Tafuta

2021.01.12 Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa ripoti kuhusu chakula duniani ambapo kuna uhaba wa chakula na lishe kwa ujumla. 2021.01.12 Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa ripoti kuhusu chakula duniani ambapo kuna uhaba wa chakula na lishe kwa ujumla. 

Ripoti mpya ya Mashirika ya FAO/IFAD/UNICEF/WFP/WHO:kuna hatari ya njaa

Ripoti mpya ya Mashirika ya FAO/IFAD/UNICEF/ WFP/WHO kuhusu hali halisi ya chakula na lishawkatika ulimwengu.Kwa mujibu wa tafiti za karibuni ni kwamba ni karibia watu milioni 735 ambao wanateseka na njaa leo hii kulingana na watu milioni 613 wa takwimu za mnamo 2019.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Kuendeleza kazi ya mtu, wakati ambapo hatua madhubuti na zenye uwezo haziepukiki kutokomeza janga la njaa duniani, ambalo linaendelea badala ya kupungua. Ulikuwa ni mwaliko wa Papa  Francisko kwa washiriki wa kikao cha 43 cha Mkutano wa FAO, katika ujumbe kwa lugha ya Kihispania  uliousomwa na Askofu Mkuu Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya: Chakula na Kilimo (FAO, IFAD na  WFP) mnamo tarehe 3 Julai 2023. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu alibanisha kuwa Mamilioni ya watu wanaendelea kuteseka kutokana na umaskini na utapiamlo duniani, kutokana na migogoro ya silaha, pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na majanga ya asili yanayotokana nao na huvyo Papa Francisko alishutumu na, ambaye kwa mujibu wake kuhama kwa watu wengi, kunaongeza madhara mengine, mivutano ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi kwa kiwango cha sayari inadhoofisha juhudi zinazofanywa ili kuhakikisha uboreshaji wa hali ya maisha ya watu, kwa sababu ya utu wao wa asili.

Ukosefu wa chakula unahatarisha maafa makubwa na hasa kwa watoto
Ukosefu wa chakula unahatarisha maafa makubwa na hasa kwa watoto

Umaskini, ukosefu wa usawa, ukosefu wa rasilimali za msingi kama vile chakula, maji ya kunywa, huduma za afya, elimu, ni dharau kubwa kwa utu wa binadamu, Papa alikariri na kukemea jinsi lengo la kufikia sufuri ya njaa bado halijafikiwa na jumuiya ya kimataifa. Kwa  hiyo hiyo Baba Mtakatifu Francisko, alibainisha kuwa mila za kiutamaduni na maalum za kiutamaduni za jumuia mbali mbali haziwezi kubadilishwa au kuharibiwa kwa jina la wazo fupi la maendeleo ambalo, kiukweli, lina hatari ya kubadilishwa kuwa ukoloni wa kiitikadi”. Katika muktadha huo  Mtazamo wa njaa unatishia zaidi ya watu milioni 122 zaidi duniani kote kuliko mwaka wa 2019, kutokana na janga hili na mfululizo wa majanga ya hali ya tabianchi na migogoro, ikiwa ni pamoja na vita nchini Ukraine. Haya ndiyo yanayosomeka katika ripoti za hivi karibuni yenye kupewa  jina la kichwa   “Hali ya usalama wa chakula na lishe duniani (SOFI), iliyochapishwa kwa pamoja  na mashirika matano maalumu ya Umoja wa Mataifa. Bila mabadiliko bila shaka, Lengo la Maendeleo Endelevu la kumaliza njaa ifikapo 2030 halitafikiwa. Walioonya ni  Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP)

Msukumo mpya katika mapambano dhidi ya njaa

Katika Toleo la 2023 la ripoti hiyo linaonesha kuwa, mnamo 2022, njaa iliathiri kati ya watu milioni 691 na 783, na wastani wa milioni 735 waliugua njaa. Idadi hiyo inawakilisha ongezeko la watu milioni 122 ikilinganishwa na 2019, mwaka mmoja kabla ya kuzuka kwa janga la UVIKO-19. Ikiwa ni kweli kwamba, kati ya 2021 na 2022, data kuhusu njaa duniani ilikabiliwa na upungufu, ni hakika kwamba maeneo mengi ya sayari sasa yanakabiliana na kuzuka upya kwa majanga ya chakula. Licha ya mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na njaa katika bara la Asia na Amerika Kusini, mwaka wa 2022, hali hiyo bado ilionekana kukua katika Asia ya Magharibi, Karibiani na kanda zote ndogo za bara la Afrika. Huku mtu mmoja kati ya watano akiathiriwa na njaa, ambayo ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa kimataifa, Afrika inasalia kuwa eneo lililoathiriwa zaidi na dharura hii.

Ukame ndio usiseme katika maeneo mengi barani Afrika kwa mfano ukanda wa Sahel
Ukame ndio usiseme katika maeneo mengi barani Afrika kwa mfano ukanda wa Sahel

“Hakuna uhaba wa sababu za matumaini: baadhi ya mikoa iko njiani kufikia malengo yanayohusiana na lishe ifikapo 2030. Kwa ujumla, hata hivyo, tunahitaji kuja kuokoa Malengo ya Maendeleo Endelevu, kwa uingiliaji kati wa kimataifa wenye nguvu na wa haraka. Tunahitaji kujenga ustahimilivu dhidi ya migogoro na mishtuko inayosababisha uhaba wa chakula, kutoka kwa migogoro hadi hali ya hewa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres katika ujumbe kwa njia ya  video uliotangazwa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Wakuu wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa, ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa FAO QU Dongyu; Rais wa IFAD, Alvaro Lario; Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell; Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, waliandika katika Dibaji ya ripoti hiyo kuwa “Kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu 'Zero ifikapo 2030 bila shaka ni changamoto kubwa. Kiukweli, inatabiriwa kwamba, katika 2030, karibu watu milioni 600 bado watakuwa na njaa. Sababu kuu zinazosababisha uhaba wa chakula na utapiamlo ni 'kawaida yetu mpya', ambapo hatuna chaguo ila kuongeza maradufu juhudi zetu za kubadilisha mifumo ya chakula, tukiiwezesha kufikia malengo ya maendeleo endelevu(SDG 2).”

Sio njaa tu

Hali ya usalama wa chakula na lishe iliendelea kuwa mbaya mwaka 2022. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takriban asilimia 29.6 ya watu duniani, au watu bilioni 2.4, hawakuwa na uhakika wa kupata chakula mara kwa mara, jambo ambalo linaonyesha kuwepo kwa uhaba wa chakula wa wastani au mkubwa. Kati ya hawa, takriban watu milioni 900 wamekabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Wakati huo huo, uwezo wa watu kupata chakula cha afya umezorota duniani kote: mwaka 2021, asilimia 42 ya wakazi wa sayari, au zaidi ya watu bilioni 3.1, hawakuweza kumudu chakula cha afya. Ikilinganishwa na 2019, hii ni sawa na ongezeko la jumla la watu milioni 134. Mamilioni ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wanaendelea kukabiliwa na utapiamlo: mwaka 2022, watoto milioni 148 chini ya umri wa miaka mitano (asilimia 22.3) walidumaa, milioni 45 (asilimia 6.8) walikuwa na dalili za kukonda kupita kiasi na milioni 37 (asilimia 5.6) walikuwa na uzito kupita kiasi.

Kila kona na hasa wanaoteseka watoto
Kila kona na hasa wanaoteseka watoto

Maendeleo yamepatikana katika unyonyeshaji wa kipekee, huku asilimia 48 ya watoto wachanga hadi miezi 6 wakinufaika na mila hiyo, ambayo ni karibu na lengo la 2025. Ili kufikia malengo ya 2030 ya utapiamlo, hatua zaidi zinahitajika. Ripoti hiyo pia inachunguza kuongezeka kwa ukuaji wa miji kama inayoathiri ubora na aina ya lishe ya watu. Kwa kuzingatia kwamba karibu watu saba kati ya kumi wataishi mijini ifikapo 2050 kulingana na utabiri, serikali na wengine waliojitolea kukabiliana na njaa, ukosefu wa chakula na utapiamlo watalazimika kujaribu kuelewa michakato hii ya ukuaji wa miji na kuzizingatia katika ufafanuzi wa sera zao. Hasa, dhana rahisi ya "pengo" kati ya jiji na mashambani haitoshi tena kuelewa jinsi ukuaji wa miji unaathiri mifumo ya chakula cha kilimo. Mtazamo changamano zaidi unahitajika, unaoendelezwa hadi katika mwendelezo wa mijini na vijijini, ambao unazingatia kiwango cha muunganisho kati ya watu na aina za miunganisho inayounganisha maeneo ya mijini na vijijini.

Ripoti mpya ya mashirika ya UN inayoeleza uhaba wa chakula tangu 2019 hadi sasa
13 July 2023, 16:37