Tafuta

Manusura wa tetemeko la ardhi huko Siria na Urutuki. Vifo vinazidi kuongezeka lakini hata matumaini ya kuwapata wengine hai kutoka kwenye vifusi Manusura wa tetemeko la ardhi huko Siria na Urutuki. Vifo vinazidi kuongezeka lakini hata matumaini ya kuwapata wengine hai kutoka kwenye vifusi 

Tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Siria:idadi ya vifo inaongezeka!

Idadi ya wahanga wa tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki na Sria Jumatatu iliyopita imezidi 8600.Msako mkali wa kuwatafuta watu ambao bado wamekwama chini ya vifusi unaendelea na wengine wanatolewa wakiwa hai.Mshikamano wa kimataifa wa pamoja na kutuma watu,njia na misaada ya msingi inaendelea.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi inaendelea kuongezeka, nchini Uturuki waliofariki kufikia hadi sasa ni 6,234 kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la dharura la Uturuki la Afad, ambapo zaidi ya 2,400 waliorekodiwa nchini Siria. Makumi ya maelfu walijeruhiwa, ambapo  37,000 katika eneo la Uturuki peke yake, na idadi kubwa isiyojulikana. Wengine hufanikiwa kupiga simu kwa msaada kupitia simu za mkononi pia kutuma video na picha ili kutambuliwa.

Mwanamke na mkewa baada ya kusaidiwa kutoka kwenye vifusi huko Urutuki
Mwanamke na mkewa baada ya kusaidiwa kutoka kwenye vifusi huko Urutuki

Hofu na kukata tamaa, lakini pia hasira ya kuchelewa kwa shughuli za uokoaji kati ya watu wanaosubiri kujua hatima ya jamaa na marafiki kati ya mamia ya mitetemeko ya baadaye. Kwa hiyo inasemakana kuwa watu 8,000 wameokolewa nchini Uturuki kufikia sasa.

Kanisa Kuu la Iskenderun lilianguka kwa sababu ya tetemeko
Kanisa Kuu la Iskenderun lilianguka kwa sababu ya tetemeko

Mshikamano wa kimataifa unaendelea kwa kasi

Rais wa Uturuki Bwana Erdogan ametangaza hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu katika majimbo 10 ya kusini-mashariki mwa nchi hiyo na kutumia mkono wa chuma kukomesha utata huo: watu wanne waliokamatwa na polisi, wakishutumiwa kuwa “ni wachochezi waliolenga kuunda hofu na na kiwewe kwa kuandamana kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya ucheleweshaji wa uokoaji. Hali nchini Siria pia ni ngumu zaidi, ambapo upinzani dhidi ya serikali unashutumu kwamba “mamia ya familia” bado wamenaswa chini ya nyumba zilizoporomoka na juhudi za kimataifa za kutoa misaada zinatimizwa, kama aina ya kufungwa kwa upande wa  Damasco.

Misaada ya kupelekea Siria kufuatia na tetemeko la ardhi.
Misaada ya kupelekea Siria kufuatia na tetemeko la ardhi.

Msaada kutoka NATO na Marekani

Kadiri saa zinavyosonga mbele,  ndivyo utumaji wa misaada kutoka ulimwenguni  kote katika maeneo yaliyoathiriwa, unaendelea kama vile kutoka Ulaya, na hata kutoka Mexico na Venezuela.  Vile vile hata Misaada kutoka NATO imewasili Uturuki, huku Marekani ikielekeza misaada ya kibinadamu zaidi ya yote kaskazini-magharibi mwa Siria, katika maeneo yasiyodhibitiwa na Rais Bashar al-Assad.

Hali ni ngumu sana Uturuki na Siria baada ya Tetemeko, vifo vinazidi kuongezeka
Hali ni ngumu sana Uturuki na Siria baada ya Tetemeko, vifo vinazidi kuongezeka
08 February 2023, 11:27