Tafuta

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Chamwino, Ikulu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Chamwino, Ikulu. 

Rais Samia Suluhu Hassan Achangia Ujenzi wa Kanisa la KKKT, Chamwino, Ikulu

Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuchangia milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Chamwino Ikulu. Kanisa limemwandikia Rais Samia barua maalum ya kumpongeza huku KKKT Dayosisi ya Dodoma ikitoa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa.

Na Faustine Gimu Galafoni - Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya Shilingi Milioni 50 aliyoahidi hivi karibuni kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chamwino Ikulu. Akizungumza tarehe 18 Septemba, 2022 kwa niaba ya Rais katika Kanisa hilo mara baada ya kukabidhi hati ya cheti cha udhibitisho wa pesa hiyo iliyotolewa katika Benki ya NMB Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka watanzania hususan Mkoa wa Dodoma kutumia fursa zilizopo ikiwemo mradi wa Treni ya umeme kipande cha Morogoro hadi Makutupora ambao umefikia asilimia 89%. "Rais Samia amenituma nije nikabidhi hati hii kuwa ni Shilingi Milioni 50 tayari zimeshawekwa kupitia akaunti ya 52810010215 NMB yenye jina KKKT UJENZI IKULU CHAMWINO, Rais Samia ametoa hizo fedha kwani ana hofu ya Mungu na anatusihi tuchangamkie fursa zinazotuzungauka" amesema. Hivyo amesisitiza kuwa ni lazima kujitafakari kila mwanadodoma ananufaikaje na fursa za Jiji la Dodoma. "SGR imeajiri watu 6000, Ofisi za Dodoma zipo wazi zitumieni fursa hizo. Aidha, Senyamule amesema kati ya viongozi wanaotaka watanzania waishi kwa haki bila kuonewa ni Rais Samia hivyo na kuwasihi waamini waendelee kumwombea kwa Mungu jambo alilofanya, pia, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha mikakati kabambe Wilayani Chamwino kuwa ni pamoja na miradi ya kilimo maeneo ya kimkakati mawili moja likiwa na hekta 8000 na linafuatia jingine likiwa na hekta 11000.

Rais Samilia anataka watanzania wajenge umoja, upendo na mshikamano
Rais Samilia anataka watanzania wajenge umoja, upendo na mshikamano

Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuchangia milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Chamwino Ikulu. Hivyo, Kanisa limemwandikia Rais Samia barua maalum ya kumpongeza huku KKKT Dayosisi ya Dodoma ikitoa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa. "Mungu ambariki sana Rais wa Tanzania anazungumza kwa vitendo sio kwa maneno, tunaona mwendelezo wa kuhamia Dodoma, miradi mikubwa kuendelea kujengwa ni kwa vitendo" amesema. Pia, amesema kutokana na fedha walizopata kutoka kwa Rais Samia haitawafanya wabweteke huku akiomba kusaidiwa kufanikisha kibali cha ujenzi katika eneo jingine ambalo tayari wameshapatiwa na mmoja wa washirika kwa ajili ya miradi ya Kanisa.  Aidha, amezungumzia umuhimu wa kuweka akiba na tumaini kwa Yesu Kristo. "Unakuta watu wengine wanaweka matumaini na wanafanya maombi makaburini ili wabarikiwe, makaburi hayatoi baraka, jiwekee hazina mbingu kwa kuweka tumaini kwa Mungu" amesema. Amesema mahali pekee penye baraka na neema ni kwa Mwenyezi Mungu Mungu hivyo wakristo wanatakiwa kujiwekea akiba kwake kwani ni hazina kuu.

Waamini wajiwekee akiba kwa Kristo Yesu
Waamini wajiwekee akiba kwa Kristo Yesu

Askofu Kinyunyu amesema watumishi wa Serikali na sekta binafsi nao pia wanatakiwa kujiwekea akiba ili kuondokana na changamoto za kiuchumi pindi wanapostaafu. "Anza kuweka akiba ukijua kuwa miaka 7 za neema na miaka 7 za njaa, usharika anza kuwa na mfuko wa akiba hizi fedha hazitoshi"amesisitiza. Hata hivyo, Askofu Kinyunyu amesema sasa Kanisa limejikita katika uinjilisti wa kutopiga makelele. "Uinjilisti tunaotaka kujikita zaidi ni wa vitendo na si kupiga kelele "amesisitiza. Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amesema suala la usumbufu wa kupata kibali cha ujenzi katika eneo jingine lililotajwa na Askofu lipo ndani ya uwezo wake na atalifuatilia ili kupata ufumbuzi. Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kanisa la KKT usharika wa Chamwino Ikulu   Afisa miradi Dickson Mlela amesema gharama za jengo la Kanisa hilo ni shilingi za Kitanzania Milioni mia tatu ishirini na sita, laki sita sabini na saba elfu na mia Tano (326,677,500). Ikumbukwe kuwa Katika ibada ya harambee ya tarehe 28/08/2022, mifuko ya saruji 236, fedha taslimu Tsh.10,132,000 na ahadi Tsh.17,407,000 ikiwa ni jumla ya Tsh.27,539,000 zilipatikana huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiahidi Tsh.Milioni 50 ambayo imekabidhiwa tarehe 18 Septemba 2022. Hata hivyo, bado kuna upungufu wa fedha kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 144,285,290 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa

 

20 September 2022, 09:06