Tafuta

Jenerali Abdourahmane Tiani,amejitangaza kuwa mkuu mpya wa Niger Jenerali Abdourahmane Tiani,amejitangaza kuwa mkuu mpya wa Niger 

Niger:A.Tchiani,mkuu wa walinzi wa rais,ajitangaza kuwa mkuu wa Nchi

Siku mbili baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Bazoum kiongozi Jenerali Abdourahamane Tchiani,mkuu wa walinzi wa rais,alijitangaza kuwa mkuu mpya wa nchi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Abdourahamane Tchiani, mkuu wa walinzi wa rais, kwa sasa ndiye anaonekana kuwa  sura mpya ya madaraka nchini Niger. Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 64 aliongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum, kwa madai ya kukomesha kile kilichoitwa “Jamhuri ya Saba” nchini humo. Tichiani alisoma taarifa hiyo kwenye televisheni ya taifa yenye nukuu iliyoandikwa juu zaidi ikimuorodhesha kama “Rais wa Baraza la Kitaifa laKulinda Nchi Mama,” iliyopindua serikali. Na alihalalisha kunyakua madaraka kwa kunyooshea kidole chake "ukosefu wa hatua za kukabiliana na mzozo wa kiuchumi na kuzorota kwa hali ya usalama katika nchi iliyodhoofishwa na ghasia za vikundi vya kijihadi". Na zaidi Bazoum ilijaribu kuwashawishi watu kwamba kila kitu kinaendelea vizuri, lakini ukweli mbaya ni vifo vingi, watu waliokimbia makazi yao, fedheha na kufadhaika. Njia ya usalama kwa hiyo bado  haijaleta usalama licha ya kujitolea sana.

Mataifa ya Afrika na mapinzu ya kijeshi

Wafuasi wa mapinduzi hayo hata hivyo walionekana walipeperusha bendera za Urussi barabarani, wakishambulia makao makuu ya chama tawala, wakashambulia hata  baadhi ya wanasiasa na wakitukana dhidi ya kuingilia Ufaransa. Matukio hayo hayakumwacha Wagner Yevgeny Prigozhin kutojali, ambaye ana vikosi vyake  vilivyotumwa katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso. Yeye alisema  "Kilichotokea Niger si chochote zaidi ya mapambano ya watu wa Niger dhidi ya wakoloni ambao wanajaribu kuweka sheria zao za maisha", alisema katika ujumbe uliotangazwa na idhaa inayoshirikiana naye huko "akihakikishia kwamba inaweza kurejesha utulivu". Kwa kifupi, licha ya kufunguliwa kwa mazungumzo yanayowezekana na kurudi nyuma kwa jeshi linalotarajiwa katika saa chache zilizopita na jumuiya ya kimataifa, Niger, ambayo ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa urani duniani, inajikuta ikilazimika kukabiliana na Mapinduzi ya tano ya kijeshi tangu uhuru kutoka kwa Wafaransa, yaliyoidhinishwa mnamo 1960.

Hawa ni mamia ya wanaounga mkono mapinduzi ya Niger huku wakipeperusha hata bedera ya Urussi
Hawa ni mamia ya wanaounga mkono mapinduzi ya Niger huku wakipeperusha hata bedera ya Urussi
29 July 2023, 12:00