Tafuta

Ujumbe wa wakuu saba wa Nchi za Kiafrika ambao unalenga kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini Ukraine, unatembelea Kiev na Jumamosi tarehe 17 Juni 2023 huko Saint Petersburg. Ujumbe wa wakuu saba wa Nchi za Kiafrika ambao unalenga kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini Ukraine, unatembelea Kiev na Jumamosi tarehe 17 Juni 2023 huko Saint Petersburg. 

Umoja wa Afrika Unatafuta Suluhu ya Amani Kati ya Ukraine na Urusi

Ujumbe wa wakuu saba wa Nchi za Kiafrika ambao unalenga kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini Ukraine, unatembelea Kiev, Ijumaa tarehe 16 Juni 2023 na hivyo kukutana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Jumamosi tarehe 17 Juni 2023 huko Saint Petersburg, ili kukutana na hatimaye kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi. Tayari maandalizi muhimu ya kukutana na viongozi hawa wawili yamekwisha kukamilika, umebaki utekelezaji wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Umoja wa Afrika: Ujumbe wa wakuu saba wa Nchi za Kiafrika ambao unalenga kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini Ukraine, unatembelea Kiev, Ijumaa tarehe 16 Juni 2023 na hivyo kukutana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Jumamosi tarehe 17 Juni 2023 huko Saint Petersburg, ili kukutana na hatimaye kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi. Ziara ya wakuu wa nchi za Kiafrika ilitangazwa na Mfuko wa Brazzaville “Brazzaville Foundation,” Asasi isiyo ya Kiserikali (NGO) iliyoanzishwa London nchini Uingereza kunako mwaka 2014, ambayo inasema iliwezesha "mikutano muhimu ya kidiplomasia katika maandalizi ya ujumbe wa kulinda amani wa Afrika 'Road to Peace' kwa mzozo wa Ukraine na Urusi,” Viongozi hawa ni kutoka Jamhuri ya Kongo, Rais Denis Sassou Nguesso, kutoka Uganda, Rais Yoweri Kaguta Museveni, kutoka Senegal, ni Rais Macky Sall, kutoka Zambia, ni Rais Hakainde Hichilema, na kutoka Misri, ni Rais Abdel Fattah al-Sisi. Hivi karibuni, Rais Ramaphosa wa Afrika ya Kusini alikuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Putin kuhusu ujumbe wa kulinda amani wa viongozi wa Afrika nchini Ukraine na Urusi, kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Afrika Kusini. mazungumzo ya simu na Rais Putin yalifanyika baada ya mkutano wa Jumatatu, tarehe 5 Juni 2023 kati ya viongozi wa Afrika kama sehemu ya maandalizi ya mikutano na Rais Putin na Zelensky, na kujadili njia za kukomesha vita nchini Ukraine.

Umoja wa Afrika unatafuta suluhu ya amani kati ya Urusi na Ukraine
Umoja wa Afrika unatafuta suluhu ya amani kati ya Urusi na Ukraine

Siku ya Jumanne, mjini Pretoria, Mkuu wa Nchi wa Ureno, Marcelo Rebelo de Sousa, alisifu jukumu la Afrika Kusini na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, katika ujumbe wa Afrika unaotaka kujadili amani kati ya Urusi na Ukraine.Umoja wa Afrika: Ujumbe wa wakuu saba wa Nchi za Kiafrika ambao unalenga kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini Ukraine, unatembelea Kiev, Ijumaa tarehe 16 Juni 2023 na hivyo kukutana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Jumamosi tarehe 17 Juni 2023 huko Saint Petersburg, ili kukutana na hatimaye kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Urusi. Ziara ya wakuu wa nchi za Kiafrika ilitangazwa na Mfuko wa Brazzaville “Brazzaville Foundation,” Asasi isiyo ya Kiserikali (NGO) iliyoanzishwa London nchini Uingereza kunako mwaka 2014, ambayo inasema iliwezesha "mikutano muhimu ya kidiplomasia katika maandalizi ya ujumbe wa kulinda amani wa Afrika 'Road to Peace' kwa mzozo wa Ukraine na Urusi,” Viongozi hawa ni kutoka Jamhuri ya Kongo, Rais Denis Sassou Nguesso, kutoka Uganda, Rais Yoweri Kaguta Museveni, kutoka Senegal, ni Rais Macky Sall, kutoka Zambia, ni Rais Hakainde Hichilema, na kutoka Misri, ni Rais Abdel Fattah al-Sisi. Hivi karibuni, Rais Ramaphosa wa Afrika ya Kusini alikuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Putin kuhusu ujumbe wa kulinda amani wa viongozi wa Afrika nchini Ukraine na Urusi, kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Afrika Kusini. mazungumzo ya simu na Rais Putin yalifanyika baada ya mkutano wa Jumatatu, tarehe 5 Juni 2023 kati ya viongozi wa Afrika kama sehemu ya maandalizi ya mikutano na Rais Putin na Zelensky, na kujadili njia za kukomesha vita nchini Ukraine. Siku ya Jumanne, mjini Pretoria, Mkuu wa Nchi wa Ureno, Marcelo Rebelo de Sousa, alisifu jukumu la Afrika Kusini na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, katika ujumbe wa Afrika unaotaka kujadili amani kati ya Urusi na Ukraine.

Umoja wa Afrika
14 June 2023, 15:07