Tafuta

Utafutaji wa watu ambao bado wamefunikwa na vifusi kutokana na tetemeko kali huko Uturuki na Siria lakini pia kulipuka kwa moto. Utafutaji wa watu ambao bado wamefunikwa na vifusi kutokana na tetemeko kali huko Uturuki na Siria lakini pia kulipuka kwa moto.  (ANSA)

Tetemeko la Ardhi kali kati ya Uturuki na Siria na vifo vingi sana

Tetemeko ka limetikisa kwenye usiku wa manane.Idada ya waathrika inazidi kuongezea na operesheni imeendelea kuwa ngumu kwa sababu ya kulipuka moto na halisi ya hewa.Jumuiya ya kimataifa iko tayari kutoa msaada lakini pia nchi nyingine,wakati katika pwani za Italia kuna hatari ya tsunami.Tetemeko lilisikika pia Israeli na Lebanon.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kwaghafla,mtikisiko wa kwanzaulianza saa 8.17 za usiku wa manane Jumatatu. Kitovu  cha tetemeko la ardhi hasa ni katika mji wa Kahramanmaras, kati ya Uturuki na Siria. Hadi sasa habari kutoka Uturuki na Siria ni za uchungu sana. Inakadiliwa kwamba watu 2,30, lakini itazidi kuongezeka kadiri ambavyo wanaendelea kuchimba na kutafuta waliofunikwa na vifusi.

Makadirio ya watu waliokufa kutokana na tetemeko bado hayaelezeki
Makadirio ya watu waliokufa kutokana na tetemeko bado hayaelezeki

Tetemeko la kwanza ambalo liliendelea zaidi ya 49, lakini ambalo kwalimesababisha maelfu na maelfu ya waathirika. Kwa hiyo sio rahisi kuelezea idadi ya vifo na majeruhi kwa mujibu wa Mkuu wa eneo lakini madhara ni makubwa sana. Watu wanaendelea kutafuta watu ambao bado wamefunikwa na vifusi na sehemu nyingine ya mpaka. Ni tukio la kutisha, ambalo labda wataalamu wa matetemeko, wanabainisha kwamba ni moja yaliyo makuu kwa miaka 100.

Tetemeko baya sana kuwahi kutoka kwa miaka 100 kulingana na wataalamu wa matetemeko
Tetemeko baya sana kuwahi kutoka kwa miaka 100 kulingana na wataalamu wa matetemeko

Kanisa Kuu limeanguka lote na hasa mnara wa kengele, amesema hayo kwa simu Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Paolo Bizetti, akiwa katika  makao yake huko  Iskenderun. Na uaskofu wote na majengo ya kukaribisha yameharibika pia. Shukrani kwa mungu hakuna waathrika katika eneo lakini madhara yake ni makubwa yasiyo elezeka. Hali halisi hiyo ngumu na  bahati mbaya tetemeko la ardhi pia limesababisha moto nchini Siria na Uturuki. Idadi kubwa ya moto katika baadhi ya miji kama picha zilivyoshuhudiwa na pia video zilizowekwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Watu wanachimba kutafuta watu chini ya vifusi
Watu wanachimba kutafuta watu chini ya vifusi

Katika jukwaa la Twitter, matamko kutoka kwa Mwakilishi mkuu wa Kisiasa  wa nchi za Nje Josep Borrell: “Mawazo yeti yanawageukia watu wa nchi ya Uturuki na Siria. Umoja wa Ulaya huko tayari kusaidia.” Israeli, Holand, Umoja wa Mataifa, ni nchi za kwanza kwa kunda mtandao wa msaada wa kutuma katika maeneo yaliyokumbwa ambamo wengi wamehusika katika utafutaji wazalendo ambao hawajapatikana.

Msalaba mwenkundu kutoka Lebanoni wakiwa tayari huko Siria kutoa msaada
Msalaba mwenkundu kutoka Lebanoni wakiwa tayari huko Siria kutoa msaada

Katika mahojiani na Fabrizio Curcio, Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi na usalama kwenyd majanga, na Zima Moto, ametamka juu ya uwezekano wa kuingilia kati: "Tunajitahidi kutoa upatikanaji wa timu zetu na Kikosi cha Zimamoto cha Taifa kuingilia kati. Imeamilishwa na utaratibu wa Ulaya, tumetoa upatikanaji wetu, tunasubiri kuona ikiwa timu hizi zitakubaliwa”. Kwenye ukanda wa pwani ya kusini mwa Italia, wametoa tahadhari ya tsunami kama ilivyoelezwa na Idara ya Ulinzi wa Raia kwa misingi ya takwimu iliyotolewa na Kituo cha Tahadhari ya Tsunami. Kama tahadhari, saa 12.30, hata njia za reli zilikuwa zimekatizwa kuanzia mikoa ya kusini ya Sicilia, Calabria na Puglia nchini Italia.

Tetemeko kali huko Uturuki na Siria limesababisha vifo vingi sana
Tetemeko kali huko Uturuki na Siria limesababisha vifo vingi sana

 

07 February 2023, 10:11