Tafuta

Mkutano Mkuu II kati ya  Urussi na Afrika kuhusu "Uchumi na ubinadamu umekunja jamvi. Mkutano Mkuu II kati ya Urussi na Afrika kuhusu "Uchumi na ubinadamu umekunja jamvi. 

Putin atia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na zaidi ya nchi 40 za Afrika

Wakati viongozi Afrika wakifanya mkutano na Rais Putin mashambulizi yaliendelea huko Ukrane, Kombora la Kirusi liligonga jengo la ghorofa huko Dnipro na kuwajeruhi 9,roketi ililipuka katika mkahawa huko Taganrog, mji wa bandari huko Rostov na kujeruhi watu 16.Rais alitangaza nchi yake kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na zaidi ya nchi 40 za Afrika.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Wakati Rais wa Urussi Vladmir Putin anatazamia  siku zijazo na kujifungulia katika Nchi za bara la Afrika, hali ya Ukraine ya kutoegemea upande wowote ina umuhimu mkubwa kwa Shirikisho la Urussi. Alisema wakati wa kukutana na viongozi wa Afrika katika mkutano huko Mtakatifu Peterburg  tarehe 27-28 Julai 2023 ambapo mkutano huo umekunja jamvi lake. Katika nchini ya Ukraine mashambulizi ya mabomu yanaendelea hadi sasa  bila kukoma kwani Kombora la Urussi liligonga jengo la ghorofa huko Dnipro na kuwajeruhi  watu 9, wakati roketi ililipuka katika mkahawa huko Taganrog, mji wa bandari katika mkoa wa Rostov nchini Urussi na kujeruhi watu 16. Milipuko pia katika eneo la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia iliyorekodiwa na waangalizi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia (International Atomic Energy Agency (IAEA).

Mkutano kati ya Urussi na Afrika umehitimishwa
Mkutano kati ya Urussi na Afrika umehitimishwa

Kwa njia hiyo basi kutoka katika mkutano huo  uliohitimishwa, mkuu wa Kremlin alijifungua kwa bara la Afrika. Baada ya kuahidi nafaka ya bure kwa nchi zilizo katika matatizo makubwa zaidi, alizungumzia kufutwa kwa deni la nje la dola bilioni 23. Rais Putin alikuwa na maneno ya kuthamini majaribio ya upatanisho yaliyofanywa na baadhi ya nchi za Kiafrika na hatimaye akathibitisha ukaribu wake na bara hilo kwa kuzingatia mpangilio mpya wa ulimwengu: wa haki na wa kidemokrasia, wa pande nyingi, kwa kuzingatia kanuni zinazotambulika duniani kote za sheria za kimataifa na kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Ni marais wa nchi 17 tu waliodhuria na wengine waliwakilishwa na mawaziri
Ni marais wa nchi 17 tu waliodhuria na wengine waliwakilishwa na mawaziri

Rais Putin alisema hayo 28 Julai ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano Mkuu wa II wa kilele wa Urussi na viongozi wa Afrika. Rais Putin alisema kwa madhumuni ya kuimarisha uwezo wa mataifa ya Afrika, wanapanga ushirikiano wa kijeshi na nyanja za kiufundi za kijeshi. Putin alidha alithibitisha kuwa  mataifa ya Afrika yalipokea silaha mbalimbali na teknolojia, baadhi bila malipo, kwa lengo la kuimarisha usalama na uhuru wa mataifa hayo. Wawakilishi kutoka nchi za Afrika wamealikwa kushiriki kikamilifu katika mikutano ya kijeshi iliyoandaliwa na Urussi inayoshughulikia masuala ya kiufundi ya silaha hizo na kupata mafunzo kuvielewa vifaa hivyo na matumizi yake. Rais Putin pia  alisisitiza kuwa Urussi itaendelea kuwa msambazaji wa kutegemewa wa nafaka kwa nchi za bara Afrika. Ahadi hiyo ilikuja baada ya Urusi kujiondoa katika mkataba ambao uliruhusu nafaka za Ukraine kuuzwa nje kupitia Bahari Nyeusi. Lakini ikumbukwe kuwa Ukraine ni muuzaji mkuu wa nafaka barani Afrika.

Rais Museveni na Rais Putin
Rais Museveni na Rais Putin

Kadhalika Urussi pia inalenga kupanua uwepo wake barani Afrika kwa kufungua balozi mpya na kuongeza wafanyakazi wake katika uwakilishi wa diplomasia zilizopo. Baada ya miito ya amani nchini Ukraine wakati wa Mkutano huo Rais Putin alisisitiza nia yake ya kufanya mazungumzo kuhusu Ukraine. Hata hivyo Putin amesema kuwa hakuna njia ya kulazimisha upande wowote katika mazungumzo kama hayo. Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak, amekosoa matamshi hayo ya Putin na kusema haina maana kwasasa kwa  Ukraine kufanya mazungumzo na Urusi. Katika hotuba yake ya kufunga mkutano huo wa kilele, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Azali Assoumani, alisema pendekezo la Putin la kutoa nafaka halitoshi. Assoumani alisema hatua hiyo ni muhimu lakini huenda isitoshe kufanya hivyo akiongeza kwamba kile wanachohitaji kuafikia ni usitishaji wa mapigano.

Picha ya viongozi wa kiafrika wakiwa na Putin
Picha ya viongozi wa kiafrika wakiwa na Putin

Kiongozi huyo ya Umoja wa Afrika alisema kuwa rais Putin ameonesha kuwa yuko tayari kushiriki katika mazungumzo na kutafuta suluhisho na kwamba sasa wanahitaji kuushawishi upande wa pili. Wakati wa mikutano na wakuu wa nchi na serikali wa Afrika, Rais Putin alitaka kuonesha kwamba hajatengwa kimataifa. Kulingana na ikulu ya Kremlin, nchi 49 kati ya 54 za bara Afrika zimewakilishwa, huku wakuu wa Nchi  na Serikali wakiwa ni 17 tu, hii ikiwa idadi ya chini ikilinganishwa na Mkutano wa  kwanza mnamo  mwaka 2019.

Katika picha ya pamoja anaonekana hata Waziri Mkuu  wa Tanzania Majaliwa mara baada ya Mkutano Mkuu II kati ya Urussi na Afrika
Katika picha ya pamoja anaonekana hata Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa mara baada ya Mkutano Mkuu II kati ya Urussi na Afrika
29 July 2023, 11:25