Tafuta

Kimbunga kikali nchini Libia kimesababisha vifo vya watu 2000, na zaidi ya elfu moja kutoweka. Kimbunga kikali nchini Libia kimesababisha vifo vya watu 2000, na zaidi ya elfu moja kutoweka. 

Libya:Zaidi ya watu 2000 wamekufa na mamia elfu kupotea

Takriban watu 2,000 wamekufa na maelfu kupotea baada ya mabwawa mawili ya maji kuporomoka kwa wakati mmoja huko Derna kutokana na Kimbunga Daniel.Na wakati huo huo Waziri Mkuu wa Cyrenaica ametoa taarifa za kuomba msaada.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa siku mbili zilizopita, Kimbunga kiitwacho  Daniel kimepiga mashariki mwa Libya. Hakuna mtu aliyekuwa anatarajia pepo na mvua kuzidi kiasi hicho. Kitovu cha maafa hayo ni eneo la Derna, mji wenye wakazi laki moja unaotazamana na bahari ya Mediterania, ambao sasa umezama na mita tatu za maji. Kimbunga kikali  Daniel kilisababisha kuporomoka kwa mabwawa yaliyojengwa kando ya Mto Wadi unaotiririka kutoka kwenye milima ya karibu hadi mjini. Mita za ujazo milioni 33 za maji zilimwagika ghafla kwenye maji na kusababisha mafuriko yasiyokuwa ya kawaida na kuzamisha mitaa na majengo yaliyo karibu. Kwa njia hiyo vitongoji na mitaa vyote vimetoweka. Hata magofu ya Kurene ya kale yanaonekana kuzama. Hadi sasa lakini haiwezekani, hata hivyo, kufanya tathmini kamili ya maafa, kutokana na ugumu wa kufikia eneo linalozozaniwa kati ya tawala mbili zinazopingana na zinazoshikiliwa na wanamgambo mbalimbali wenye silaha.

Kimbgunga kikali Daniel kimesababisha maporomoko ya mabwawa mawili ambayo yamesababisha vifo vya watu huko Libia
Kimbgunga kikali Daniel kimesababisha maporomoko ya mabwawa mawili ambayo yamesababisha vifo vya watu huko Libia

Shirika la Hilali Nyekundu lilisalia kuwa waangalifu na lilizungumza juu ya mamia ya vifo. Kulingana na waziri mkuu wa serikali inayojiita ya mashariki mwa Libya, Osama Hamad anabainisha kuwa karibu watu elfu mbili watakuwa wamekufa huku zaidi ya watu elfu moja wakikosekana. Manispaa, kupitia kwa diwani Ahmed Amdur, iliomba uingiliaji wa haraka wa kimataifa kuwaokoa pamoja na kufunguliwa kwa ukanda wa baharini kusaidia wakazi. Wakati huo huo, Bunge la Mashariki limetangaza sikukuu mbili za umma, isipokuwa katika sekta muhimu.

Kimbunga kimeacha maafa makubwa sana nchini Libya
Kimbunga kimeacha maafa makubwa sana nchini Libya

Serikali ya Abdulhamid al-Dbeibah, yenye makao yake mjini Tripoli, ilijibu kwa kutangaza siku tatu za maombolezo na kuahidi kuwafidia wale wote walioathiriwa na mafuriko. Tripoli pia ilitangaza kutumwa kwa ambulensi 50 na madaktari 75 huko Derna na msafara wa kuimarisha kliniki za vijijini. Mkuu wa Kampuni ya Ya Huruma Kuu ya Tripoli, Mohamed Ismail, alituma makumi ya wachimba madini kusaidia shughuli za uokoaji.

Watu 2000 wamekufa huko Libya kutokana na maporomoko ya mabwa mawili huko Libya
Watu 2000 wamekufa huko Libya kutokana na maporomoko ya mabwa mawili huko Libya

Kusonga kwenye ardhi na kufika unakokwenda, hata hivyo, si rahisi. Dbeibah ina, kwa faida yake, kutambuliwa kwa Benki Kuu ya Libya, ambayo fedha za tawala za mitaa zinatoka. Umoja wa Mataifa umehakikisha uungaji mkono wake kwa Cyrenaica kwa magoti yake kupitia ujumbe wa ndani wa UNSMIL. Wakati wa kwanza kuhamasishwa kutoka nje walikuwa Tunisia, Misri, Algeria na Qatar. Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Antonio Tajani, alisema alikuwa katika mawasiliano ya karibu na mamlaka ya Libya kutathmini aina ya msaada wa kutuma mara moja na alisisitiza kwamba hakuna Waitaliano waliohusika. Kulingana na wataalamu, dhoruba Daniel ni tukio kubwa kutokana na kiasi cha maji kilichoanguka.

Kimbunga na maporomoko nchni Libya yaua makumi elfu ya watu
11 September 2023, 18:34