Tafuta

Kuwania Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake Australia na New Zealand 2023 - Kundi B - Australia na Jamhuri ya Ireland Kuwania Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake Australia na New Zealand 2023 - Kundi B - Australia na Jamhuri ya Ireland 

UN WOMEN na FIFA kushirikiana katika mashindano ya kombe la dunia

“Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN linashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA katika mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA la wanawake yaliyoanza tarehe 20 Julai 2023 mpaka 20 Agosti 2023 huko nchini Australia na New Zealand na kutazamwa na zaidi ya watu bilioni mbili duniani kote.

Taarifa iliyotolewa na UN Women huko  New York Marekani imesema kuwa  malengo ya ushirikiano huo ni kusherehekea ujuzi na mafanikio ya timu na wachezaji, kuendeleza usawa wa kijinsia katika soka, na kuzuia unyanyasaji na ubaguzi ndani na nje ya uwanja. Chini ya mwavuli huo wa ushirikiano mashirika hayo yanatoa wito wa masuala mawili makuu. Kwanza kabisa: “Kuunga Mkono Usawa wa Kijinsia”; ambapo lengo ni kutambua usawa wa kijinsia kama haki ya msingi ya binadamu na muhimu kwa ulimwengu wa amani na endelevu. Pili: “Kuungana kwa ajili ya Kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake”.  Lengo lake  ni kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana kama ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani kote.

Michuano ya kugombea kombe la dunia la mpira wa miguu limeanza huko Australia
Michuano ya kugombea kombe la dunia la mpira wa miguu limeanza huko Australia

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women,  Sima Bahous amesema: “Wanawake wanaoshindana katika Kombe hili la Dunia ni mifano ya kuigwa kwa kila msichana kwenye sayari hii. Kwa kuongeza  kuwa mashindano hayo ni ukumbusho kwamba kuna wanawake na wasichana wengi sana ambao wametengwa na ulimwengu wa michezo, na kwamba hata kwa wale wanaoshiriki mara nyingi hukumbana na ubaguzi na, hata katika baadhi ya matukio, unyanyasaji.  Kwa hiyo Kombe la Dunia la Wanawake linatuonesha ni kwa kiasi gani si wao tu bali dunia nzima inakosa wakati tunaposhindwa kumudu kutoa fursa sawa kwa wanawake na wasichana fursa sawa kama zitolewavyo kwa wanaume na wavulana.” Alikazia kusemama Mkuu huyo wa UN WOMEN.

Ushirikiano huo wa UN WOMEN na FIFA utahusisha kampeni ya kimataifa ya ‘Soka ambapo inaunganisha Dunia’, kwa kulenga kuonesha dhamira na nia ya dhati ya kushughulikia hilo kwa manufaa ya kila mtu. Miito miwili  hata hivyo  ya  kuchukua hatua kuhusu usawa wa kijinsia itakuwa ikihamasishwa kupitia kwa manahodha wa kila timu kupitia kitambaa cha unahodha wa timu. Maeneo ya matangazo katika mbao za pembeni ndani ya uwanja yatawekwa matangazo hayo, kutakuwa na bendera kubwa zitakazooneshwa uwanjani, runinga kubwa viwanjani, na kupitia mitandao ya kijamii. 

Je ni nani ataibuka na kombe la dunia kwa mpira wa miguu wanawake?
Je ni nani ataibuka na kombe la dunia kwa mpira wa miguu wanawake?

Kwa njia hiyo “Unganeni kwa Usawa wa Jinsia utakuwa ujumbe utakaoangaziwa siku 3  kunzia tarehe 30 Julai  hadhi 3 Agosti 2023 na “Unganeni Kukomesha Unyanyasaji dhidi ya Wanawake” utakuwa ujumbe ulioteuliwa wakati wa Nusu Fainali  tarehe 16 Agosti 2023. Mashirika mengine matano ya Umoja wa Mataifa yamejiunga na kampeni hiyo ya “Football Unites the World” yaani, “Mpira unaunganisha dunia”  ikiwa ni pamoja na lile la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO), la masuala ya wakimbizi (UNHCR), Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR), Mpango wa Chakula Duniani(WFP), na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO).

Kuogombea soka la dunia mpira wa miguu kwa wanawake huko Australia

 

20 July 2023, 17:18