Tafuta

Kila mwaka tarehe 3 Mei ni Siku ya Kimataifa ya Vyombo vya habari. Kila mwaka tarehe 3 Mei ni Siku ya Kimataifa ya Vyombo vya habari.  (AFP or licensors)

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2023:kuunda mstakhabali wa kujieleza

Taarifa potofu na kauali za chuki,Wana habari na vyombo vya habari,Uhamasishaji wa haki na uhuru wa wanahabari,Tuzo ya Uhuru wa vyombo vya Habari ya Umoja wa Mataifa;Ndiyo yaliyomo katika kilele cha miaka 30 ya Siku ya kKmataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,ilyoandaliwa na UNESCO katika UN, New York Marekani Mei 2.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Tarehe 3 Mei 2023 Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UN) inaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kwa kuongoza na kauli mbiu iliyochaguliwa ya  kwa mwaka huu:  “Kuunda mustakbali wa haki: uhuru wa kujieleza kama chachu ya haki zote za binadamu.” Katika kuelekea kilele hicho, Umoja wa Mataifa tarehe 2 Mei 2023 umeadhimisha miaka 30 ya siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari katika tukio maalum lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Tukio hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliwaleta Pamoja watetezi wa haki za binadamu, wakuu wa mashirika ya mawasiliano na vyombo vya habarina wanahabari Hafla ya maadhimisho hayo imefunguliwa na mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay lakini pia kulikuwa na wazungumzaji wengine mbalimbali ukiwemo ujumbe maalum kwa njia ya video kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres.

Waandishi 67 wa vyombo vya habari walikufa kwa 2022

Kupitia ujumbe wake wa video kwa ajili ya siku hiyo, Katibu Mkuu  amesema “Uhuru wetu wote unategemea uhuru wa vyombo vya habari.” Kwa hiyo, utendakazi kamili wa sekta hiyo ndio msingi wa demokrasia na haki. Lakini alionya kwamba uhuru huu unashambuliwa, na kwamba ukweli unatishwa na habari zisizo sahihi na kauli za chuki ambazo zinatia ukungu kati ya ukweli na hadithi na kati ya sayansi na njama. Bwana Guterres anaongeza kuwa kuongezeka kwa mkusanyiko wa tasnia ya habari mikononi mwa wachache, kuanguka kifedha kwa makumi ya mashirika huru ya habari na kuongezeka kwa sheria na kanuni za kitaifa ambazo zinakandamiza wanahabari kunazidi kupanua udhibiti na kutishia uhuru wa kujieleza. Afghanistan inaadhimisha Siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani  waandishi wa habari kwa kazi yao ynye kumulika masuala muhimu ya kitaifa na kisiasa,na kwa ujumla wafanyakazi wa tasnia ya habari wakilengwa wanapofanya kazi zao, kunyanyaswa, kutishwa, kukamatwa na kufungwa. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amebainisha kuwa wafanyakazi wasiopungua 67 waliuawa mwaka 2022 na hii inawakilisha ongezeko la asilimia 50 kutoka 2021. Takriban asilimia 75 ya waandishi wa habari wanawake wamekumbana na ukatili mtandaoni na mmoja kati ya wanne ametishiwa kimwili.

Uhuru wa kujieleza na jukumu la haki za binadamu

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi la Utaladauni UNESCO Audrey Azouley akizungumza katika tukio hilo amesema duniani kote mazungumzo ya kisiasa na kijamii yenye mgawanyiko, mmomonyoko wa uaminifu, kuwepo kwa hali ya dharura na kuzimwaa kwa mitandao ikiwemo ya kijamii, ukandamizaji wa sauti muhimu na vyombo vya habari huru, ukame wa tarifa kwa sababu ya kuporomoka kwa vyombo vya habari vya mitindo ya kitamaduni na kukabiliana na kauli za chuki na madhara mtandaoni ambayo yanapuuza viwango vya habari kimataifa, vinaleta vitisho vipya kwa uhuru wa kujieleza, na jukumu la msingi la haki za binadamu.

Kwa mwaka 30 wa  siku hii ni kuhakikisha uhuru wa habari hauna ukandamizwaji

Mkuu huyo wa Unesco aliongeza kusema kuwa kutokana na changamoto kama hizo na kukabiliana na hali hizi mbaya na vitisho, kwamba uhuru wa vyombo vya habari, usalama wa waandishi wa habari na upatikanaji wa habari inakuwa ni nguzo muhimu. “Haki ya uhuru wa kujieleza", iliyoainishwa katika Kifungu cha 19 cha Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, ni sharti na kichocheo cha kufurahia haki nyingine zote za binadamu. Maadhimisho haya ya mwaka huu ya miaka 30 ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani ni wito wa kuhakikisha kuna uhuru wa habari na kutokuwa na ukandamizaji, pamoja na vyombo huru vya habari, vingi na tofauti, kama ufunguo muhimu wa kufurahia haki nyingine zote za binadamu.”

Lengo la siku ni kulinda vyombo vya habari na wafanyakazi

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Umoja wa Mataifa linabainisha kwamba Wakati wa hafla hiyo pia washindi wa tuzo ya UNESCO ya Guillermo Cano ya Uhuru wa vyombo vya Habari duniani imetangazwa na washindi ni wanawake watatu wanahabari nchini Iran ambao wanatumikia kifungo. Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka kwa mtu, shirika au taasisi ambayo imetoa mchango bora katika kutetea au kukuza uhuru wa vyombo vya habari popote duniani, hasa ikiwa hatari zinahusika. Na ikumbukwe Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ulimwenguni ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1993, kufuatia mapendekezo ya kikao cha 26 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO mwaka wa 1991. Siku hii inaadhimisha kanuni msingi za uhuru, inachunguza hali ya uhuru duniani kote, inalinda vyombo vya habari dhidi ya kujitegemea na hulipa kodi kwa waandishi wa habari ambao wamepoteza maisha yao wakiwa kazini.

Siku ya Vyombo vya habari kimataifa 2023
03 May 2023, 09:53