Tafuta

Ukanda wa Gaza watu wengi wamekufa kufuatia na uperesheni kubwa dhidi ya magaidi. Ukanda wa Gaza watu wengi wamekufa kufuatia na uperesheni kubwa dhidi ya magaidi.  (AFP or licensors)

Israeli yatangaza kuzingira kamili kwa Gaza,watu 800 waliouawa

Baada ya operesheni ya usiku wa Jumamosi,wanajeshi wa Israeli walibomoa karibu malengo 500 ya Ukanda wa Gaza,ambapo waliendelea na mashambulizi mapana katika vituo mbali mbali vya mkakati wa Hamas,huku makombora yakiendelea kurushwa kutoka Gaza kuelekea eneo la Israeli.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Waziri wa Ulinzi wa Israeli aliamuru kutengwa kwa Ukanda huo baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Jumamosi 7 Oktoba 2023  iliyopita. Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi alisema  Hakuna umeme, wala maji wala Gas. Hakuna chakula na wala petrol. Kila kitu kimesimamishwa. Tunapigana kama wanyama binadamu na athari zitakuwa juu yetu.

Malengo 500 yalipigwa wakati wa usiku

Baada ya operesheni ya usiku ule wa Jumamosi 7 Oktoba 2023, wanajeshi wa Israeli walibomoa karibu malengo 500 ya Ukanda wa Gaza, ambapo waliendelea na mashambulizi mapana katika vituo mbali mbali vya mkakati wa Hamas, huku makombora yakiendelea kurushwa kutoka Gaza kuelekea eneo la Israeli, na wakati huo huo zaidi ya laki moja wakihama makazi yao ambapo ni mamia ya wahanga wa raia kati ya pande hizo mbili. Askari wa akiba elfu 300 walifikiwa katika masaa 48  baada ya kuanza operesheni hiyo.

Mamia ya raia walikufa

Kati ya idadi ya watu milioni 2.3, elfu 123 walikimbia makazi yao, kulingana na ofisi ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Takriban watu 550 wamekufa na 2300 kujeruhiwa Wakati huohuo, idadi ya wahanga wa Israel waliouawa na Hamas siku ya Jumamosi ilipanda hadi 800, wakiwemo vijana 260 waliokuwa wamekusanyika kwa tafrija ya rave, 750 walipotea, 130 waliwekwa mateka. Ving'ora vya kengele pia vilisikika kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mpaka na Lebanon, huku serikali ya Beirut ikidai kuwa ina hakikisho kwamba Hezbollah haitaingilia kati.

09 October 2023, 15:46