Tafuta

Picha za ndege zisizo na rubani zinaonesha moshi mzito ukitokana na  moto karibu na mji mkuu Khartoum Picha za ndege zisizo na rubani zinaonesha moshi mzito ukitokana na moto karibu na mji mkuu Khartoum 

Watu nchini Sudan wataabika kwa njaa kutokana na vita

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilisema hivi karibuni kwamba watu wengine milioni mbili wamekuwa wakimbizi wa ndani na takriban 600,000 wamekimbia nje ya mipaka ya Sudan.Wakati huo huo mgogoro wa chakula na afya ni mbaya katika muktadha wa mzozo mkali wa wenyewe kwa wenyewe ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa.

Angella Rwezaula – Vatican.  

Takriban watu 2,800 wameuawa nchini Sudan tangu mapigano yalipoanza katika mji mkuu Khartoum Aprili 15, kulingana na takwimu mpya za mashirika yanayofuatilia vita hivyo. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilisema hivi karibuni  kwamba watu wengine milioni mbili wamekuwa wakimbizi wa ndani na takriban 600,000 wamekimbia nje ya mipaka ya Sudan. Na mgogoro wa chakula na afya ni mbaya katika muktadha wa mzozo mkali wa wenyewe kwa wenyewe ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa. Hayo yameripotiwa pia  na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF)ambalo linaendesha shughuli zake nchini humo na nchi nyingine ulimwenguni pia na zaidi ya yote kushughulikia kesi za washukiwa wa surua katika muktadha huo wa mirundikano ya watu.

Mahangaiko ya watu wasio na hatia nchini Sudan:Zigambano fahari wawili ziumiazo ni nyasi
Mahangaiko ya watu wasio na hatia nchini Sudan:Zigambano fahari wawili ziumiazo ni nyasi

Katika muktadha huo zaidi ya yote ni wanawake na watoto wanaukimbia mji mkuu wa Sudan Khartoum, kutafuta wokovu kutokana na mzozo wa umwagaji damu ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa kati ya Jeshi na vikosi vya msaada vya haraka vya kijeshi. Kulingana na takwimu  kutoka kwa Madaktari Wasio na Mipaka, zaidi ya watu 140,000 wametafuta hifadhi katika Jimbo la White Nile, katika hali ngumu ya kutisha ya kibinadamu: uhaba mkubwa sana wa chakula, maji, malazi, huduma za afya, katika kambi kumi ambazo, kulingana na mamlaka mahalia, hupokea watu wapatao 387,000 na ambapo, kulingana na shirika linalosimamia kliniki kadhaa katika eneo hilo, visa vipya vya washukiwa wa surua vinaripotiwa ambao tayari unasababisha wahasiriwa wa kwanza.

Wakimbizi wengi wanatafuta mahli pa kukimbilia nchini Sudan
Wakimbizi wengi wanatafuta mahli pa kukimbilia nchini Sudan

Mbele hayo ambapo tunaweza kusema ni moja ya ncha tu ya hali halisi  ambayo inawaona wakimbizi wa ndani karibu milioni 2 na nusu na wapatao 700,000 ambao wamevuka mipaka ya Sudan. Matokeo ya mzozo huo yamelaaniwa na Umoja wa Ulaya, baada ya siku 100 za mapigano. Huko katika Baraza la Ulaya jijini Brussels wametangaza kuwa iko tayari kupitisha vikwazo ili kukomesha vita vya ndani. Katika taarifa yake, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa Sera za Kigeni, Borrell, alisisitiza kushangazwa na  ukatili na dharau kamili ya wapiganaji dhidi ya raia na kwamba zaidi ya waathirika 1,100, pamoja na watoto 435, na wengine 12,000 wajeruhiwa. Hali ambayo inaweza kusababisha Umoja wa Ulaya (EU) kuwawekea vikwazo wale wanaohusika na mzozo, ili kujenga msingi wa kukuza amani.

Madaktari Bila Mpaka wanajikita katika nyanja ya kusaidia wagonjwa na kila shida ya watu
Madaktari Bila Mpaka wanajikita katika nyanja ya kusaidia wagonjwa na kila shida ya watu

Ikumbukwe Shirika la 'Médecins Sans Frontières', linalojulikana zaidi kama la 'Madaktari Wasio na Mipaka' au kwa kifupi MSF, ni Shirika lisilo la kiserikali,  la kibinadamu linalolenga kutoa misaada ya kimatibabu na usaidizi kwa watu katika maeneo yote duniani ambapo haki ya matibabu haijahakikishwa. Shirika hilo MSF lilianzishwa mjini mjini Paris,  Ufaransa mnamo mwaka 1971 na kundi la madaktari na waandishi wa habari na lina makao yake makuu mjini Geneva, Uswizi. Kwa kazi yake alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1999. Kwa njia hiyo MSF inafanya kazi katika nchi 75 yenye nguvu kazi ya zaidi ya wafanyakazi 68,000 na watu wa kujitolea (kwa takwimu za  2022). Wafadhili wa kibinafsi hutoa 97% ya ufadhili wa shirika hili, huku michango ya mashirika ikitoa iliyobaki, na kuipatia  MSF bajeti ya kila mwaka ya takriban dola bilioni 1.9. MSF inaundwa na vituo vitano vikubwa vya uendeshaji nchini Ubelgiji, Ufaransa, Uswizi, Uholanzi na Hispania, vyama vitatu vya kikanda na sehemu 21 za washirika zinazoshiriki katika harakati na usimamizi wa moja kwa moja wa baadhi ya miradi au na shughuli za uchangishaji fedha, kuajiri wahudumu wa kibinadamu, wafanyakazi kwa ajili ya  taarifa na ufahamu wa maoni ya umma.

28 July 2023, 15:14