Tafuta

Makamu Rais wa Marekani, Bi Kamala ametembelea  Cape Coast nchini Ghana katika lango lilikokuwa linapitia watumwa kwenye ziara yake:Ghana,Tanzania na Zambia(26Machi-2 Aprili). Makamu Rais wa Marekani, Bi Kamala ametembelea Cape Coast nchini Ghana katika lango lilikokuwa linapitia watumwa kwenye ziara yake:Ghana,Tanzania na Zambia(26Machi-2 Aprili). 

Makamu Rais wa Marekani ziarani nchini Ghana,Tanzania na Zambia!

Mamakamu Rais wa Marekani yuko ziarani Barani Afrika ambapo tarehe 28 Machi alitembelea Cape Coast,nchini Ghana,katika lango walipofikia watumwa kabla ya kusafirishwa kwenda Amerika na visiwa vyake.Ni katika ziara yake kwa nchi Tatu ambayo inampeleka Tanzania na hatimaye nchini Zambia aliyoanza 26 Machi hadi tarehe 2 Aprili 2023.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Makamu Rais wa Marekani Bi Kamala Harris alianza ziara yake ya Barani Afrika  kwa Juma moja kuanzia tarehe 26 Machi na atahitimisha mnamo  tarehe 2 Aprili 2023 ambapo  anatembelea nchi tatu kuanzia na Ghana, Tanzania na hatimaye Nchini Zambia. Akiwa nchini Gana mnamo Jumanne tarehe 28 Machi Bi Kamala alifanya ziara yake katika jengo lililokuwa lango la kuwapitisha watumwa waliosafirishwa kutoka Afrika kwenda bara Amerika na visiwa vya Karibeani, lililo katika mji wa mwambao wa Cape Coast nchini Ghana.

Makamu Rais wa Marekani akihutubia Ghana
Makamu Rais wa Marekani akihutubia Ghana
Bi Hariss akitembelea jengo lililohifadhi watumwa
Bi Hariss akitembelea jengo lililohifadhi watumwa

Jengo hilo limewekwa katika orodha mirathi za dunia. Bi Kamala Harris akiwa hapo aliweka shada la maua kwa ajili ya heshima ya watu waliopoteza maisha yao katika biashara mbaya ya watumwa na wakati wa kutoa neno alisema kuwa historia hiyo inapaswa kufundishwa nchini Marekani.

Bi Harris akiwa anatembelea Mwambao wa Cape Coast Ghana
Bi Harris akiwa anatembelea Mwambao wa Cape Coast Ghana
Bi Harris alipewa maua
Bi Harris alipewa maua

Hata hivyo kabla  hapo alitoa hata wito wa uwekezaji zaidi katika sekta ya uvumbuzi barani Afrika huku akielezea matumaini yake makubwa kwa mustakabali wa bara hilo. Tarehe 29 Machi 2023, Bi Kamala anatua Nchini Tanzania na kituo cha mwisho cha ziara yake  barani Afrika kitakuwa nchini Zambia.

Bi Harris akiwa katika maeneo ya soko la utumwa huko Ghana akielekea hata Tanzania na Zambia
Bi Harris akiwa katika maeneo ya soko la utumwa huko Ghana akielekea hata Tanzania na Zambia
Makamu Rais wa Marekani akiwa nchini Ghana na wenyeji
Makamu Rais wa Marekani akiwa nchini Ghana na wenyeji
29 March 2023, 13:26