Tafuta

Katika Kanda ya Ulaya ya shirika la WHO,linabainisha kuwa kufa maji kunapoteza Maisha ya takriban watu 20,000 kila mwaka.  Katika Kanda ya Ulaya ya shirika la WHO,linabainisha kuwa kufa maji kunapoteza Maisha ya takriban watu 20,000 kila mwaka.   (ANSA)

Watu 236,000 hupoteza maisha kila mwaka duniani kwa kuzama barani Ulaya

Katika fursa ya kuelekea kilele cha Siku ya Kuzuia Watu Kuzama duniani,” ambayo hufanyika kila tarehe 25 Julai ya kila mwaka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) kanda ya Ulaya, ilisem Julai 24 Julai kuwa takriban watu 236,000 hupoteza maisha kila mwaka duniani kote kwa kuzama huku 20,000 kati yao ni barani Ulaya vifo ambavyo vinaweza kuzuilika.

Habari za Umoja wa Mataifa

Katika taarifa yake iliyotolewa tarehe 24 Julai 2023 mjini Copenhagen, Mkurugenzi wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa duniani(WHO ), Kanda ya ulaya, Dk. Hans Henri P. Kluge alisema: “Wengi wetu mara chache, kama itawahi kutokea, hufikiri juu ya kuzama kama hatari ya afya ya umma yenye athari kubwa. Lakini hivi karibuni kupinduka kwa meli ya Adriana kwenye maji kati ya Ugiriki na Italia, meli ndogo ya wavuvi iliyojaa mamia ya watu wanaotafuta maisha mapya Ulaya, kumebadilisha hilo. Katika janga hilo moja zaidi ya watu 600 waliokuwemo katika hali ya kukata tamaa walizama pamoja na maiti nyingi hazitapatikana tena.” Alisema hayo katika fursa ya kuelekea kilele cha Siku ya Kuzuia Watu Kuzama duniani, ifanyikayo kila tarehe 25 Julia yak ila mwaka.

Watu wanapoteza maisha katika bahari wakiwa wanavuka
Watu wanapoteza maisha katika bahari wakiwa wanavuka

Kwa kuongezea alisema “lakini ni kawaida zaidi, wanaume, wanawake na watoto kuzama kimya kimya na peke yao katika hali nyingi. Na sababu zinazochangia kuzama, kwa mujibu wa WHO, kuruka bila usimamizi ndani ya mabwawa ya kuogelea ya nyuma ya nyumba yasiyo na uzio, kwa mfano huchangia vifo vya kuzama, au kubebwa na mkondo wa maji ufukweni ambapo kuogelea pekee hauwezi kuwakomboa watu katika hilo.  Pia shirika hilo limesema kuteleza kwemye meli au michezo ya kwenye maji bila kuvaa majaketi ya kuokoa maisha na kuanguka ndani ya maji wakati wanatembea nyumbani peke yao ni baadhi tu ya sababu lakini kuna sababu nyingi zinazochangia watu kupoteza Maisha kwa kuzama.

Shab la maua kuwakumbuka waliokufa baharini
Shab la maua kuwakumbuka waliokufa baharini

Siku ya Kuzuia watu kuzama ambayo ni 25 Julai ilipitishwa na Baraza Kuu la umoja wa Mataifa kwa mtazamo mmoja tu wa kuzuia kabisa watu kuzama ili vifo visitokee. Takwimu za vifo vitokanavyo na kuzama Ulimwenguni kote, sgirika la WHO linakadiria kuwa angalau watu 236,000 hupoteza maisha yao kutokana na kuzama kila mwaka.  Kwa upande wa Kluge alisema “Ninasema angalau kwani nambari hizi zinawakilisha kuzama bila kukusudia. Kulingana na hali ya uainishaji, matukio ya kuzama yanayohusiana na usafiri wa maji, maafa ya mazingira, kujidhuru au mashambulizi hayajajumuishwa hapa. Hii kwa kweli inapunguza idadi kamili ya mzigo wa kimataifa wa kuzama kwa kati ya asilimia 30-50.”

Kinachobaki ni kuweka ishara ya Msalaba kwa wale ambao hawapatikani hata kwenye fukwe baada ya kuzama baharini
Kinachobaki ni kuweka ishara ya Msalaba kwa wale ambao hawapatikani hata kwenye fukwe baada ya kuzama baharini

Katika Kanda ya Ulaya ya shirika la WHO, linabainisha kuwa kufa maji kunapoteza Maisha ya takriban watu 20,000 kila mwaka.  “Hii inaweza kuonekana kama sehemu ndogo ya idadi yote ya ulimwengu, lakini bado ni sababu ya pili ya vifo kwa watoto wa kati ya miaka 5-14.” Kwa kuongezea alisema kuwa kuzama pia ni suala muhimu la usawa, kukiwa na tofauti ya mara 20 ya viwango vya vifo katika nchi 53 za Kanda ya Ulaya huku nchi za mashariki kwa ujumla zikiwa na viwango vya juu zaidi. Takwimu sahihi ni muhimu katika kuelewa upeo wa changamoto na mambo mengi yanayohusika alisisitiza. Kwa mfano, kwa kuzingatia mzigo wa kweli wa vifo vya kuzama nchini Uingereza ambako visababishi vyote vya kuzama majini vimehesabiwa, kwa hakika ni asilimia 165 zaidi kuliko wigo mdogo uliokadiriwa na WHO, pamoja na vifo vya kuzama kwa sababu ya kujidhuru kwa makusudi kwa wasiwasi fulani na kuongezeka kwa kipaumbele cha kitaifa kama janga linalopaswa kushughulikiwa.

Mwezi Machi mamia ya watu walikufa kabla ya kufika fukwe za Cutro huko Calabria Italia.
Mwezi Machi mamia ya watu walikufa kabla ya kufika fukwe za Cutro huko Calabria Italia.

Tofauti miongoni mwa nchi hata hivyo ongezeko la kuzama majini katika Kanda ya Ulaya WHO inasisitia  pia kuwa ni tofauti sana na ulimwengu wote. “Vifo vya kuzama kwa wanaume wenye umri wa miaka 30-49 ni kubwa zaidi kati ya kanda zote sita za WHO. Hii inaonesha ukweli kwamba kuzama kunahusishwa zaidi na burudani ya maji badala ya kuishi.” Kisha, vifo vinavyoripotiwa vikiwa juu tu ya ncha ya barafu, kuzama pia husababisha wigo mpana wa majeraha yasiyoweza kusababisha kifo na athari kubwa za kiafya, kuanzia kuharibika kwa mfumo wa upumuaji kwa sababu ya kuvuta pumzi ya maji hadi majeraha ya ubongo na athari za muda mrefu maishani. “Ulaya pia ina unywaji wa pombe wa juu zaidi ya kila mtu wa Kanda yoyote ya Shirika la Afya duniani (WHO). Hii inawakilisha sababu kuu ya hatari kwa aina zote za vurugu na majeraha. Pombe inahusishwa na asilimia 26 ya vifo vyote vya kuzama katika Kanda ya Ulaya, kuanzia asilimia 3 hadi zaidi ya asilimia 55 katika nchi za Kanda hiyo.”

Vimitumbwi vyenyewe ni vya kiajabu ambavyo watu hawafikirii madhara na hatari
Vimitumbwi vyenyewe ni vya kiajabu ambavyo watu hawafikirii madhara na hatari

Isitoshe, shirika hilo la afya linasema kuwa wana  changamoto ya uhamiaji na viungo vyake vya kuzama, kama janga la hivi karibuni la Mediterania lilivyodhihirisha. Kwa mujibu wa mradi wa watu waliopotea wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji (IOM) takriban watu 34,000 wamezama katika kipindi cha uhamiaji tangu rekodi zilipoanza kukusanywa mwaka wa 2014. Hii inawakilisha asilimia 60 ya vifo vyote vinavyohusishwa na uhamiaji vilivyorekodiwa, na kati ya hivi, karibu wanne kati ya watano sawa na asilimia 76  vimetokea katika Kanda ya Ulaya  English Channel na Mediterania. Kuna dalili kuwa suala la kuzama majini linawekwa zaidi kwenye ajenda za afya na usalama. Mwezi Mei 2023, Baraza la afya Ulimwenguni, lilipitisha azimio la kihistoria juu ya kuzuia kuzama, lililosimamiwa na nchi 72 zikiwemo 42 kati ya nchi 53 za Kanda ya Ulaya.

25 July 2023, 14:53