Tafuta

G20 kuanzia tarehe 30 hadi tarehe 31 Oktoba 2021 zimefanya mkutano wake mjini Roma, kwa kuongozwa na vipaumbele vikuu vitatu: Maendeleo ya watu, Mazingira na Uchumi. G20 kuanzia tarehe 30 hadi tarehe 31 Oktoba 2021 zimefanya mkutano wake mjini Roma, kwa kuongozwa na vipaumbele vikuu vitatu: Maendeleo ya watu, Mazingira na Uchumi. 

Tamko la Mkutano wa G20 Roma 2021: Watu, Mazingira na Uchumi!

G20 kuanzia tarehe 30 hadi tarehe 31 Oktoba 2021 zimefanya mkutano wake mjini Roma, kwa kuongozwa na vipaumbele vikuu vitatu: Maendeleo ya watu, Mazingira na Uchumi. Ni mkutano ambao umejielekeza zaidi katika mchakato wa kukabiliana na changamoto pevu zilizoibuliwa na janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 katika masuala ya afya na maendeleo ya watu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani au maarufu kwa jina la G20 kuanzia tarehe 30 hadi tarehe 31 Oktoba 2021 zimefanya mkutano wake mjini Roma, kwa kuongozwa na vipaumbele vikuu vitatu: Maendeleo ya watu, Mazingira na Uchumi. Ni mkutano ambao umejielekeza zaidi katika mchakato wa kukabiliana na changamoto pevu zilizoibuliwa na janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 katika masuala ya afya na maendeleo, kiasi hata cha kukwamisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu ifikapo mwaka 2030. Kumekuwepo na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta usalama, hifadhi na maisha bora zaidi. Viongozi wa G20 wamewapongeza na kuwashukuru wafanyakazi na wataalamu katika sekta ya afya waliojisadaka bila ya kujibakiza katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Wakuu hawa wameamua kuendelea kushikamana katika kipindi hiki cha kufufua uchumi baada ya kuathirika kutokana na UVIKO-19.

Mshikamano huu, unaelekezwa pia kwa Nchi changa duniani, ili kuzijengea uwezo wa kupambana na UVIKO-19 ambao kwa sasa ni tishio kwa usalama na maisha ya watu wengi duniani. Usalama na uhakika wa chakula duniani pamoja na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote sanjari na usawa wa kijinsia ni mambo ambayo pia yamepewa uzito wa pekee. Viongozi wa G20 wamejielekeza zaidi katika kukuza ulimwengu wa kidigitali, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi na hivyo kupunguza pengo kubwa lililopo kati ya Nchi tajiri zaidi ulimwengu ni zile Nchi changa. Kuhusiana na Uchumi, G20 zitaendelea kuimarisha mchakato wa ukuaji wa uchumi kitaifa na Kimataifa, kwa kuzingatia ushauri ulitolewa na Magavana wa Benki Kuu za Jumuiya Umoja wa Ulaya. Kuhusu Sekta ya Afya lengo ni kuhakikisha kwamba, hadi kufikia mwishoni mwa Mwaka 2021 asilimia 40% ya watu wote duniani wawe wamapata chanjo na hadi kufikia kati kati ya mwaka 2022, kiwango hiki kiwe kimefikia asilimia 70% kadiri ya malengo ya Shirika la Afya Duniani, WHO. Afrika ya Kusini, Brazil na Argentina zitakuwa ni nchi za kwanza kuwezeshwa kutengeneza chanjo na wadau wengine, wanaalikwa ili kuchangia katika mchakato huu utakaowezeshwa pia kwa ushirikiano wa Benki ya Dunia, WB. Shirika la Fedha la Kimataifa, IFM pamoja na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu kufikia mwaka 2030 ni mchakato wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inajizatiti katika kutokomeza umaskini, baa la njaa na magonjwa duniani. Watu wanapaswa kupatiwa elimu bora, kwa kuhakikisha usawa wa kijinsia pamoja na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote. Jumuiya ya Kimataifa inataka kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na upatikanaji wa maji safi na salama; nishati mbadala kwa gharama nafuu pamoja na uwepo wa mipango bora ya miji na makazi ya watu, ili kudumisha usalama na upatikanaji wa maendeleo fungamani ya binadamu. Jumuiya ya Kimataifa haina budi kujifunga kibwebwe kulinda mazingira pamoja na kudumisha amani duniani! G20 zitaendelea kuunga mkono juhudi za Nchi changa duniani katika kupambana na changamoto mamboleo. Ukweli, uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma umepewa mkazo wa pekee. Uhakika na usalama wa chakula duniani ni muhimu sana, ili kuwakumbusha walimwengu kwamba, baa la njaa linazidi kuongezeka kutokana na madhara ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.

Leo hii kuna changamoto kubwa ya ugavi wa chakula kutokana na UVIKO-19, jambo ambalo linawaacha mamilioni ya watu wakisiginwa kwa baa la njaa sehemu mbalimbali za dunia. Utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, umepewa kipaumbele cha pekee, ili kulinda ardhi na bahari dhidi ya athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi. G20 zimeahidi kutekeleza kikamilifu ahadi zake za kuchangia mfuko wa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi sanjari na kudumisha Ushirikiano na mshikamano katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. G20 inahimiza pia mchakato wa kuwajengea uwezo wanawake na wasichana ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo. Ulinzi na usalama katika sekta ya afya unapaswa kuimarishwa zaidi dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Jumuiya ya Kimataifa itambue kwamba, elimu ni sehemu ya haki msingi za binadamu, ili kudumisha usawa hata katika ajira. Changamoto kubwa ya wakimbizi na wahamiaji ni kati ya changamoto zitakazoendelea kufanyiwa kazi kuanzia sasa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama: Shirika la Uhamiaji Duniani, IOM na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Ukuzaji wa sekta ya utalii kimataifa, utamaduni na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi wa mali ya umma ni kati ya mambo yaliyopewa kipaumbele cha pekee na G20 katika mkutano wake wa Roma.

G20 Tamko Roma
02 November 2021, 15:08