Tafuta

Mapinduzi ya Niger: Hawa ni wale wanauunga mkono Jeshi la mapinduzi nchini Niger. Mapinduzi ya Niger: Hawa ni wale wanauunga mkono Jeshi la mapinduzi nchini Niger.  (ANSA)

Niger:ECOWAS inataka Rais Mohamed Bazoum aachiliwe mara moja!

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) inataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Mohamed Bazoum halali wa Niger anayetambuliwa na ECOWAS.Kulingana na mkuu wa diplomasia ya Ufaransa:Ecowas ilijieleza kwa uwazi na pengine itafanya mkutano wake Julai 30.UNICEF ina wasiwasi kwa watoto milioni mbili.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Huko Niamey, tarehe 27 Julai 2023, jeshi lilitoa msaada wake kwa wapangaji mapinduzi waliomteka nyara rais wa Niger siku ya Jumatano jioni tarehe 26 Julai 2023. Viongozi hao wa mapinduzi waliishutumu Ufaransa, ambayo ina wanajeshi 1,500 nchini Niger, kwa kukiuka kufungwa kwa mpaka kwa kutua ndege ya kijeshi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey. Waliwaomba “mara moja na kwa wote kufuata madhubuti na masharti” yaliyochukuliwa pamoja. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) inataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Mohamed Bazoum ambaye anasalia kuwa rais halali na halali wa Niger anayetambuliwa na ECOWAS.

Cha kushangaza,wanaounga mkono Jeshi la mapinduzi wanasheherekea katika Ikulu
Cha kushangaza,wanaounga mkono Jeshi la mapinduzi wanasheherekea katika Ikulu

Kwa mujibu wa  mkuu wa diplomasia ya Ufaransa, alisema kuwa “Ecowas ilijieleza kwa uwazi kabisa na pengine itafanya mkutano wa kilele siku ya Dominika”, yaani tarehe 30 Julai 2023.  Hata hivyo nchini “Ufaransa inalaani jaribio la mapinduzi kwa maneno makali. Ikiwa unanisikia nikizungumzia jaribio la mapinduzi, ni kwa sababu hatulichukulii kuwa la uhakika” alisema  Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bi Catherine Colonna. Na Rais wa Niger alisema yuko katika afya njema na kwamba “hatutaki yeye tu bali pia familia yake iachiliwe kwa usalama kamili kama sharti la kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.”

Unicef, ina wasiwasi mkubwa kwa watoto milioni mbili

Wakati  mamabo yanaendelea hayo ya mapinduzi , hata UNICEF inaelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kile kinachotokea Niger siku hizi, ambacho kinahatarisha kuzidisha hali ya kibinadamu ambayo tayari ni hatari nchini humo. Watu milioni 3.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu, ambapo milioni 2 ni watoto, na 430,000 chini ya umri wa miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo wa kukithiri. Hayo yalisisitizwa na msemaji wa Unicef ​​​​Italia Andrea Iacomini.

Shida za kukosa chakula na hasa katika sehemu zenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe
Shida za kukosa chakula na hasa katika sehemu zenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe

Niger tayari inakabiliwa na mchanganyiko wa migogoro ya haraka na ya muda mrefu kama vile ukame, uhaba wa chakula, mafuriko ya mzunguko, magonjwa ya milipuko na migogoro, ambayo yana matokeo tofauti kwa ajili ya maisha na ustawi wa watoto na familia zao. Kufikia Juni 2023, kulikuwa na watu  358,000 waliosajiliwa nchini humo wakimbizi wa ndani na wakimbizi 285,000 na wanaotafuta hifadhi. Idadi ya watu waliokimbia makazi yao imeongezeka kwa 35.5% tangu Juni 2022. Jumla ya shule 987 zimefungwa, na kuathiri watoto 86,000 nchini kote, wakiwemo wasichana na wavulana 41,000.

28 July 2023, 15:43