Tanzania:Ask.Mkuu Rugambwa aonesha ukaribu kwa jumuiya ya Arusha
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kuafuatia na kifo cha Padri Pamphili Nada aliyefariki dunia mnamo tarehe 19 Julai 2023 katika Hospital ya Fem Karatu akiwa anapata matibabu na ambapo taarifa ya kifo hicho ilitolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Askofu Anton Lagweni ambaye alifika eneo la tukio na kutoa pole kwa waamini wa Parokia ya Karatu, naye Askofu Mkuu Protase Rugambwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora Tanzania na Kardinali Mteule, hivi karibuni aliyetuliwa na Baba Mtakatifu tarehe 9 Julai 2023, alitoa salamu za rambi rambi na kuonesha ukaribu wake kwa waamini wa Mbulu, Arusha. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka habari za Kimisionari Fides, zinabainisha kuwa Padre huyo alifariki wakati akipelekwa hospitalini, na mshukiwa aliuawa na wananchi waliokuwa na hasira waliokuwa wakimsubiri nje ya eneo la ajali. Na haya ndiyo aliyoyaripoti kamanda wa polisi mkoani Arusha kwa waandishi wa habari kuhusiana na mauaji ya Padre Pamphili Nada katika Parokia ya Mama Yetu Malkia wa Mitume Jimbo la Karatu Jimbo la Mbulu.
Kwa upande wa askofu Mkuu mwandamizi wa Tabora, Protase Rugambwa, ambaye Papa Francisko alimejumuisha katika orodha ya Makardinali wajao, tarehe 9 Julai 2023 aliliambia Fides kuwa watu “Walishindwa kuvumilia maumivu ya mauaji ya mchungaji wao mpendwa na kuwapiga vikali wale waliohusika na kifo cha Padre Nada. Watu walishangazwa sana na tukio hili la ghafla na la kusikitisha. Kuhusiana na ajali mbaya inaripoti kwamba mnamo Jumatano tarehe 19 Julai 2023 mwanamume mmoja alikuwa ameingia kanisani kusali, wakati badala yake fulani alimpiga Padre Nada akiwa na kitu kizito butu kilichosababisha kifo cha padri huyo wakati wa kukimbizwa hospitali. Muuaji huyo anaonekana kuwa na matatizo ya afya ya akili.
“Alikuwa ni baba wa kiroho, anayejulikana kwa imani yake kubwa na kujitolea kwake, akitamani kutimiza wajibu wake kwa ari,na ujasiri”, alitangaza Askofu Anthony Gaspar Lagwen wa Jimbo la Mbulu kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania. Kituo cha Mawasiliano cha Mwananchi kinachorusha habari na matukio mbalimbali kiliripoti taarifa za baadhi ya wakazi wa Karatu ambao walisema kuwa muuaji huyo alikuwa akiendelea na jitihada za kuingia kanisani kusali tangu juzi usiku, lakini walinzi walimzuia. Siku iliyofuata, asubuhi na mapema, yule mtu aliendelea kupiga kelele ili aruhusiwe kusali, ndipo Padri Nada alipotoka na kumtaka mlinzi amfungulie mlango. Mwaka huu pekee ni tukio la tatu la kutisha dhidi ya Kanisa la Tanzania kwa watu wenye magonjwa ya akili. La kwanza lilikuwa ni tukio la kunajisiwa kwa Kanisa Kuu la Bikira Maria, Malkia wa Amani Jimbo Kuu Katoliki la Geita mnamo tarehe 26 Februari 2023. Tendo la pili lilitokea mnamo tarehe 11 Mei 2023, ambapo mtu asiyejulikana alivunja mlango mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Charles Lwanga Jimbo Kuu la Kahama.