Tafuta

2023.07.18 Mkutano mkuu huko Rwanda  unaohusu mada ya  'Women's Delivery' 2023.07.18 Mkutano mkuu huko Rwanda unaohusu mada ya 'Women's Delivery' 

Women Deliver 2023:Ni Mkutano Wanawake kutoka ulimwenguni wanakutana Rwanda

Nchini Rwanda kuanzia tarehe 17 hadi 20 Julai 2023 unafanyika Mkutano kwa washiriki kutoka duniani kote unaojumuisha midahalo na ushiriki wa utendaji mzuri ulioandaliwa na makundi ya mashirika ya kiraia,serikali,watu binafsi,mifuko ya vyama vya hisani,hali halisi ya vijana,pamoja na jumuiya zinazokabiliwa na ubaguzi wa kimfumo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Mji wa Kigali nchini Rwanda unafanyika mkutano wa kimataifa unaoongzwa na kauli mbiu  "Women Deliver 2023," ambao uliozinduliwa tarehe 17 Julai 2023. Katika mkutano huo ulimwemwona hata aliyekuwa mke wa Nelson Mandela, Graça Machel, katika moja ya mikutano mikubwa ya sekta mbalimbali ya kuhamaisha usawa wa kijinsia, ambao hufanyika kila baada ya miaka mitatu na kwa sasa kwa mara ya kwanza  umefanyika barani Afrika, katika mjini mkuu Rwanda. Mkusanyiko huo kutoka duniani kote unaojumuisha midahalo na ushiriki wa utendaji mzuri ulioandaliwa na makundi ya mashirika ya kiraia, serikali, watu binafsi, mifuko ya  vyama vya hisani, hali halisi ya vijana, , watawa pamoja na jumuiya zinazokabiliwa na ubaguzi wa kimfumo. Kwa hiyo ni Wanawake elfu sita kutoka sayari nzima ili kuweza kuhamasisha mabadiliko.

Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya wanawake "Women's Delovery" Kigali Rwanda 17-20 Julai 2023
Mkutano wa Kimataifa kwa ajili ya wanawake "Women's Delovery" Kigali Rwanda 17-20 Julai 2023

Mpango huo ni mkubwa sana, haukuundwa kwa ajili ya walio hapo tu lakini pia kwa njia ya mtandaoni na meza za mduara za pande zote juu ya mada kuanzia afya hadi uchumi, na  elimu hadi sanaa. Katika uzinduzi huo tarehe 17 Julai, walikuwepo pamoja na marais wa Rwanda, Senegal, Ethiopia na Guinea. Mkuu Mwangalizi wa Wanawake Duniani, Bi Lia Beltrami, ambaye ni mtengenezaji wa filamu na mkurugenzi wa sanaa, mwandishi wa maonesho ya Kilio cha Wanawake ambayo, pamoja na filamu ya hali ya juu ya In-Visibles, imefika katika maeneo maalum ndani ya tukio hilo, amefafanua kwa vyombo vyatu vya Vatican news juu ya tukio hilo. Mpango wa kuzunguka kwa filamu hiyo unaoungwa mkono pia na  Baraza la Kipapa la Mawasiliano na mitandao, hiyo ndio hatua kali, na ndiyo muhtasari wa mkurugenzi ambaye siku hizi anashiriki katika kile kinachojidhihirisha kama uungawaji halisi wa ubinadamu wa kike ambaye anatamani, wengne waweze kuoneshanana kuwa kama dereva yaani nguvu kwa ajili ya ustawi na ushirikiano mzuri wa kijamii.

Mkutano kuhusu Women's Delivery huko Kigali Rwanda.
Mkutano kuhusu Women's Delivery huko Kigali Rwanda.

Washiriki  wa mifuko ya hisani watuzwa  tuzo za kimataifa, za Nobel, na harakati kubwa hapo pamoja na mambo mengine, katika uzinduzi wote ulifanywa na wanawake nchini Rwanda ambao uliwasilishwa kwa mfano kupitia wanawake wanaofanya kazi kwa ajili ya  ujenzi tofauti, kuanzia kulainisha majeraha ya makovu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa maana hiyo Bi Lia alisema Filamu ya  "Maonesho ya kilio cha wanawake" yanataka kuleta mabadiliko kupitia sanaa. Kiukweli, ni sehemu ya mpango mkubwa Emotion to generate change ambao unalenga kugusa mioyo kupitia sanaa. Ndani ya mada  zao  kuna kazi, uzazi, uhamaji wa kulazimishwa, migogoro, elimu, uzee, kazi ya watawa, mandhari ya mazingira" pia shukrani kwa msaada wa Washirika wa Kushikana Mikono ambao wameunga mkono maonesho tangu mwanzo.

Lia Beltrami
Lia Beltrami

Ni kazi ambayo ina ufanisi mkubwa hivi kwamba imefika hatimaye katika Tamasha la Sanaa na Filamu la WD2023 pamoja na kazi zingine 140 ambazo zimeshinda uteuzi kati ya maelfu yaliyowasilishwa. Baada ya miaka ambayo kila kitu kimekuwa mtandaoni, kukutana na wanawake wengi kutoka kila pembe ya dunia ni jambo la kufurahisha alisisitiza Beltrami. “Wanawake wanaofanya kazi na maelfu ya wanawake wengine, hakuna wazo moja, kuna nafasi kwa wote. Ukweli kwamba ulimwengu wa Kikatoliki upo na maonesho ni mtazamo wa juu sana. Katika ya mambo mengine katika meza ya mdua , wa pande zote  tarehe 17 ilifanyika juu ya kazi ya wanawake katika kuzaliwa upya kwa maeneo, mara nyingi wao ni watawa.

Lia Beltrami katika maandalizi ya Filamu
Lia Beltrami katika maandalizi ya Filamu

Filamu ya In-Visibles pia ilioneshwa kwa mzunguko unaoendelea, ambao tayari umeshinda Tuzo katika Tamasha la Filamu la Stockholm na katika Tamasha la Filamu la Hisani la Montecarlo. Kwa kuongeza, ilitunukiwa nchini Zimbabwe, kama sehemu ya mapitio muhimu huko Harare, na ilichaguliwa katika tamasha sita. “Ina maana kwamba wanawake hawa wasioonekana kwa mujibu wa lia  hawaonekani tena. Ukweli kwamba Afrika ni mwenyeji wa njia panda za kina na za kinabii za wanawake wenye uzoefu ambao unaweza kufanya kama kichocheo cha ukweli mwingine ambapo hali ya wanawake bado ni ya chini yenyewe ni ishara ya mchakato wa wema. Katika bara la Afrika ambalo Papa Francisko alitoa wito kuwa isisahaulike. Bi Lia Beltrami alielezea kuwa ni uthibitisho mzuri katika suala hilo kwamba: “Tayari nimepata wanawake hapa ambao walikuwa wamekwenda kumuona Papa huko Congo na Sudan Kusini. Waliniambia walikwenda kumsikiliza 'kwa sababu sauti yake ni mwanga kwa kila mtu, wengi wasiokuwa- Wakatoliki pia waliniambia hivi.”

18 July 2023, 16:57