Tafuta

Hawa ni waandamanaji nchini Niger wanaounga mkono Jeshi la kimapindizi huko Niamey. Hawa ni waandamanaji nchini Niger wanaounga mkono Jeshi la kimapindizi huko Niamey.  (AFP or licensors)

Maaskofu wa Niger:Kila kinachowezekana kifanyike ili kuepusha 'Libya ya pili'

Uwezekano wa kuingilia kati katika nchi ya jirani Niger kumezusha hofu na upinzani nchini Nigeria,huku Baraza la Seneti la shirikisho halijidhihirisha kwa upande wake,na katika majimbo 7 ya kaskazini mwa Nigeria yanayopakana na Niger sauti dhidi ya suluhisho la kijeshi zimesikika zaidi.Maaskofu wa Niger,Burkina Fasi na Nigeria wako kinyume na kuingilia kijeshi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tunaelekea kurefusha muda uliopendekezwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kwa njama ya mapinduzi ya kijeshi ili kumwachilia Rais Mohamed Bazoum, na kurejesha mamlaka kwa serikali halali ya kiraia. Kauli hiyo ilisikika Dominika tarehe 6 Agosti 2023, ambayo ilitishia kuingilia kijeshi kwa baadhi ya mataifa yanayofuata ECOWAS yanayoongozwa na Nigeria, ambayo Mkuu wa Nchi, Bola Ahmed Tinubu, ndiye Rais wa sasa wa Jumuiya hiyo. Hata hivyo, uwezekano wa kuingilia kati katika nchi hiyo jirani kumezusha hofu na upinzani nchini Nigeria yenyewe, huku Baraza la Seneti la shirikisho halijidhihirisha kwa upande wake, wakati katika majimbo 7 ya kaskazini mwa Nigeria yanayopakana na Niger sauti dhidi ya suluhisho la kijeshi zimejifanya kusikika Nguvu zaidi.

Baraza Katoliki la Maaskofu wa Nigeria limeelezea upinzani wake kwa kauli ya Rais wake, Askofu Mkuu Lucius Iwejuru Ugorji, Askofu Mkuu wa Owerri. “Tunamwomba Rais Bola Ahmed Tinubu awazuie Wakuu wa Nchi za ECOWAS kutokana na kishawishi cha kuingia vitani dhidi ya waliopanga mapinduzi,” alisema  Askofu Mkuu Ugorji, kuwa “Tunawaomba wazuie umwagaji damu unaokuja ambao utafuatia uingiliaji wa kijeshi. Tumepoteza maisha mengi barani Afrika. Pia tumepoteza maisha ya thamani nchini Nigeria na hatuwezi kuendelea kwa njia hii ya kutisha, kwa sababu yoyote ile.”

“Wakati tunasema hapana kwa mapinduzi, pia tunasema hapana kwa vita, kwa sababu yoyote,” alisisitiza  Askofu Mkuu Ugorji. “ Rais Tinubu tafadhali asianzishe msafara wowote wa kijeshi nchini Niger. Tusisahau kwamba wakati wa msafara wa ECOMOG (utume ulioongozwa na jeshi la Nigeria huko Liberia na Sierra Leone), Nigeria sio tu ilichukua jukumu muhimu, lakini pia ilibeba mzigo mkubwa wa hasara katika rasilimali watu na nyenzo alisisitiza. “Wakuu wa nchi za ECOWAS tafadhali wafikirie juu ya nini hatma ya shirika inapaswa kuwa, kama wataanzisha uingiliaji wa kijeshi nchini Niger,” analiongeza kusema Askofu Mkuu Ugorji, “Vita havitasuluhishi mizozo. Ni afadhali kuwa na mazungumzo kuliko kuingia katika vita vikubwa, ambavyo hakuna anayeweza kusema ni lini hasa vitaisha,” anahitimisha.

Baraza la Maaskofu la Burkina Faso-Niger pia linatangaza upinzani wake kwa kuingilia kijeshi. Hatuamini hata kidogo katika utatuzi wa nguvu, ambao tunasema hapana, wanasema katika ujumbe uliochapishwa tarehe 4 Agosti, uliotiwa saini na Rais wake, Askofu Laurent Dabiré, wa Jimbo katoliki la  Dori, kaskazini-mashariki mwa Burkina Faso. “Kiukweli, hatuwezi kutokuwa na wasiwasi wakati mzuka wa vita unaonekana katika suluhisho zilizopendekezwa ili kujiondoa kwenye mzozo, na kumfanya mtu kufikiria juu ya ‘Libya ya pili’, hata kama matokeo mabaya na mabaya  zaidi ya kudhoofisha utulivu wa nchi hizi kuendelea kuifanya nchi kuteseka vibaya sana kwa watu wa Sahel,” walihitimisha. Waraka wao.

Maaskofu wa Niger, Burkina Faso na Nigeria kupinga jeshi
09 August 2023, 14:33