Tafuta

Aina za Pasta inayotengenzwa kwa ngano. Aina za Pasta inayotengenzwa kwa ngano. 

Migogoro ya kivita inaongeza baa la njaa ulimwenguni!

Data kutoka Ripoti ya hivi karibuni kuhusu Usalama wa Chakula Duniani(GFSR)inabainisha watu karibu milioni 260 duniani wanakabiliwa na njaa.Hati hiyo ilihaririwa na wahusika 16 wa mtandao kimataifa kuhusu migogoro ya chakula,inayojumuisha Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mpango wa Chakula Duniani(WFP) na Umoja wa Ulaya.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mashtaka ya kuuma dhidi ya kutokuwa na uwezo wa binadamu wa kumaliza njaa na kufikia usalama wa chakula na lishe bora kwa wote ndio ulitolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana António Guterres, mbele ya kukabliwa na data ya Ripoti ya hivi karibuni kuhusu  Usalama wa Chakula Duniani (Gfsr) ambayo inaweka, rangi nyeusi na nyeupe, kuhusu ukweli wa kutatanisha kwa  karibu watu milioni 260 duniani kukabiliwa  na njaa. Kiukweli, ni  milioni 258. Hati hiyo iliyohaririwa na wahusika 16 wa mtandao wa kimataifa kuhusu migogoro ya  chakula, inaojumuisha Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Umoja wa Ulaya(EU),  ambapo inabainisha ukweli kwamba katika muda wa mwaka mmoja tu, walioathirika na uhaba mkubwa wa chakula waliongezeka kutoka asilimia 21.3 mwaka 2021 hadi asilimia 22.7 mwaka 2022, ambapo ni ongezeko la asilimia 1.4. Ni Nchi na maeneo 58 yanayohusika, ikilinganishwa na 53 mwaka 2021, na ongezeko zaidi kwa mwaka wa nne mfululizo.

Migogoro ya kivita inasababisha athari mbaya zaidi

Migogoro mingi ya kivita ndio yenye kuleta athari mbaya zaidi na ambayo kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa yaliyohamasishwa bado ni injini kuu ya migogoro ya chakula, inayohusisha watu milioni 117, hata ikiwa chini ikilinganishwa na mwaka  2021,  matokeo ya zaidi ya mwaka wa vita nchini Ukraine na kukosekana kwa utulivu duniani, mambo mengine yanaongezwa, kama vile mshtuko wa kiuchumi pia unaohusishwa na janga la Uviko-19, ambalo katika miezi kumi na miwili iliyopita limekuwa na athari kubwa hasa katika nchi za Afghanistan, Siria na Sudan Kusini. Na, mwisho kabisa, matukio makubwa ya hali ya Tabianchi ambayo yamekuwa janga kwa karibu watu milioni 57 katika nchi 12. 

Nchi zenye shida kubwa ya baa la njaa kwa sababu ya migogoro

Ripoti hiyo  sasa katika toleo lake la saba inabainisha kuwa Uhaba mkubwa wa chakula, unaleta tishio la papo hapo kwa maisha na maisha ya watu, na kuwafanya kutumbukia katika njaa. Tangu 2016, idadi ya watu wanaoishi chini ya mkazo wa chakula imeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka milioni 83.3 hadi milioni 253 mnamo 2022. Pia inaangazia hali ya muda mrefu ya dharura nyingi. Migogoro kumi kubwa zaidi ya chakula mnamo 2022 iliyoathiri watu milioni 163, ambayo ni asilimia 63 ya idadi ya watu ulimwenguni, kwa mpangilio wa ukubwa ni ile ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Afghanistan, Nigeria, Yemen, Myanmar, Siria, Sudan, Ukraine na Pakistani.

Somalia ipo mwisho

Ni lazima ieleweke, kwamba u haba mkubwa wa chakula, ni pamoja na viwango vya 3 hadi 5 kwa kiwango cha kimataifa: hali hiyo ni moja ya mgogoro, dharura na maafa Somalia iko katika kundi la mwisho, ambapo tangu 2020, kama ilivyo katika Pembe ya Afrika "tumekuwa tukikumbwa na ukame mbaya zaidi katika miaka 40 iliyopita. Hali ya kushangaza ya picha inayotokana na ripoti hiyo inatia wasiwasi zaidi wakati, katika kuichunguza, tunagundua kuwa kuna zaidi ya watoto milioni 35 walio chini ya umri wa miaka 5 ambao wameteseka kutokana na upotevu."

Uingiliaji kati haraka unahitajika bila kuchelewa

Ikiwa Bwana Guterres, katika utangulizi wa hati hiyo amezungumzia hali isiyowezekana, Rein Paulsen, mkurugenzi wa Ofisi ya Dharura na Ustahimilivu ya FAO, amefafanua hali hiyo kuwa inatia wasiwasi sana. Kwa hiyo: Ripoti nne kwa miaka minne mfululizo ilirekodi hali mbaya ya mara kwa mara", alisisitiza  huku akikumbuka hitaji la uingiliaji wa haraka na aina sahihi ya hatua za kuchukuliwa ili kukabiliana na"mgogoro huo. Kwa sababu, "lazima tusingoje hadi iwe ni kuchelewa sana". Mwisho wa mwaka 2023, kuna kunatarajiwa kurudi kwa El Niño ambapo  matokeo yake yanaweza kuwa mabaya zaidi.

05 May 2023, 15:37