Tafuta

Maendeleo ya teknolojia hadi kufikia akili bandia na matumizi ya roboti. Maendeleo ya teknolojia hadi kufikia akili bandia na matumizi ya roboti.  (ANSA)

UNESCO yaongoza mazungumzo ya kimataifa juu ya maadili ya teknolojia ya neva

Kwa mara ya kwanza umefanyika mkutano wa kimataifa huko Paris Ufaransa ,katika Makao Makuu ya UNESCO,tarehe 13 Julai 2023 ili kuunda mfumo wa maadili katika sekta ya teknolojia ya neva.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Nchi Wanachama wa Bodi ya Utendaji ya UNESCO zimeidhinisha pendekezo la Mkurugenzi Mkuu la kufanya mazungumzo ya kimataifa ili kuunda mfumo wa kimaadili kwa sekta ya Teknolojia ya Neva inayokua na isiyodhibitiwa kwa kiasi kikubwa, ambayo inaweza kutishia haki za binadamu na uhuru wa kimsingi. Mkutano wa kwanza wa kimataifa umefanyika katika Makao Makuu ya UNESCO huko Paris, Ufaransa tarehe 13 Julai 2023.  Kwa mujibu wa taarifa kuhusu Mkutano huo wa kwanza wanabainisha kuwa “Teknolojia ya Neva inaweza kusaidia kutatua maswala mengi ya kiafya, lakini pia inaweza kufikia na kudhibiti akili za watu, na kutoa habari kuhusu utambulisho wetu, na hisia zetu. Inaweza kutishia haki zetu kwa utu, uhuru wa mawazo na faragha. Kuna haja ya dharura ya kuanzisha mfumo wa pamoja wa kimaadili katika ngazi ya kimataifa, kama UNESCO imefanya kwa ajili ya utafiti bandia,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO  Bi Audrey Azoulay.

Kuchunguza uwezo mkubwa wa teknolojia ya neva

Mkutano huo kwa njia hiyo umeanza  kuchunguza uwezo mkubwa wa teknolojia ya neva kutatua matatizo ya neva na matatizo ya akili, huku ukibainisha hatua zinazohitajika kushughulikia vitisho vinavyoleta haki za binadamu na uhuru wa kimsingi. Mazungumzo hayo yamehusisha maafisa wakuu, watunga sera, mashirika ya kiraia, wasomi na wawakilishi wa sekta binafsi kutoka kanda zote za dunia. “Weka misingi ya mfumo wa kimaadili wa kimataifa” ndiyo kauli mbiu iliyoongoza  mkutano huo wa kimataifa. Wakati mazungumzo hayo pia iliarifiwa ripoti ya Kamati ya Kimataifa ya UNESCO ya Maadili ya Kibiolojia (IBC) kuhusu “Masuala ya Kimaadili ya Teknolojia ya Neva” na utafiti wa UNESCO unaopendekeza ushahidi wa mara ya kwanza juu ya mandhari ya teknolojia ya neva, uvumbuzi, wahusika wakuu duniani kote na mielekeo mikuu.

Mkutano wa UNESCO kuhusu Tekolojia ya Neva
13 July 2023, 16:03