Tafuta

Ulifanyika mkutano wa kimataifa kuhusu maendeleo na uhamiaji. Ulifanyika mkutano wa kimataifa kuhusu maendeleo na uhamiaji.  (ANSA)

Viongozi wa Nchi 21 wakutana Roma katika ishara ya mpango wa Mattei

Umefanyika mkutano jijini Roma Julai 26 chini ya ishara ya Mpango wa Mattei,uliowaona viongozi wa nchi 21 zinazopakana na bahari.Ni muktadha wa,(wahamiaji na wakimbizi)lakini pia wawakilishi wa wafalme wa Ghuba pamoja na Umoja wa Afrika,viongozi wa Ulaya na taasisi za fedha za kimataifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Viongozi wa nchi zinatoka na kuwasili,(wahamiaji na wakimbizi), lakini pia wawakilishi wa wafalme wa Ghuba pamoja na Umoja wa Afrika, viongozi wa Ulaya na taasisi za fedha za kimataifa wamekutana jijini Roma tarehe 26 Julai 2023 katika  ishara ya 'Mpango wa Mattei' na hivyo “Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo na Uhamiaji”, tukio lililoandaliwa na serikali ya Italia katika jengo la Farnesina ambao ulilenga kuzindua mchakato wa kimataifa wa kutekeleza hatua madhubuti za ukuaji na maendeleo ya Bahari ya Mediterania na Afrika iliyopanuliwa. Kiukweli ni hatua ya kwanza kuelekea ufafanuzi wa Mpango wa Mattei ambao Italia itaonesha mnamo Novemba 2023 wakati wa Mkutano wa Italia na Afrika. Ni taarifa kutoka vyanzo vya kidiplomasia. Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Italia, Bi Giorgia Meloni alikutana na rais wa Tunisia, Kaïs Saïed.

Katika  vyanzo vya habari kutoka Jumba la Chigi, Roma walibainisha kuwa Bi Giorgia Meloni alionesha malengo ya Mkutano huo kwa rais wa Tunisia na Rais Saïed alielezea shukrani zake. “Huu ni mwanzo wa safari. Tunisia na Italia zina mustakabali wa pamoja”, alijibu Saïed. Kusaidia nchi za Kiafrika ili ziweze kukua kwa uhuru kutokana na kugawana ujuzi (na pesa) kutoka Ulaya, kwa lengo la kupunguza kasi ya kuwasili kwa wahamiaji kwenye pwani ya Italia ambayo tangu mwanzo wa 2023 tayari ni watu 83,400 ikilinganishwa na 34,000 ya kipindi kama hicho cha  mwaka 2022. Ili kupata maendeleo, hata hivyo, “tunahitaji hatua ya mshikamano, iliyodhamiriwa na yenye uwezo wa kutazama mbele” ilieleza , serikali, kwa sababu ni kwa njia hii tu “itawezekana kushinda shughuli za uhalifu za wafanyabiashara wa binadamu, kusaidia na kukuza uhamiaji wa kisheria katika muktadha uliodhibitiwa”. Kwa kifupi, washirika wanahitajika, ambapo Roma imejaribu kutafuta na iwe katika Ulaya na mahali pengine kutokana na operesheni kali ya kidiplomasia ambayo inaonekana kuwa imefanikiwa kulingana na uwepo uliothibitishwa.

Rais wa Tume ya Ulaya Bi Ursula von der Leyen na rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel walikuwapo kwenye  mkutano huo kuwakilisha (UE) Umoja wa  Ulaya  lakini muundo huo pia ulijumuisha viongozi wa karibu majimbo yote ya mwambao wa kusini wa Bahari ya Mediterania iliyopanuliwa. Mashariki ya Kati na Ghuba, mshirika wa Sahel na Pembe ya Afrika, na pia Mataifa ya Jumuiya ya Ulaya ya kutua kwanza, kwa hivyo ndio walioathiriwa zaidi na hali ya uhamiaji kama vile Ugiriki, Kupro, Malta na Hispania, na vile vile dhahiri nchini Italia.

Kwa jumla, bendera za nchi 21 zilipepea za: Algeria, Misri, Libya, Bahrain, Qatar, Falme za Kiarabu na Saudi Arabia. Miongoni mwa waliohudhuria ni wakuu wa taasisi za fedha za kimataifa kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa na mifuko ya maendeleo ya Waarabu, pamoja na Benki ya Dunia, wajumbe kutoka FAO, Mpango wa Chakula Duniani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji. Kwa upande mwingine, mkutano huo umefanyika katika mkesha wa 'UN Food Systems Summit +2 Stocktaking Moment', kilele cha mkutano wa usalama wa chakula duniani ambao unafunguliwa Jumatatu tarehe 31 Julai 2023 tena mjini Roma mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres na Waziri Mkuu Giorgia Meloni.

27 July 2023, 10:10