa wa hadubini na maikrofoni yenyewe kama chombo cha msingi kwa kipindi hiki cha miaka miwili ambacho kimejitolea kwa sauti ya kielektroniki na sauti ya dijitali, lakini pia kwa sauti ya ala iliyoinuliwa katika nafasi ya  sauti kubwa (acustico -akustika).

Kuhusu Tamasha la 67 la Kimataifa la Muziki Mdogo

Tamasha la 67 la Kimataifa la Muziki Mdogo wa Kisasa limejitolea kwa sauti za kidijitali, utayarishaji wake na usambazaji wake katika anga ya akustika, kupitia teknolojia ya hali ya juu na utafiti wa majaribio. Tamasha linawasilisha mielekeo mingi ya kimtindo na utafiti wa kibunifu wa ubunifu kutoka eneo la kimataifa la muziki, kulingana na usakinishaji, utendakazi na mtindo wa mtandaoni, na maonesho mengi ya kwanza ya ulimwengu yalioneshwa katika Tamasha la Tatu la  na Muziki  na utayarishaji shirikishi na sherehe muhimu zaidi za kimataifa.

Muziki Mdogo una lengo la kutaka kuinua muziki unaozalishwa kupitia uchukuaji wa Vipaza sauti (maikrofoni) na kuchunguza asili ya sauti ndogo sana. Kwa hiyo hili ni tamasha ambalo linalenga kuimarisha uzuri na utata wa sauti ya kidijitali na upeo mpya wa utunzi. Alama maalum ya akustika ya kila mandhari na kitendo cha kusikiliza kama usomaji wa nafasi inayozunguka, kupitia sauti zilizotamkwa na kubadilisha ambazo mazingira  yake huturudishia, hujitokeza katika ubunifu wa kielektroniki wa sehemu tofauti za tamasha, inayolenga kutafuta, sauti katika muktadha wa usanifu wa majengo ya Venezia.  Wasanii walioalikwa, na kufika kutoka ulimwenguni kote, watengenezaji wa mtindi wa  sauti, waundaji wa sauti za akustisk, waakiolojia wa sauti zilizopotea na watafiti wa asili isiyoweza kuelezeka, ya muda mfupi, na sauti za ajabu wanashangaza na kuhusisha umma kwa sauti kubwa na isiyo ya kawaida na ambayo ni uhai wa  muziki.

20 October 2023, 14:07