Tafuta

Mkutano Mkuu wa 43 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika tarehe 17 Agosti. Mkutano Mkuu wa 43 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika tarehe 17 Agosti.  (AFP or licensors)

Mkutano Mkuu wa 43 wa SADC unafanyika Agosti 17

Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanafanya Mkutano Mkuu wa 43 Alhamisi 17 Agosti 2023.Kabla ya kilele Baraza la mawaziri lilifanyika mjini Luanda,Jamhuri ya Angola tarehe 13-14 Agosti 2023 ili kujadiliana kuhusu utekelezaji wa masuala ya mtangamano wa kikanda.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baraza la wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) linashughulikia ajenda ya ushirikiano wa kikanda. Kabla ya kilele cha Mkutano Mkuu wa 43 wa Wakuu wa Nchi Kusini mwa Afrika (SADC), ulifanyika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya maadalizi mjini Luanda, katika Jamhuri ya Angola tarehe 13-14 Agosti 2023 ili kujadiliana kuhusu utekelezaji wa masuala ya mtangamano wa kikanda, ambao ndio kiini hasa cha kilele cha Mkutano huo  ambao unafanyika Alhamisi tarehe 17 Agosti 2023. Katika hotuba yake ya kuwakaribisha, mawaziri wa Nchi wanachama, Mheshimiwa Balozi Téte António alisema kuwa, chini ya urais wa Angola, kanda taweka maanani na kuzingatia mtaji wa watu na kifedha kama kichocheo cha ukuaji wa viwanda. Hizi ni rasilimali watu wa kutosha katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi na mapinduzi ya nne ya viwanda, pamoja na rasilimali fedha za kutosha ili kuhakikisha mifumo endelevu zaidi ya ufadhili. Rais wa Baraza hilo pia alisisitiza kuwa kanda ya SADC imetekeleza shughuli zinazolenga kuboresha utekelezaji wa programu za uanzishaji viwanda na utangamano wa soko. Rais alitoa wito kwa Kanda kutafuta njia za kuwawezesha vijana wote kufungua uwezo wao na kutengeneza njia za mafanikio yao.

Rais Lazarus Cakweta ni mmoja wa wanachama wa SADC
Rais Lazarus Cakweta ni mmoja wa wanachama wa SADC

Naye Katibu Mtendaji wa SADC Elias Mpedi Magosi, akisisitiza hatua iliyofikiwa na Kanda hiyo  katika kufikia matokeo ya mkakati  RISDP 2020-2030, alisisitiza moyo wa mshikamano wa nchi wanachama katika kujenga amani na utulivu katika eneo hilo. Bwana  Magosi alisema kuwa kanda hiyo imeidhinisha kutumwa kwa tume ya SADC katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC) kama jibu la kikanda dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa DRC. Baraza la la Wakuu wa Nchi Kusini mwa Afrika liliona muda wa kimya katika mshikamano na ukumbusho na kutoa rambirambi kwa serikali na familia za wanajeshi waliopoteza maisha wakati wakihudumu katika SAMIM, pamoja na kupongeza azimio, upekee, na kukamilishana kwa juhudi za pamoja kupambana na tishio la ugaidi na itikadi kali kali katika Mkoa wa Cabo Delgado.

Mkutano wa  Barazala la Mawaziri linasimamia utendakazi na maendeleo ya SADC na kuhakikisha kuwa sera za shirika hilo zinatekelezwa ipasavyo. Baraza hilo lina Mawaziri kutoka kila Nchi Mwanachama, kwa kawaida kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Mipango ya Kiuchumi au Fedha. Kwa kawaida Mkutano huo hutanguliwa na mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Viongozi Wakuu ya SADC, ambayo ni kamati ya ushauri wa kiufundi wa Baraza la Mawaziri.

17 August 2023, 09:08