Ghana:Suluhisheni migogoro ya ndani ili kuondoa ardhi ya makundi ya kijihadi!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Lazima kuwa na umakini juu ya vitisho vya kigaidi kutoka mataifa jirani kama vile Burkina Faso, Togo na Ivory Coast. Ndivyo wameomba Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ghana (GCBC)katika wito ulio zinduliwa mnamo tarehe 31 Mei na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ghana, Askofu Mathayo Kwasi Gyamfi, wa Jimbo katoliki la Sunyani wakati wa kikao cha majadiliano ya kikanda kuhusu maendeleo ya migogoro katika mkoa wa Bono huko Sunyani.
Maandalizi ya mkutano kwa makundi yote ya kikanisa na kijamii
Sekretarieti ya Kitaifa ya Kanisa Katoliki Ghana iliandaa mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa kimila, wawakilishi wa vyombo vya kidini, vyombo vya usalama, vikundi vya vijana, wanasiasa, vyama vya wafanyabiashara na wanafunzi wa shule za sekondari. Kwa hiyo Askofu mkuu Gyamfi alisema kuwa, ulinzi na usalama wa taifa hauna budi kuwa jambo la watu wote na kutoa wito wa kujitolea kwa pamoja kwa nchi iliyo salama na yenye maelewano zaidi. “Kila mtu lazima afanye sehemu yake kusaidia kukuza amani, utulivu na mshikamano wa kijamii”, alisema.
Kuzuia kuliko kutibu
Nchi ya Ghana inachukuliwa kuwa mojawapo ya nchi tulivu zaidi katika Afrika Magharibi lakini kuwepo kwa migogoro iliyofichika, kama vile ile iliyoko katika eneo la Bawku kaskazini kwenye mpaka na Burkina Faso inaweza kutoa mazingira yenye rutuba ya kujipenyeza na vikundi vya wanajihadi vilivyopo katika mataifa jirani. Wanajihadi kutoka Burkina Faso wanaweza kutoa msaada kwa wapiganaji, silaha au mafunzo kwa pande zote mbili kama njia ya kushinda washirika wa ndani kwa uasi wa siku zijazo dhidi ya serikali ya Accra. Katika muongo uliopita imeonekana jinsi vikundi vya jihadi vimeweza kuenea nchini Mali, Burkina Faso na Niger kwa kutumia mizozo ya ndani.
Makundi ya kijihadi yanatafuta kuingia kwa kulenga vikosi vya usalama
Katika miaka ya hivi karibuni, wanajihadi wameingia nchini Ghana, wakilenga vikosi vya usalama km. 40 tu kutoka Bawku kuvuka mipaka ya Burkina Faso na Togo. Kwa sababu hiyo Baraza la Maaskofu nchini Ghana (GCBC) pamoja na hali halisi nyingine za Kanisa Katoliki nchini Ghana linaunga mkono mipango inayolenga kutatua migogoro ya ndani. Kwa upande wa mkoa wa Bono, Waziri wa Mkoa wa Bono Justina Owusu-Banahene alisema ni moja ya mikoa mitatu yenye amani nchini na kupongeza vyombo vya usalama kwa kusaidia kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo. Pamoja na hayo, Waziri wa Kanda alisema kuwa changamoto za kiusalama kama vile migogoro ya kudumu miongoni mwa machifu wa makabila, migogoro ya ardhi na migogoro, uchimbaji haramu wa madini, ukosefu mkubwa wa ajira na shughuli za wafugaji wanaohamahama wa Fulani zinatishia amani na utulivu wa eneo hilo.